Mr. Hillary Mrosso
Founder & Chief Editor

Karibu sana Wildlife Tanzania!

Tunafurahi kukupa fursa ya kujiunga nasi katika safari hii ya kuvumbua na kuelewa zaidi kuhusu maliasili na hifadhi za taifa za Tanzania. Blog yetu inalenga kutoa elimu na maarifa muhimu yanayohusu uhifadhi wa wanyamapori, utalii, na jinsi jamii inavyoweza kunufaika na uwepo wa wanyamapori katika maeneo yao. Tunakualika kujifunza kwa njia rahisi ili kila Mtanzania na mtu mwingine yeyote aweze kuelewa misingi na manufaa ya hifadhi za Taifa na kushiriki kikamilifu katika uhifadhi wa mazingira na maliasili zetu. Kupitia blog yetu, utapata taarifa za thamani zitakazokusaidia kufanya maamuzi sahihi kuhusu maeneo ya uhifadhi na usimamizi wa maliasili. Tunajenga tabia za kizalendo kwa watanzania ili tushiriki kikamilifu katika utalii wa ndani na kuwa walinzi wa maliasili zetu. Kwa wanafunzi na wote wenye ndoto ya kufanya kazi kwenye sekta ya maliasili au kuanzisha biashara za utalii, blog yetu ni rasilimali muhimu ya kukupa mwongozo. Kupitia machapisho yetu, utapata fursa za pekee zinazopatikana kwenye hifadhi zetu na maeneo mengine yenye mvuto kwa watalii. Tunakukaribisha kuwa sehemu ya jamii hii inayopenda maliasili na inayotaka kujenga na kuendeleza urithi wetu kwa vizazi vya sasa na vijavyo. Ni wajibu wetu kushirikiana katika kuweka misingi imara kwa ajili ya kizazi kijacho. Karibu tena, Mtanzania mwenzangu! Twende pamoja katika kuchunguza, kujifunza, na kushirikiana kwa pamoja katika kulinda maliasili zetu. Asante kwa kujiunga nasi!

Habari za Wanyamapori na Uhifadhi

Makala Mpya

Siku ya wafanyakazi duniani

By |May 1, 2024|

Leo ni siku ya wafanyakazi duniani. Tunajua umuhimu wa kazi kwenye maisha yetu. Bila kazi masiaha hayana maana, bila kazi hatuwezi kufikia malengo yetu. Bila kazi hakuna

Ushirikiano Baina ya Viumbe wa Mbugani

By |April 26, 2024|

Kwa kawida wengi hudhani kwamba wanyama wa mwituni wote ni maadui. Lakini leo ningependa nikufahamishe kuwa si wote ni maadui, wapo wanyama ambao hushirikiana kwa pamoja licha ya tofauti zao za kibaiolojia, au hata aina

Kila Kitu Unachopaswa Kujua Kuhusu Reptilia

By |April 25, 2024|

Katika makala zilizopita nilijikita sana katika kuelezea kundi la wanyama jamii ya swala na kwa uchache ndege. Makala ya leo napenda kutambulisha mfululizo wa kundi lingine la wanyama ambao wanajulikana kama REPTILIA (watambaaji).

Makala hii itazungumzia

Sauti ya Dhiki Kutoka Mbugani

By |December 16, 2023|

Ukiwa eneo la Ruaha kusikia sauti nzuri za ndege, fisi, nyani, simba, tembo na wanyama wengine ni jambo la kawaida sana. Pia sio jambo la kushangaa kusikia sauti za viboko wakicheza na kufurahia maji ya