Hakuna wakati mzuri wa kupata taarifa na maarifa kama kipindi hiki katika historia ya dunia, dunia imepitia katika vipindi vingi vyenye zama mbali mbali ambazo ni moja ya maendeleo ya binadamu katika kugundua na kuyafanya maisha kuwa rahisi, njia nyingi na teknologia nyini zimeanzishwa na kufikia hatua nzuri ya kurahisisha badhi ya mambo kwenye maisha. Kwa mfano ugunduzi wa magari, ndege na hata usafiri wa baharini kwa kutumia meli umechangia kwa kiasi kikubwa katika kurahisisha usafiri, uwepo wa simu na intenet umechangia mapinduzi makubwa sana ya taarifa kwenye ulimwengu huu. Hivyo hiki ni kipindi kizuri sana kuishi katika dunia kuliko kipindi kingine chochote kilichopita. Naamini kabisa kuna mambo mengine mazuri yanaendelea kufanyika na kugunduliwa ili kuboresha zaidi na zaidi maisha ya binadamu.
Kama nilivyoanza kwenye utangulizi hapo juu, zama hizi ni zama za taarifa ni zama muhimu sana ambazo kila mtu anaweza kufanikiwa na kufanya chochote anachotaka na kuwafikia watu wowote anaowataka kwa muda mfupi na kwa gharama kidogo sana. Kwenye sekta yetu ya maliasili na utalii hii ni fursa ambayo tunatakiwa kuitumia kwa ubunifu ili kuboresha na kuendelea kuboresha zaidi sekta hii, hasa sekta ya utalii.
Kwa utafiti wangu nimegundua kukua kwa utalii sehemu yoyote ukiachilia uwepo wa miundombinu mizuri, ni kutokana na upatikanaji wa taarifa sahihi wakati wote kwenye maeneo muhimu, pia nimegundua kuwa wanaofanikiwa kukuza na kuwa bora kwenye utalii ni kuwa wabunifu kwenye namna ya kutumia mawasiliano na matangazo kwa njia zote, yani kwa njia ya mtandao na kwa njia nyingine kama vile mabango, kutangaza kupitia TV, majarida na mitandao ya kijamii.
Kwa kiasi kikubwa jamii yetu ya sasa inatumia mitandao ya kijamii katika kupata habari mbali mbali. Hivyo njia nzuri ya kuwafanya watu wapate habari za utalii, vivutio na hata historia za kuvutia kuhusu maeneo fulani imechangia sana kupata kukuza utalii na kujenga au kuongeza uelewa kwa jamii kuhusu maliasili na vivutio mbali mbali. Uwepo wa teknologia na wingi wa njia za mawasiliano na upatikanaji wa taarifa umechangi sana ukuaji wa sekta mbali mbali, nimeona watu wakikuza biashara zao kupitia mitandao ya kijamii, nimeona watu wakifanya biashara kupitia mitandao ya kijamii. Hivyo basi hata taarifa muhimu za kuboresha maliasili na utalii wetu inaweza kukuzwa na kuwa bora zaidi kupitia mitandao ya kijamii.
Nimejifunza watu wanaweza wasiwe na nia ya kujua kuhusu masuala ya utalii na maliasili nyingine. Lakini namna tunavyotaka kuwajulisha ni jambo muhimu, tunatakiwa kuwajulisha watu kuhusu uhifadhi, kuhusu rasilimali tulizo nazo, kuhusu kutembelea vivutio ulivyo navyo. Kazi yetu kubwa ni kuwafanya watu waone sababu ya kutembelea vivutio vya kitalii kwenye maeneo yao. Hata kama hawana utamaduni na nia ya kufanya hivyo kwa sababu ya kukosa hamasa na malezi au tamaduni za muda mrefu zisizosisitza watu kuwa na utaratibu wa kutembelea hifadhi za wanyama au vivutio vingine kwenye maeneo yao. Na sehemu nzuri ya kufanya hivyo ni kwa kutumia vizuri mitandao ya kijamii na njia njingine.
Kwa kuwa na taarifa sahihi kwenye mitando ya kijamii tutakuwa na kundi kubwa la watu wanaohitaji taarifa hizi na watakuwa wanzitafuta na kama watakuwa wanataka kujua kitu fulani basi watatafuta kupitia sehemu hizi. Kila mtu ana haki ya kujua na kujifunza maliasili za nchi yake, kwa mujibu wa katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania kila mtanzania ana haki ya kufahamu, kuhoji, kusimamia na kunufaika na rasilimali za nchi yake. Hivyo basi hili sio jambo la watu fulani tu wanaotakiwa kuelewa na kujua kuhusu maliasili na utalii kwenye nchi yetu, hili ni jambo linalomhusu kila mtu. Na kwa sababu hiyo kila mtu kwa anafasi yake anaweza kuwa chanzo na chachu ya kukua kwa utalii na kuendelea kuwa na uifadhi endelevu.
Tutumie fursa hii ya uwepo wa mitandao mingi ya kijamii kukuza na kuboresha utalii wetu.
Hillary Mrosso
Wildlife Conservationist
+255 683 862 481/+255 742 092 569
www.mtaalamu.net/wildlifetanzania