Ukwei ni kwamba hata kama tuna mali na rasilimali nyingi kiasi gani, kama hakuna usimamizi mzuri hakuna atakayenufaika na rasilimali hizo, usmamizi ni jambo muhimu sana kwenye sekta yaoyote, kwenye biashara usimamizi ni kiu muhimu sana maana ukikosea kwenye usimamizi hata faida hutaiona na utapata hasara mara kwa mara na utashindwa kuendelea na biashara yako. Usimamizi wa jambo fulani sio kazi ndogo, inahitaji nguvu, weledi, ujasiri, ukweli, uaminifu na kujitoa.
Bila usimamizi hakuna kitu kinaweza kwenda vizuri, usimamizi unatakiwa kwenye mambo yote ya msingi, ukianzia na familia zetu mpaka kwenye mali zetu. Kwenye serikali hakuna kitu kinajaliwa na kuangaliwa zaidi kama usimamizi. Ili nchi au serikali ifanye kazi zake vizuri na kufikia malengo yake lazima iwe na wasimamizi wazuri, ndio maana serikali nyingi hubadilisha badilisha wasimamizi ili kuboresha jambo fula ni au sekta fulani. Hii ni kwasababu hakuna maendeleo bila usimamizi. Hakuna kusogea mbele bila usimamizi , hakuana mafanikio bila usimamizi. Usimamizi ni nguzo muhimu katika kuleta maendeleo ya kweli kwenye sekta za maaendeleo, kuanzia maendeleo bianfsi hadi maeneleo ya nchi.
Tanzania ni nchi yenye rasilimali nyingi sana, ambazo zinahitaji simamizi makini na wa uwajibikaji. Kwa mfano sekta ya maliasili na utalii ni sekta kubwa na pana, ina mambo mengi ambayo yote yanahitaji usimamizi makini. Sekta hii ni sekta nyeti kwenye nchii hii, ni sekta inayoongoza kwa kuchangia pato la taifa, ni sekta ambayo inaongoza kwa kuingiza fedha za kigeni katika nchi. Na kwasabau hiyo ni sekta ambayo ina nafasi kubwa sana ya kuendelea kufanya vizuri sana kwa kadri siku zinavyo kwenda, lakini ili iweze kufanya vizuri lazima kuwepo na usimamizi makini na unaowajibika.
Katika sekta hii ya utalii ina vitengo na imegawanyika kwenye idara nyingi ambazo huitaji usimamamizi makini ili kuifanya sekta nzima kuwa na manufaa kwa jamii na kwa taifa kwa ujumla. Kwa mfano kama tunataka kukuza sekta ya utalii Tanzania, tunaakiwa kuhakikisha tunakuwa na usimamizi mzuri kwenye maeneo ya wanyamapori, misitu, utamaduni, miundombinu, mambo ya kale au historia za mambo ya kale, usimamizi mzuri wa mazingira, uongozi mzuri wa kisiasa, pamoja na ushirikiano wa karibu kutoka sekta zote na pia uelewa wa jamii kuhusu rasilimali za nchi yao.
Kila kitu nilichokitaja hapo kina mchango wake kukuza au kuharibu utalii hapa Tanzania, kwa mfano usimamizi wa mazingira ni muhimu sana, kusimamiwa vizuri na wadau na watu wote, kwasababu kama hakuna mazingira mazuri, kama kuna uharibifu wa mazingira, watu wanakata miti hovyo, watu wanachoma misitu hovyo, watu wanaharibu vyanzo vya maji, kama mazingira ni machafu, kama hamna miundombinu mizuri ya maji safi, kama hakuna usimamizi mzuri wa fukwe za bahari, ni wazi kabisa hatuwezi kuwa kivutio kwa watalii na wageni wanaopenda kutembelea sehemu hizi.
Kila kitu kinaweza kuwa kivutio endapo kitathaminiwa na kutunzwa, kwa mfano unaweza kuwa na bustani nzuri ya miti au maua karibu na nyumba yako, bustani hiyo kwa kuwa unaitunza vizuri imekuwa kivutio kwa watu wengi kuja kuona na kufurahia ubunifu wako na uzuri wa bustani yako. Hivyo utapata wageni wengi na unaweza kutengeneza pesa kwa kuwa na bustani nzuri karibu na nyumba yako. Hivi ndivyo ilivo kwenye sekta zote lazima kuwa na usimamizi mzuri makini na unaojitambua ili kuboresha na kuhakikisha rasilimali zilizoko Tanzania au wanazozisimamia zianaleta faida na kutengeneza faida maradufu, hili ni jambo ambalo linawezekana kabisa na lipo kwenye uwezo wetu kulifanya.
Usimamizi ni uongozi, na huwezi kuwa msimamizi mzuri na makini bila kuwa kiongozi mzuri, hivyo basi tuna kazi ya kuangalia kila kitu ambacho tumepewa kusimamia, tuanatakiwa kukisimamia kwa ubora na kuhakikisha kinaleta faida maradufu. Kwenye sehemu yoyote ile hata kama ni nafasi ndogo ya usimamizi kwenye sekta hii ya maliasili na utalii, kumbuka ina mchango mkubwa wa kukuza utalii wetu, hasa utalii wa ndani na utalii wa nje. Hivyo na sisi ambao tunaishi kwenye jamii hii, tunaishi na tumezungukwa na mazingira ya aina nyingi, na kazi yetu kubwa ni kuhakikisha maingira yetu yanakuwa nadhifu na yenye mvuto kila mara, hili ndio jambo ambalo tuanatakiwa kulifanya sehemu yoyote ambayo tupo.
Kwa wale wanao simamia fukwe za bahari, hapa ni muhimu sana, fukwe za bahari huwa zinavutia sana watalii, na Tanzania tumebarikiwa kuwa na fukwe nyingi na nzuri sana kwa utalii, pwani yote ya Tanzania ni maeneo muhimu sana kwa utalii wa pwani na kuona bahari na kupata au kupunga upepo wa baharini. Hivvyo usimamizi mzuri na makini kwa sehemu hizi utachangaia kukuza sana idadi ya watalii wanaokuja kuitambalea Tanzania. Pia jamii yetu inatakiwa kuelimishwa kuhusu manufaa ya fukwe za bahari na jinsi ambavyo zinatakiwa kuwa katika hali ya usafi ili kuvutia watalii .
Asante sana kwa kusoma makala hii, karibu kwa makala yingine muhimu
Ahsante sana.
Hillary Mrosso
Wildlife Conservationist
+255 683 862 481/+255 742 092 569