Tanzania ni nchi iliyo barikiwa sana na uwepo wa vivutio vingi vya kila aina, kuna vivutio vya wanyama, misitu, milima, mambo ya kale, utamaduni na fukwe za bahari. Hivyo karibu kila sehemu ya Tanzania ina vivutio vya utalii. Kati ya vivutio vyote hivyo, vivutio vya wanyamapori ndio hujulikana zaidi na watu wengi kuliko vivutio vyote. Kwa kiasi kikubwa vivutio vya wanyamapori vimekuwa vikitangazwa kila mara na watu wengi wanafahamu kuwa wanyamapori ni vivutio na wanahamasika kutembelea mbuga za wanyama kwa ajili ya kujionea vivutio hivyo.
Ka kwa tuna utajiri wa vivutio vingi namna haii, sekta ya utalii haina budi kuwa na mikakati ya muda mrefu ya kuhakikisha kila sehemu yenye vivutio inatangazwa na kujulikana kitaifa na kimataifa. Utalii wa mambo ya kale na mambo ya kitamaduni ni sehemu kubwa sana ya utalii hapa Tanzania, tuna kila kinachofaa kutufanya kuwa mstari wa mbele kwenye masuala ya utalii.
Kwenye makala hii nitazungumzia kuhusu utalii wa mambo ya kale, mambo ya kale au historia za mabo ya kale ni sehemu ambayo inakuwa na mvuto kitaifa na kimataia endapo itapewa kipaumbele na kutangazwa ipasavyo na vyombo husika. Tanzania ina historia ndefu sana ya mambo ya kale, kuna historia ambazo zimekuwapo tangu karne ya 9, sehemu zenye historia hizi ni sehemu za ajabu sana na zina hadithi za kusisimua kuhusu maisha ya watu waliowahi kuishi sehemu hizi ambazo zina mabaki na historia hii.
Mji wa Kilwa, ni miongoni mwa miji ya ajabu sana katika historia ya maisha ya binadamu, kuna historia ya kusisimua sana kweye miji hii, mji wa Kilwa ni kati ya miji mikongwe sana hapa dunini. Ni mji ambao ulipata mafanikio na kuwa maarufu kutokana na kumiliki biashara ya dhahabu. Mji huu unafahamika kama kitovu cha biashara katika karne ya 9 hadi 15, na 16. Kabla ya ukoloni kuingia biashara kubwa ilikuwa ni dhahabu. Hivyo kwa kuwa mwenye dhahabu ndie mwenye nguvu basi, mji huu wa Kilwa uliendelea kushika hatamu kwa kipindi kirefu sana kutawala sehemu kubwa hadi sehemu za kusini karibia na Zimbabwe.
Kwa kuwa mji huu ulijulikana kama kitovu cha biashara kwa muda mrefu katika pwani ya Afrika Mashariki, kuna maeneo ya mji huu yalijengwa vizuri sana, maeneo hayo yalijengwa na mabaki yake yanaweza kuonekana hadi leo. Meneo ya Kilwa Kisiwani ndio yalikuwa ni kitovu na sehemu kuu ya biashara hii, ambayo hujulikana kama mji wa masultani.
Kukua na kuwa na nguvu kwa mji huu wa Kilwa Kisiwani haukwenda mbali sana, historia inaonyesha katika karne ya 15 mambo yalianza kwenda mrama na mji huu kukosa umaarufu na nguvu kama hapo mwanzo. Mnamo karne ya 16 mji huu ulikuwa tayari chini ya utawla wa Wareno ambao walimiliki kila kitu kwenye mji huu.
Katika historia inaonyesha kuwa baada ya miaka 200 baadaye mji huu wa mji huu ulikuwa kwa kasi kubwa sana na kuwa maarufu zaidi kutona na bishara za watumwa ambazo kwa kiasi kikubwa zilifanywa na waarabu. Hivyo katika pwani yote ya Afrika mashariki sehemu hii ndio ikawa kiini na kitovu cha kusafirishia watumwa kwenda kwenye visiwa vya Mauritania, Reunioni na Komoro.
Kwa mujibu wa historia na vyanzo mbali mbali vya habari za mambo ya kale vinasema mwaka 1870, Kilwa ilikuwa chini ya utawala wa sultani wa Omani, ambaye kwa kiasi kikubwa alimiliki na kuitawala biashara ya watumwa na biashara nyingine kwenye eneo hili.
Kilwa ni sehemu ndogo ya Tanzania, lakini ina maeneo na historia inayoshangaza duniani kote, watalii kutoka duniani kote wanakuja na kujionea historia ya miji huu maarufu katika pwani ya Afrika Mashariki. Hii ni sehemu ya ajabu ambayo utajifunza na kusikia mambo mengi kwa macho yako na unaweza usiamini kama mambo haya yalishawahi kutokea kwenye nchi hii ya Tanzania.
Kilwa ina sehemu nyingi zenye mabaki ya majengo yanye historia ya tangu karne ya 9, hivyo hii ni fursa nzuri kwetu watanzania kwenda kutembelea sehemu hizi na kujionea mambo yaliyopo kwenye mji huu mkongwe wa kilwa.
Kutokana na maajabu ya kusisimua kuhusu maisha ya watu walioishi katika mji huu mkongwe wa Kilwa, kazi walizofanya, na majengo yalijengwa kwa miaka mingi na kuwepo hapo kwa karne nyingi. Shirika la Kimataifa la Elimu na Utamaduni, UNESCO imetaja sehemu hii ya Kilwa kuwa sehemu ya Urithi wa Dunia. Hii ni kutokana na sifa ya kipekee ambayo inapatikana kwenye mji huu. Hvivyo dunia imetambua na kuifanya sehemu hii kuwa sehemu itakayolindwa na kuhifadhiwa kama sehemu muhimu inayoelezea maisha na historia ya biandamu ambao waliishi karne nyingi katika eneo hili.
Ukitembelea Kilwa utakutana na maeneo mengi yenye historia ya kustaajabisha kama sio ya kusisimua. Kuna sehemu nyingi kwenye mji huu ambako kuna mabaki ya majengo makongwe sana. Mfano maeno kama Arab fort au Ngome ya waarabu, Msikiti mkubwa, Msikiti mdogo, kuna Makutani, Husuni kubwa na ndogo. Haya ni maeneo makongwe sana katika mji wa Kilwa, ambayo yamekuwa kivutio kikubwa kwa watalii kutoka nje ya nchi kuja kutembelea sehemu hizi.
Sambamba na hayo kuna maeneo mengine ya Songo mnara ambayo ni eneo lililopo kilomita 8 kutoka Kilwa kisiwani, ni mabaki ya majengo ya kale ambayo yapo hapo kuanzia karne ya 14. Ukitoka hapo utafika Kilwa kivije ambapo ni mji ambao ulipata umaarufu mkubwa baada ya mji wa Kilwa kisiwani kupoteza umaarufu wake na makao makuu ya kibiashara yakahamishiwa kilwa kivinje, hii ni baada ya kuingia kwa utawala wa Wajerumani katika Afrika Mashariki, kuna maeneo ya Mikindani nayo yana historia ndefu sana ya misafara ya biashara ya utumwa.
Naamini umepata mwanga kwa eneo hili moja tulilojifunza leo, la Mji mkongwe wa Kilwa. Tanzania kuna maeneo mengi sana ya kihistoria na yana mambo mengi ya kujua na kujifunza. Uzuri wa maeneo haya ukitaka kutembelea wala hata sio gharama kubwa, ni sehemu unaweza kwenda na kurudi siku hiyo hiyo. Maeneo mengine yapo karibu zaidi na watu wengi hivyo sio ngumu kwenda kutalii kwenye maeneo haya ya kihistoria.
Kuna maeneo yanajulikana sana kwa historia hapa Tanzania, kuanzaia Zanzibar hadi pwani ya Afrka Mashariki yote yamejaa mmbo mengi ya kihistoria, pia unaweza kwenda kutembelea maeneo ya Kondoa irangi, Isimila, Kalenga Bagamoyo, Oldupai Gorge na sehemu nyingine kujua na kujifunza masuala ya kihistoria yaliyopo hapa Tanzania. Huundio utaliiwa mambo ya kale na hapa Tanzania ni sehemu nzuri ya kuukuza na kujua zaidai yaliyokuwa yanafanyika kwenye maeneo haya.
Talii Tanzania, talii maeneo ya kihitoria!
Asante sana!
Hillary Mrosso
Wildlife Conservationist
+255683 862 481/+255742 092 569
www.mtalaam.net/wildlifetanzania