Ustawi wa wanyamapori wetu ni jukumu la kila mmoja wetu. Kwa jinsi viumbe hai wanavyoishi katika mifumo yao ya maisha ni kwamba kila upande unahitaji uwepo wa kiumbe hai mwenzake. Ili kuendelee kuwepo kwa wanyamapori, inahitajika mimea, hewa, maji na hali safi ya mazingira ambayo hayajaharibiwa na shughuli zozote za asili na shughuli za kibinadamu.

Kwa jinsi ambavyo tunaona mwendendo wa wanyamapori na kushamiri kwa biashara haramu ya pembe za faru, meno ya tembo na bidhaa nyingine za wanyamapori ni matokeo ya uepo wa uhitaji wa bidhaa hizi kwenye masoko makubwa ya bidhaa hizi kwenye nchi ya za bara la Asia.

Uhitaji huu wa bidhaa za wanyamapori hawa ndio mwanzo wa biashara zote haramu zinazohusisha wanyamapori na mimea. Dunia inatakiwa kufahamu na kujua kuwa, ujangili hautaisha kwenye bara la Afrika hadi pale ambapo mahitaji na uhitaji wa bidhaa hizi utakapozuliliwa au kufungwa na kutokomezwa, yaani kufunga na kufungia masoko yote yanayojihusisha na biashara hizi.

Wanyamapori wa Afrika hasa tembo na wanyamapori wengine hawana raha kabisa kwa sababu ya kukosekana utulivu kwenye maeneo yao ya asili ambapo hujisikia salama na huishi salama muda wote. Mahitaji makubwa na fedha kubwa wanayopata wanaohusika na biashara hii ni kichocheo kinachofanya biashara hii haramu kuzidi kushamiri hata kwenye sehemu zenye ulinzi mkali ndani ya hifadhi zetu.

Tunatakiwa kuelewa hili wakati wote, endapo mahitaji na bishara ya maeno ya tembo na bidhaa za wanyamapori na mimea itaendelea kutumiwa kwa maslahi ya watu wachache, au zitakuwa zinatumika kuwanufaisha wachache basi, ujue tumekwisha kushindwa vibaya kwenye suala zima la uhifadhi wa wanyamapori, misitu na maliasili kwa ujumla.

Kwa namna yoyote ile, tunatakiwa kufanya kazi kubwa ya kuisaidia jamii yote kwasababu ya uwepo wa wanyamapori kwenye maeneo yao. Tunaposhindwa kudhibiti ujangili tunapoteza matumaini kwa mamilioni ya watanzania na dunia kwa ujumla. Serikali yetu inatakiwa kuwa mbele siku zote na kuonyesha wazi wazi kukabialiana na janga hili la ujangili kwenye hifadhi na mbuga za wanyama.

Ujangili na vitendo vyote vya kikatili wanavyofanyiwa wanyamapori  kwenye maeneo yao ya asili, inawafanya kutengeneza tabia za ajabu na pia kuishi kwa wasiwasi kwenye maeneo yao ya asili.

Asante sana kwa kusoma makala hii.

Hillary Mrosso

Wildlife Conservationist

+255 683 862 481/+255 742 092 569

hillarymrosso@rocketmail.com

www.mtaalamu.net/wildlifetanzania