Habari msomaji wa makala za wanyamapiri na maliasili kwa ujumla, karibu tena leo kwenye makala ya aina yake, makala iliyosheheni hisia za upendo na dhamira safi ya hifadhi wa wanyamapori. Makala hii imeandikwa na mhifadhi Lena, Lena ni mwanafunzi wa mwaka wa pili katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam (University of Dar es salaam, UDSM) anayesoma shahada ya kwanza ya Sayansi ya Uhifadhi wa wanyamapori.

Lena anapenda sana kujifunza, na ana mapenzi ya dhati sana ya wanyamapori, anapenda sana wanyamapori waendelee kuwepo anapenda uhifadhi wa maliasili uendelee kuwepo kwa vizazi vingi vijavyo. Maelezo yafuatayo hapo chini ni maandishi yake yanayoonyesha hisia na mapenzi ya kweli ya uhifadhi wa wanyamapori na maliasili kwa ujumla, ameamua kutushirikisha ili kwa pamoja tuungane naye na kuhakikiha uwepo wetu hapa duniani usaidie kutokuwepo kwa kilio cha wanyamapori.

Kwa fursa hii kubwa na ya ajabu, nikiwa kama mhifadhi chipukizi, Natoa pongezi zangu za dhati kwa Wizara ya maliasili na utalii pamoja na wafanyakazi wake wote kwa kazi kubwa iliyojaa hisia za dhati katika kulinda na kuhifadhi maliasili ikiwemo madini,vyanzo vya maji, mimea pori, wanyama pori pamoja na mazingira yake ya kiasili.

Nikiongozwa na kauli mbiu yangu ya kwanza, “mimi nikiwepo, hutosikia kilio cha wanyama pori”, ambapo hiyo “mimi” haiishii kwangu tu bali kwa mtu yeyote bila kujali kama mhifadhi au sio mhifadhi ambae yupo tayari kushuhudia fahari na maisha halisi ya wanyama pori  katika mazingira yao yanafika miaka ya mbali isiyo tabirika.

Tukiangalia upande wa pili wa kauli mbiu,”…Hutosikia kilio cha wanyama pori”,kivipi???..

-hakutokuepo na masoko makubwa na maarufu ya biashara ya meno ya tembo na pembe za vifaru kama China na nchi nyingine zinazojihusisha

-hakutokuepo na masoko ya maficho yasiyo na kibali ya biashara ya nyama pori (nyama za wanyama pori)

-hakutokuepo na Aina za wanyama ambao wapo hatarini kutoweka duniani kama vifaru na tembo wakubwa wa Afrika

-hakutokuepo na ujangili wa mimea pori, kama miti ya mpingo kwa ajili ya mbao na kutengenezea vinyago

-hakutokuepo na ujangili wa wanyama pori kwa ajili ya mambo ya kitamaduni, kama kuua simba ili aonekane mwanaume mwenye nguvu na kujipatia heshima kwa wanawake

-hakutokuepo na migogoro baina ya binadamu na wanyama pori katika upande wa matumizi bora na mgawanyo sahihi wa ardhi kwa mfano, ardhi kwa ajili ya mbuga za wanyama, ardhi kwa ajili ya mapori ya akiba, ardhi kwa ajili ya vyanzo vya maji, ardhi kwa ajili ya makazi ya watu n.k.

Hitimisho

Sote tunaoona umuhimu wa wanyama pori na kujisikia furaha iliyojawa na msisimko wa amani, tukisema kwa pamoja na sauti zetu ziwe kuu “Mimi nikiwepo, hutosikia kilio cha wanyama pori”, Naamini sauti zetu zitapaa na kufika mbali sana ili tuweze kupata msaada wa kuzuia hayo yote kabla ya kubaki historia ya wanyama pori fulani walikuepo lakini wametoweka.

Tusimame,Tutetee,Tuhifadhi,Tulinde na Tuseme kwa niaba yao.

Asante sana

Lulandala Leena

lulandalaleena@gmail.com

0755369684.