Habari ndugu msomaji wa makala zetu za utalii na uhifadhi wa wanyamapori na mazingira yake. Naamini umekuwa na mapumziko mazuri ya vipindi vyote vya sikukuu za mwisho wa mwaka, hongera sana kuingia mwaka 2019.
Kama ilivyo kawaida yetu huwa tunakuletea makala mbali mbali za uhifadhi, utalii na mambo mengine yanayohusiana na rasilimali hizi muhimu. Lengo la makala hizi ni kutoa elimu, kuhamasisha watanzania kutembelea vivutio mbali mbali vilivyopo hapa Tanzania, lakini pia kushirikiana na mamlaka za uhifadhi wa wanyamapori na maliasili kwa ujumla katika ulinzi, uhifadhi na usimamizi wa maliasili za nchi yetu.
Mwaka 2018 ulikuwa mwaka ambao nilikuwa na ratiba ngumu, ambayo ilinifanya kutoandika makala za kila siku, lakini nilijitahidi kuandika makala chache, nyingi zikiwa za uchambuzi wa mambo mbali mbali yanayoendelea katika sekta hii ya wanyamapori na uhifadhi kwa ujumla hapa Tanzania na duniani kwa ujumla.
Pia napenda kuwapongeza marafiki na waandishi wenzangu ambao wametoa mchango wao wa maandishi kwa kuandika makala nzuri zenye kuelimisha na kutoa uelewa kwa jamii yetu kuhusu masuala mbali mbali ya wanyamapori na uhifadhi wao; kipekee nipende kumshukuru Sadick Omari Kashushu na Amos B. George kwa makala nzuri sana za uchambuzi wa wanyamapori mbali mbali, kwa kweli watu hawa wamefanya kazi kubwa sana, naamini mmekutana sana na makala zao nzuri za wanyamapori kwenye mitandao ya kijamii na kwenye blogu hii ya wildlife Tanzania.
Wengine ni Leena Lulandala na Lucy Romward, hawa ni wanafunzi katika chuo kikuu cha Dare es salaam, wanaosoma masomo yao ya Sayansi ya Uhifadhi wa Wanyamapori mwaka wa pili sasa. Wanadada hawa wamekuwa na mapenzi ya ajabu kwenye uhifadhi na wametoa mchango mkubwa sana kwa makala zao nzuri ambazo tuliziweka hapa, wamekuwa sehemu muhimu sana katika kutoa elimu hii muhimu kwa jamii yetu.
Naamini kabisa kwa kadri siku zinavyokwenda watawaandilia makala nyingine nyingi ambazo tutaziweka katika blogu hii kwa ajili ya kutoa elimu na ufahamu kwa jamii yetu. Pia ifahamike kuwa waandishi wote hawa ni wataalamu wa masuala ya wanyamapori na ndio fani yao kuu waliyosomea, hivyo basi tujiandae kwa makala nyingine nzuri na bora kutoka kwao.
Katika kutoa salamu hizi za mwaka mpya pia napenda kuwashukuru sana wasomaji wote wa mtandao huu wa wildlife Tanzania kwa muda wenu wa thamani kusoma makala zetu tulizoweka katika mtandao huu na sehemu nyingine kwenye mitandao ya kijamii. Kipekee nawashukuru mliopiga simu, kutumia meseji na mlionitumia email zenu kunipongeza, kutoa maoni yenu, kushauri na hata wale walio uliza maswali, ninyi ni sehemu muhimu sana ya kazi hii, na ndio mnaotupa hamasa ya kuandika na kuandaa makala hizi, Mungu awabariki sana.
Napenda kuwaahidi kitu kimoja, bado tupo pamoja na mwaka huu wa 2019, ni mwaka ambao mimi binafsi nitaweka nguvu kubwa sana katika kuandaa makala bora sana za wanyamapori, uhifadhi na utalii, bila kusahau chambuzi mbali mbali za ripoti za kitalaamu. Hivyo nitajitahidi kuandika kila siku. Hata hivyo nakuomba rafiki yangu endelea kufuatilia makala za blogu hii pia endelea kuwashirikisha wengine maarifa haya muhimu kwa pamoja tujenge nchi yetu kupitia sekta hii muhimu ya maliasili na utalii.
Pia napenda kuwakaribisha marafiki na wasomaji wenzangu ambao mnashauku ya kuandika makala za wanyamapori na utalii, hata misitu, msisite kuwasiliana nami, au kama una maoni ushauri maswali, au unapata changamoto kwenye usomaji wa makala hizi karibu tuwasiliane.
Pia hata wale wanaotaka makala hizi ziingie kwenye magazeti, majarida au vitabu vyao, wasisite kuwasiliana na mimi, tupo hapa tufanye kazi pamoja.
Karibu sana rafiki yangu tuendelee kufanya kazi pamoja mwaka 2019.
Uhifadhi, utalii, na ulinzi wa maliasili zetu upo mikononi mwetu.
Hillary Mrosso
+255 683 862 481/255 742 092 569
www.mtalaamu.net/wildlifetanzania