Habari msomaji wa mtandao wako wa wildlife Tanazania, jana katika makala yangu niliyoipa kichwa cha habari, “Habari njema kwa msoamji wa mtandao huu,”nilikuambia nitakuwa na habari njema za kukushirikisha leo, ili tuzifahamu hifadhi za taifa. Hivyo basi makala hii ndio nitakayokuelezea kwa undani juu ya hifadhi ya taifa ya Ziwa Manyara. Hii ni hifadhi niliyoitembelea na kujifunza, hivyo ni hifadhi ninayoijua baada ya kukaa muda wa wiki tatu kujifunza hifadhi hii nzuri. Hivyo msomaji nimeamua kukushirikisha yale ambayo niliyaona na kujifunza katika hifadhi hiii iliyopo kaskazini mwa Tanzania ikiwa ni moja ya hifadhi maarufu sana na yenye kupendwa sana na watu wengi wa ndani na nje ya nchi, kutokana na upekee wake na sifa zake ambazo zimefahamika duniani kote. Nakukaribisha ufuatane nami kuingalia hifadhi hii.
Hifadhi ya ziwa manyara ilianzashwa mwaka 1960, hifadhi hii ina ukubwa wa kilomita za mraba 330 ambapo imepakana na hifadhi ya Arusha upande wa kaskazini. Hii ni hifadhi ambayo imeathiriwa zaidi na Bonde la Ufa kwa eneo la kusini mwa hifadhi hii. Kiini cha hifadhi hii ambacho ndio kimepelekea kuitwa jina hifadhi ya Ziwa Manyara kutokana na uwepo wa Ziwa Manyara upande wa Mashariki, ziwa ambalo lina uasili wa magadi. Hifadhi hii ina idadi kubwa ya wanyama na ndege wengi sana, tafiti zinaonyesha kuna idadi ya jamii zaidi ya 400 ya ndege, ambopo kwa wageni wenye haraka au wenye siku chache wanaweza kuona zaidi ya jamii 100 za ndege. Kwa kuwa leo nilitaka uifahamu hifadhi hii, ngoja nikuonyeshe hatua kwa hatua vivutio muhimu na adimu ambavyo hutavipata katika hifadhi nyingine, vivutio hivi ndivyo vimewafanya watalii na wageni kufunga safari kutoaka nchi mabali mbali dunianina kwa gharama kubwa kuja kuviona.
- Simba wanaopanda miti
Inawezekana ulikuwa unasikia kwamba simba wanapanda miti na huamini, basi kwa taarifa yako simba ambo wanapanda miti wapo Tanzania na wanapatikana katika hifadhi hii ya Ziwa Manyara. Hii ni sifa ya kipekee sana ambayo inaishangaza dunia kwa wanyama hawa kupanda miti, tabia hii ya simba kupanda miti imewavutia wageni na watafiti wengi kutoka sehemu mbali mbali duniani kuja kuona maajabu haya. Asili ya hifadhi hii ni misitu minene na miti mingi aina ya migunga (acacia), na vile vile kutokana na hali ya maji maji kwenye ardhi ya hifadhi hii ndio imesababisha simba hawa kupanda miti; ili simba aweze kuwinda vizuri ni lazima amuone windo lake vizuri, sasa kutoakana na asili ya hifadhi hii kuwa na miti na misitu simba anashindwa kuona windo lake hivyo hiyo huwa ndio sababu ya kupanda juu ilia one windo lake vizuri. Karibu sana hifadhi ya Ziwa Manyara ili ujionee mwenyewe maajabu haya.
- Chemi chemi za maji moto
Ulishawahi kuona maji moto yakitoka chini ya ardhi, basi kama ulikuwa unasoma tu kwenye masomo ya jografia kwamba kuna miamba ipo ndani ya ardhi ambayo hupashwa moto na volcano iliyopo chini ya ardhi, na maji yaliyopo kwenye miamba hii hupata joto sana, hivyo yanapopata nafasi ya kutoka nje kutokana na mgandamizo wa hewa iliyo chini ya ardhi hupasua miamba na kutoka nje au juu ya ardhi na kuwa chemichemi ya maji moto. Haya ndio maajabu yaliyotokea kwenye miamba iliyopo kusini mwa Ziwa Manyara. Katika hifadhi hii kuna chemi chemi mbili za maji moto, ambpo moja ipo kilomita tano kutoka mto Bagayo na inaitwa maji moto ndogo, maji haya ni ya moto na huwa kuna kuwa na gesi huambatana na chemichemi hizi, maji haya ya yana joto linalokadiriwa kufikia zaidi nyuzi za sentigredi 40. Na pia chemichemi ya pili ipo mpakani kabisa mwa hifadhi hii ya Ziwa Manyara ambayo ina nyuzi joto za sentigredi zaidi ya 60. Watu wengi wanaotembelea chemichemi hizi hunawa miguu yao na kuamini ni dawa ya fangasi na magonjwa mengine ya ngozi. Ni sehemu nizuri sana kutembelea, unapofika Manyara usiache kufika hapa.
- Kundi kubwa la Flamingo
Ziwa Manyanya ndio moyo wa ndege hawa duniani kote, kama hamna ziwa Manyara basi hakuna tena Flamingo. Kwasababu asili ya ziwa hili lina magadi, maji ya ziwa hili hayatembei na hivyo baadhi ya mimea na baadhi ya wadudu wanaozalishwa na asili ya ziwa hili huwa ndo chakula kikubwa cha ndege hawa aina ya Flamingo. Ndege hawa wenye mwonekano mzuri na wakuvutia pamoja na staili yao ya kusimama wanapokuwa hapo ziwani huwaacha watu mdomo wazi. Ukiwa kwa mbali kabla ya kufikia karibu na ziwa hili utaona rangi nyeupe na ya kuvutia ya ndege hawa.
- Mji yaliyopo chini ya misitu (underground water forest)
Hifadhi hii mara nyingi huonekana ya kijani kutokana na maji yaliyopo aridhini, ambayo hifanya misitu na hifadhi kuwa yenye majani mengi kwa karibu mwaka mzima. Mwonekano huu wa kipekee huwavutia wageni na watafiti wengi sana kutembelea hifadhi hii ya Ziwa Manyara. Kutokana na kuwa na maji mengi ardhini hupelekea uwepo wa chakula kingi kwa wanyama kama nyani, kima wa bluu na aina nyingine za kima wanaokula matunda na wadudu. Hivyo kuwa na wanyama wengi sana kwa mwaka mzima.
- Miinuko na mabonde ya Bonde la Ufa
Miinuko na mabone yaliyosababishwa na Bonde la Ufa imecha hifadhi kuwa na mandhari na mwonwkano mzuri, ukiwa katika hifadhi hii utaona vimilima na vimiinuko vyenye majani mabichi amboyo huwavutia sana wanyama kama pundamilia na swala, kongoni kuja kula nyasi mbichi kwenye eneo hili. Mwonekano mzuri unapokuwa juu ya mbao ambazo zimejengwa maalumu kwa ajili ya watu wanao tembelea hifadhi hii kuona mwonekano huu mzuri wa miinuko, na tambarare hii ya hifadhi hii.
- Makundi makubwa ya tembo
Kutokana na asili ya hifadhi hii kuwa na maji na chakula cha kutosha karibia mwaka mzima, ni hifadhi yenye idadi kubwa ya makundi ya tembo. Makundi haya ni makubwa sana kuyaona kwa maramoja. Unajua unaweza kwenda kutembelea hifadhi nyingine ukawaona tembo mmoja moja au makundi madogo ya tembo kama kumi au ishirini hivi. Lakini kwenye hifadhi hii hiyo idadi ni ndogo sana. Hapa unaweza kuona zaidi ya hapo. Ili kukata kiu yako ya kuona wanyama tembelea hifadhi hii.
- Ziwa manyara
Jina la hifadhi hii imetokana na uwepo wa ziwa hili pamoja na rasilimali adimu zilizopo kwenye ziwa hili, ndio maana Tanzania imeamua kuweka macho yake pale na kuhakikisha ziwa hili ambalo linalea ndege hawa linahifadhiwa kwa gharama yaoyote. Pia idadi kubwa ya eneo la hifadhi hii limechukuliwa na ziwa hili, Manyara.
Pamoja na hayo rafiki msomaji wangu kwa kuwa nimedhamiria kukueleza mambo yote muhimu ya hifadhi hii, pia nigependa kukushirikisha na vivutio vingine ambavyo vipo nje ya hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara kama ifuatavyo.
- Masoko ya kitamaduni at Mto wa Mbu (curio shops)
Ukifika Arusha ukiuliza mto wa mbu, utafahamu ninachota kukushirikisha. Hapa ni sehemu yenye vitu vingi ambavyo ni kivutio kwa wageni, wanaofika eneo hili. Soko hili lipo karibu sana na hifadhi hii ya Ziwa Manyara, ambapo wanauza vitu mbali mbali vya asili na kitamaduni, utapenda mwenyewe ukifika, kuna kila kitu kizuri cha kuvutia. Utawaona watanzania wakiuza vitu mbali mbali.
- Kwakuchinja corridor
Corridor ni njia ya kupita au kupisha wanyama kutoka hifadhi moja kwenda hidhi nyingine. Hii ndivyo inavyotumika kwenye mambo ya uhifadhi wa wanyamapori . Kwakuchinja corridor ni njia ya wanyama kupita kutoka hifadhi ya Ziwa Manyara kwenda hifadhi ya Tarangire au kutoka Tarangire kwenda hifadhi ya Ziwa Manyara. Corrodor huwa na faida nyingi sana kwa wanyamapori, hvyo kuna watu hawajawahi kuona njia hizi zenye kuunganisha hifadhi na hifadhi. Ukifika manyara utajione mwenyewe kabisa jinsi ilivyo.
- Ranchi ya Manyara
Manyara ranchi ipo katikati ya hifadhi ya Ziwa Manyara na hifadhi ya Tarangire. Ni moja kati ya ranchi bora kabisa kwa Afrika mashariki ambapo inamwonekano mzuri unaovutia wageni kwenda kutembelea na kujifunza mambo mengi kutoka kwenye ranchi hii maarufu sana iliyopo kwenye eneo hili muhumu. Kribu sana hifadhi ya ziwa manyara.
Mwisho, nina mengi sana ya kuelezea lakini nimeamua kukupa hayo niliyoyaona mimi mwenyewe kwa macho yangu, nisielezee sana nikamaliza uhondo wote, ngoja niishie hapa ili siku utakapotembelea hifahi hii ujionee mwenyewe. Cha msingi uwe na kamera yako unapokwenda kutembelea hifadhii maana kuna mambo mengi ungependa upige picha kwa ajili ya ukumbusho wako mwenyewe. Pia hii ni hifadhi rahisi sana kutembele kwa watu wa kaskazini kwani ni gharama nafuu sana hasa gharama za usafiri, ukilinganisha na watu waliopo kusini. Kwa vyovyote vile hata ukitaka kutembelea na unatoka sehemu za kusini, gharama zake sio kubwa ukilinganisha na wageni wengine kutoka nje ya nchi.
Nakutakia kila la kheri katika maandalizi yako ya kutembelea hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara.
Hillary Mrosso
Wildlife Conservationist
0742092569