Mara nyingi kumekuwa na taarifa ambazo tunazipokea kutoka kwa watu mbalimbali kuhusu maisha ya wanyamapori hususani wanyama wanaokua nyama. Miongoni mwa taarifa hizo zinaweza kuwa na ukwel japokuwa zingine hazina ukweli kutokana na uewlewa mdogo juu ya tabia, mwenendo na maisha ya wanyama hawa.Wanyama hawa wapo katika makundi mawili ambayo ; ni wanyama wakubwa wanaokula nyama na wanyama wadogo wanaokula nyama Katika makala hii tutajifunza siri na vita iliyopo baina ya wanyama wakubwa wanaokula nyama kama vile Simba, Chui, Fisi, Mbwa mwitu na Duma. Wanyama hawa wakubwa ni moja kati ya kivutio kikubwa cha watalii wanapotembelea katika maeneo yaliyohifadhiwa. Katika kanuni za kiasilia, wanyama hawa idadi yao ni ndogo ukilinganisha na wanyama wanaokula nyasi.Idadi yao ndogo inawasaidia wanayama hawa wanaokula nyama kuweza kuwinda na kupata chakula chao, kwa muda mfupi na pasipo kutumia nguvu kubwa.
Pamoja na yote hayo idadi yao imezidi kupungua zaidi hata kuhatarisha utoekaji wao duniani. Visababishi ni vingi ambavyo hujitokeza na kujiinua zaidi katika maeneo yao na wakati wanatafuta chakula na sehemu za kuzaliana. Visababishi hivi nimevigawanya katika makundi makubwa matatu ambayo ni (i) miingiliano yao katika kutafuta mahitaji (ii) mwingiliano wao na maisha ya binadamu na (iii) vinavyosababishwa na mawindo yao
Kwa ufupi sana, tuone jinsi wanavyowinda
Simba: Hawa ndio wanyama wkubwa kuliko wote jamii ya paka na huishi katika familia moja ambayo inaweza kuwa na simba hadi 40. Huishi kwa ushirikiano na mara nyingi majike ndo wenye jukumu kubwa la kuhakikisha wanawinda na kupata chakula cha familia nzima. Ushiriki wa simba dume katika uwindaji ni hafifu kulinganisha na jike. Mara nyingi hukaa na kusubiri majike wawinde na kisha wao waende kula. Katika uwindaji wao hutegemea zaidi katika nguvu zao pamoja na kasi japokuwa kasi hiyo haidumu kwa muda mrefu.
Chui: Ni jamii ya Paka ambao wanaishi peke yao peke yao sio kwenye makundi. Mara nyingi hukaa pamoja wakati wa kujamiana yaani jike na dume. Aina hii ya maisha imewafanya wawinde kwa njia ya kuvamia moja kwa moja na baada ya kukamilisha windo lake huweza kulificha juu ya miti ili kukwepa wanyama wengine wanaokula nyama wasiweze kumnyang’anya
Duma: Jamii hi ya wanyama wakubwa wanokula nyama hupenda kusihi katika makundi na hutegemea sana katika uwezo wao wa kukimbia kwani ndiye mnyama mwenye kasi zaidi duniani. Kasi yake katika uwindaji imemsaidia kuweza kufanikiwa japokuwa siorahisi kutokana na sababu nitakazo taja hapo chini.
Fisi: Wanyama hawa hutegemea sana katika uwindaji wa makundi, na uwindaji wao hutegemea zaidi katika uvumilivu mkubwa walionao wa kuweza kubana pumzi kubwa hivyo hawachoki haraka.
Mbwa mwitu: Ni mnyama mwenye uwindaji mbaya zaidi kuliko wanyama wote. Huwinda kwa makundi vile vile kama Fisi, lakini humla mnyama anayewindwa akiwa bado mzima na anapambana kujiokoa. Huyu anakula mkono huyu anakula kichwa mpaka anakufa na hawatumii muda mrefu ni kama dakika 15-20 windo linakuwa limeisha tayari.
Zifuatazo ni sababu za wao kuwa na maisha magumu porini na hivyo imepekea idadi yao kupungua zaidi
Sababu zitokanazo na binadamu;
- Shughuli za kitalii, hii ni sababu moja wapo inayofanya wanyama hawa wawe na mazingira magumu ya kupata chakula chao. Waongozaji wengi wa watalii wamekuwa wakiingilia pale wanyama hawa wakiwa wanawinda na hivyo kuwafanya wanyama hawa kuwashangaa binadamu na au kukimbia na kusababisha kukosa chakula. Mara chache wanyama hawa wamekuwa wakiuawa pindi wanaposababisha usumbufu kwa bindamu na hivyo kuwa miongoni ma sababu ambazo zinasababisha idadi kuzidi kupungua..
Picha kwa hisani ya: www.charlottetravel.com, Ikionyesha gari likiwa kikwazo kwa samba kuwinda
- Kuwauua pindi wanapovamia na kula mifugo ya wananchi.
Baadhi ya wananchi wamejichukulia hatua za kuwaua wanyama hawa pindi wawapo kwenye maenao yao na zaidi sana wakivamia mifugo . Baadhi ya makabila wamekuwa wakiwaua kwa kutumia mikuki lakini wengine wameenda mbali zaidi na kutumia sumu kwenye mizoga hivyo kupelekea kuuwawa kwa aina/ spishi nyingi tofauti zinazotumia nyama na mizoga kama Tumbusi na Fisi.
Picha; Ikiwa Mbwa huyo kauliwa kwa sumu, ni rahisi kwa ndege hao aina ya Tumbusi kuuawa na wao kutokana kwamba wengi wao kutegemea mizoga.
- Magonjwa yatokayo kwa wanyama wa kufugwa
- Wanyama hawa wanapitia wakati mgumu pale wanapo winda mifugo au wanyama wengine wa pori ambao walikuwa na maingiliano nao hivyo kuambukizwa magonjwa kama Kimeta na kichaa cha mbwa ambayo yanaua kwa kasi kubwa na kusambaa haraka.
- Ongezeko kubwa la watu katika maeneo yaliyo hifadhiwa
kumekuwa na ongezeko kubwa la makazi ya watu karibu na maeneo yaliyohifadhiwa. Hivyo upanuzi mkubwa wa matumizi ya ardhi umeongezeka na kupelekea kupungua kwa maeneo mengi yaliyokuwa yanatumiwa na wanyama pori.
Sababu zitokanazo na miingiliano yao katika utafutaji wa mahitaji yao,
- Wanyama wanokula nyama jamii ya samba hususani dume wamekuwa na tabia ya kuuwa watoto wa samba jike ambao sio wa kwake.
Picha kwa hisani ya : www.pinterest.com , mfano jinsi gani Simba dume akivamia familia ya dume mwingine Kuuana kama njia ya kupunguza ushindani, pasipo kujali huyu ni Simba, Chui, Fisi, Duma au Mbwa mwitu. Wanyama hawa wamekuwa wakiuana kati ya aina moja na nyinginei kupunguza ushingani/ uwindaji katika upatikanaji wa chakula chao.
Picha hisani ya : www.reddit.com , Simba akimuuwa fisi.
- Kuuana kama chakula, pia wanyama hawa wamekuwa wakiuana hasa katika nyakati ngumu za upatikanaji wa chakula. Hii inatokea kwa watoto kama watakosa ulinzi wa kutosha na hivyo huwindwa na wanyama wa aina nyingine.
Picha hisani ya www.tripadvisor.com , hapo Chui kamuua Duma kama chakula.
- Kupigana na kuumizana kipindi wanatafuta majike, hii inaonekana zaidi kwa Simba ambapo mara nyingi madume wamekuwa wakipigana na kuumizana na wakati mwingine kuuana wakati wanatafuta majike ili kuzaliana.
Picha kwa hisani ya: www.margotraggettphotography.com
- Ulishaji wa watoto wao na madume, wanyama hawa wamekuwa na mifumo tofauti tofauti ya ulinzi pia katika uwindaji. Simba jike ndo wawindaji hivyo baada ya kuwinda hula pamoja familia na nzima kitu ambacho ni tofauti kwa Mbwa mwitu hawa maisha yao kidogo ni magumu baada ya kuwinda hurudi katika familia zao na hutapika chakula ili kuwalisha watoto wao. Hivyo wawindaji wanakuwa na wakati mgumu sanaaa na mara nyingi huishia kufa kwa njaa.
Sababu zitokanazo na mawindo yao,
- Kuhama kwa mawindo yao, wanyama walao nyama wamekuwa kwenye wakati mgumu pale mawindo yao yanapohama kwa lengo la kutafuta sehemu nzuri kwa ajiri ya kuzaliana na kwenye malisho mazuri. Mfano kuhama kwa nyumbu na Punda milia wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na Ngorongoro kuelekea Masai-Mara, Kenya. Hivyo afya zao zimekuwa zikizoloteka na wengine kufa kwa sababu sio wote wanaoweza kufata mawindo hayo na wengine wanategemea wanyama hao kutokana na urahisi wa kuwawinda.
Picha kwa hisani ya: www.ngorongorocrater.com
- Wakati wmingine wanyaa wanaoliwa wamekuwa wakali hivyo kuwaumiza na wakati mwingine kuwauwa wanyamaya wanaokula nyama. Hii imekuwa ikijitokeza wakiwa wanawinda wanyama wakubwa kama nyati, twiga, tembo n.k lakini pia hata wenye maumbo ya kati mfano punda mbilia, nyumbu na jami nyingine za swala wakiwa wengi sio rahisi kuwawinda hivyo husaidiana kuwafukuza na kuwaumiza wanyama hawa wanaokula nyama.
Picha kwa hisani: www.dailymail.com , Simba akikimbizwa na nyati
Hitimisho; kwa uchache wa makala hii kuna vingi vya kuvifanyia kazi pia nikumbushe kitu hatuhifadhi kwa faida yao tu bali kwa faida yetu sote kwani kila mnyama ana mchango mkubwa katika kusaidia maisha yetu. Mfano kupitia uhifadhi wao tunapunguza madhara ya mabadiliko ya tabia ya nchi pia tunaendelea kufaidika na uwepo wa mazingira asilia yaliyohifadhiwa.
Shukrani za pekee kwa Alphonce Msigwa aliyepitia na kuhariri Makala hii.
Asante kwa kuwa pamoja
Makala hii imeandikwa na Leena Lulandala,
Mwanafunzi UDSM.
Mawasiliano: 0755369684