Fahamu Jinsi Tembo Wanavyoweza Kuwasiliana

Date:

Share post:

Mpendwa msomaji wa Makala mbalimbali  za wanyapori, utalii na mazingira , awali ya yote namshukuru mwenyezi Mungu kwa kutujalia uzima na kutuwezasha kuandaa Makala hii.  Napenda kukaribisha katika makala ambayo inaelezea namna ambavyo mnyama aina ya Tembo anaweza kuwasiliana ikiwa ni pamoja na kutoa ishara mbalimbali. Pamoja na hilo, natoa shukrani kwa kuwa msomaji mzuri wa makala ambazo zinaandaliwa kupitia mtandao huu

Utangulizi

Tembo ni miongoni mwa wanyama wanaovutia na kupendwa na watu wengi duniani huku  muda mwingine amekuwa akiitwa binadamu wa pili kutokana na matendo yake ambayo hufananishwa na binadamu kama vile kuwa na hisia za huzuni, furaha pamoja na uwezo mkubwa wa akili. Mpendwa msomaji, tembo anayo mengi maajabu ila kwa leo kupitia makala hii nipende kukukumbusha haya machache;

  • Ni myama mkubwa kuliko wanyama wote waliopo nchini kavu.
  • Ni myama anayebebeba mimba kwa muda mrefu zaidi (miezi 22) na humyonyesha mototo wake kwa takribani miaka mitano.
  • Ni mnyama mwenye uwezo wa kutunza kumbukumbu kwa muda mrefu sana, na ana uwezo mkubwa wa akili.
  • Ni mnyama anaye hatarishwa na shughuli za binadamu hususani ujangili na shughuli kama kilimo ambazo huchangia  uwepo wa  migigoro kati ya tembo na binadamu.

Njia za mawasiliano katika Tembo

Ulishawahi kujiuliza ni namna gani tembo wanawasiliana, ikizingatiwa tembo huishi katika familia kubwa ambayo inaongozwa na jike mkubwa kwa umri yaani bibi. Tofouti na wanyama wengine ambao tumekuwa kukisikia milio yao ama sauti zao ambazo hutumika kwa mawasiliano kwa tembo imekuwa nadra sana kusikia sauti hizo. Swali ni je inaama Tembo hawawasiliani? Jibu ni hapana

Kama ilivyo kwa nanyama wengine tembo huitaji mawasiliano hususani kwa ajili ya kuhakikisha usalama katika familia zao, kutoa tahadhari hasa pale wanapokumbana ama kuhisi Hali ya hatari, kuongoza wanafamilia, kuomba msaada ama mahitaji na pia mawasiliano kati ya tembo dume na jike ili kuwezesha shughuli za uzazi.

Mawasiliano ya sauti

Watafiti wa tembo wameeleza kuwa tembo hutumia zaidia ya aina 70 za sautiambazo husafiri katika uelekeo tofauti (omnidirectional) na hivyo kuweza kuwafikia tembo wengi  kwa wakati mmoja ikiwemo waliokusdiwa na ambao hawakukusudiwa. Mara nyingi sauti hizi huwa ni za muda mfupi sana hivo ni mahususi kwa ajili ya kutoa taarifa za haraka na ambazo sio za kawaida katika mazingira yao kama vile kutoa tadhari wakati wa hatari. Wanasayansi wamebaini kuwa tembo hutoa sauti za chini ambazo husafiri kwa umbali mrefu sana. Mwanasayansi B. Christy katika chhapisho lake lijulikano kama “What Elephant Calls mean, 2014”  ameonyesha kuwa sauti au milio ya tembo ambao hutofautiana kuanzia za chini ambazo hata binadamu hawezi kuzisikia hadi zile tunazoweza kuzisikia huwa na ujumbe tofauti, na sauti hutolewa kwa kukoroma (snorts), kubweka (barks), miguno (grunts) na sauti mithili ya tarumbeta

Mawasiliano ya ishara

Licha ya kuwa tembo ni mnyama mwenye uoni hafifu, bado hutumia ishara katika mawasilaiano. Hutumia viungo mbalimbali ikiwemo kichwa, mkonge, pembe na mkia kutoa ishara. Mifano ya ishara zitumiwazo na tembo katika mawasiliano ni pamoja na  tembo kusimamisha masikio  na kuyaupigapiga kwa kasi (rapid ears flapping), kukodoa macho huku akiuchezesha mkia wake  upande kushoto na kulia mithili ya mkia wa mbwa ikiwa ni ishara ya furaha au hali ya amani.  Wakati wa hofu, huzuni ama hasira mwili, masikio na macho hupanuka nahuusimamisha mkia wake katika nyuzi 90⁰. Ni vyema zaidi kuchukua tadhari dhidi ya Tembo kwani anaweza kufanya mashambulizi na kumdhuru mtu aliye karibu naye kwa wakati huu.

Picha 1; Tembo mwenye hasira, chanzo Magazine                         

Picha 2; Tembo mwenye Amani: Chanzo; Zambia daily Mail.  Articles/WWF

Mawasiliano kwa njia ya harufi

Njia hii huwa ni mahususi kwa Tembo wanata ambae ni Tembo jike aliye tayari kumpokea dume (receptive female) . Hii hufanyika kwa kuzalisha kemikali (sex pheromones) ambazo hutolewa kupitia mkojo wa Tembo jike. Tembo dume huweza kunusa harufu ya kemikali hizo, na  huchukua mkojo wa jike na kuuweka mdomoni kwa kutumia mkonge na kuulamba mkojo huo. Kitendo hicho kitaalamu kinaitwa  flehemen. Hivyo, kwa namna hii Tembo jike hutoa taarifa kwa dume kuashiria utayari wa kumpokea dume, na kwa kunusa Tembo dume humtambua jike mwenye utayari.

Picha 3; Tembo dume akinusa mkojo wa jike( Chanzo; ResearchGate).

Mawasilaino kwa njia ya kugusana

Tembo hutumia mguso kama njia mojawapo ya mawasiliano kwa kugusana kwa makusudi kwa kutumia mkonge, mkia, masikio na sehemu nyingine za mwili. Njia hii hutumika katika mukutadha mbalimbali ikiwemo; kucheza, hasira, kuhudumiana, kujilinda na hata katika mahusiano kati ya jike na dume. Tembo hutumia mkonge kuashiria salamu au umoja miongoni mwa wanafamilia. Pia Tembo husuguana masikio  kuashiria kucheza au miongoni mwa jike na dume wenye mahusiano. Pia Tembo akiwa na mimba Tembo wengine hutumia mkia kugusa tumbo kama ishara ya kumjulia hali.

Picha 4; Tembo wakisalimiana na kuwasiliana kwa njia ya kugusana Chanzo; elephantsvoices.org

Mawasiliano ya Tembo kuashiria hali ya hatari

Matukio kadha wa kadha ya binadamu kuuwawa na Tembo husikika katika mabara ya Africa na Asia ambapo Tembo hupatikana. Ikumbuke Tembo si mnyama ambaye anapenda kumdhuru ama kumshambulia binadamu. Tembo kabla hajamshambulia au kumdhuru binadamu huonesha dalili za kutofurahishwa na hali hii, kama ukizielewa dalili hizi mapema ni rahisi kujiokoa dhidi ya mashambulizi haya. Yafuatayyo ni mambo yanayofanywa na Tembo kuashiria hali ya hatari;

  • Kugongagonga miguu au visigino chini na kutimua vumbi. Katika hali hii ni vyema kuchukua tahadhari dhidi ya Tembo huyo kwani huashiria kutoridhika na hali.
  • Tembo huyatanua masikio kuelekea pembeni. Tembo hufanya hivi kuonesha namna gani alivyo mkubwa ili kumtisha adui  na kumpa nafasi adui kuchagua kati ya kukimbia au kupambana naye. Ishara hii ni tofauti na tabia ya Tembo ya kugonga masikio kwa ajili ya kuupoza mwili hususani wakati wa joto kali.  Katika hali hii masikio huonekana marefu na sio mapana kama ya Tembo mwenye hasira.
  • Kutingisha kichwa.  Hii ni ishara ya hatari zaidi kwani huonesha utayari wa Tembo kufanya mashambulizi. Kabla Tembo hajamfata adui hutingisha kichwa kwanza na anaweza kufanya hivo mara moja, mbili au tatu.
  • Kusimamisha mkia. Hali ya Tembo kuweka  mkia  usawa wa   nyuzi 90⁰, huashiria hali ya hatari. Huna budi kuchukua tahadhari.
  • Kutoa mlio mithili ya tarumbeta; sauti hii hutolewa wakati Tembo anafanya au anajiandaa kufanya mashambulizi.

Hii ndio tamati ya makala yetu , Pasi na shaka, umejifunza na kufurahia makala hii. Kwa pamoja tuendelee kujifunza na kufarahia mazingira, Wanyama pori na utalii kupitia makala zetu murua.

Asante Sana kwa kusoma makala zetu.

Makala hii imeandaliwa na Lucia Romward, mhitimu Chuo Kikuu cha Dar es salaam katika fani ya Sayansi ya Uhifadhi wa Viumbe pori, na pia imehaririwa na Alphonce Msigwa, Mwikologia Hifadhi za Taifa Tanzania.

Mawasiliano   

Linkedlin; Lucia Levelian Romward

Email; luciaromward@gmail.com ,

Mobile phone +255(0)743927610

10 Comments

  1. Ni makala nzuri… Mungu akujalie sana unapokuwa unaendelea kufafanua kwa watu wengi tusiojua mambo mengi zaidi kuhus wanyama pori na tabia zake mbalimbali katika mazingira yao na nje ya mazingra yao.

  2. Keep on because wildlife issues was being taken as a nonsense matters so we as a youth we have to wakeup and anounce our heritage

    • Very sure Rhino Fausta, we need at least to raise the awareness concerning our valuable natural resources, because most of Tanzanian don’t know what is going on in our wildlife and other natural resources. So our work is to make this information accessible to them in a very simple language. You are most welcome Fausta and thank you for Feedbacks

  3. Tunashukuru sana kwa kuweza kutujuza na kutugundisha mambo mengi kuhusu wanyamapori hususani kwa Lugha yetu hii inadhihirisha ukomavu wa uzalendo wako pamoja na kutaka jamii yetu izidi kujifunza na kuelewa zaidi tabia za wanyama wetu hii itasaidia sana jamii zetu hasa zinazopakana na hifadhi zetu kujikinga na kuchukua hatua pindi waonapo dalili hizi hatimaye migogoro itapungua .Asante sana na uendelee kutuelimisha

    • Hakika, sisi kama wahifadhi wenye ujuzi na weledi katika sekta hii tunatakiwa kuyafanya mambo yote muhimu yanayoonekana kuwa magumu yawe rahisi na ujumbe uliokusudiwa kuwafikia walengwa ambao ni watanzania. Hivyo ndio kusudi la blog hii na kuhakikisha tunatoa maarifa na ujuzi wetu katika kutetea na kulinda maliasili zetu adhimu kwa njia hii ya uandishi na kupeana maarifa na ushauri. Nakushukuru sana Mwanga kwa mrejesho huu, naamini hata mwandishi wa makala hii atafarijika na kutenga muda wa kutosha kuandaa makala nyingine bora zaidi kwa ajili ya kutoa elimu kwa jamii yetu. Pamoja sana Mwanga.

Leave a reply

Please enter your comment!
Please enter your name here

spot_img

Related articles

Safari ya Hillary Thomas Mrosso Katika Uhifadhi wa Wanyamapori Tanzania

Wakati nasoma elimu ya msingi na sekondari, nilikuwa na ndoto za kuwa daktari wa binadamu, hivyo nilipenda sana...

Zijue Sababu za TAWIRI Kukataa Matokeo ya Utafiti wa Duporge na Wenzake Kuhusu Idadi ya Nyumbu Katika Eneo la Serengeti – Masai Mara,...

Uhifadhi endelevu wa wanyamapori unahitaji tafiti za kina za mara kwa mara kwa kutumia mbinu sahihi zilizohakikiwa ili...

SHAIRI: Tutunze Makazi ya Simba

1.Ndugu zangu karibuni, nina jambo kutamka Simba wapo hatarini, majangili wawasaka Waharibu masikani, kuvuka yao mipaka Simba wanayo thamani, tutunze makazi...

Shairi: Agosti kumi ya Simba

Leo twendeni mbugani, utalii mbuga zetu Huko leo kuna nini, nataka ninene kitu Leo huko duniani, siku ya bingwa wa...