Mbwa mwitu wa Afrika (African wild dog), ni mnyama jamii ya Kanivora (carnivorres) kwa maana ya wanyama wanaokula nyama . Wanyama hawa wana mdomo mrefu na kucha zisizoweza kujificha (unsheathed claws). Katika kundi hili la mbwa mwitu kuna wanyama pia kama mbweha (fox) mbweha masikio (bat eared fox). Vile vile wanyama hawa wana  meno marefu ambayo husaidia wakati wa uwindaji na wana vidole vinne katika miguu ya mbele.

Mbwa mwitu ni mnyama ambae asili yake ni porini na anapatikana katika bara la Africa tu na ni tofauti na watu wanavvodhani kwamba wana asili moja na mbwa wa majumbani bali wana utofauti mkubwa sana kitabia na namna wanvyoishi ,kwani watu wengi wanadhani mbwa mwitu wana asili sawa na mbwa wa majumbani na badae kwenda kuishi mwituni (tabia inaitwa feral)

Mbwa mwitu wa Afrika amekuwa akidhaniwa kuwa ni mwindaji katili sana, je ni kwanini? Kabla hatujajua zaidi kuhusu tabia hii, basi hebu tujifunze kidogo kuhusu tabia za mbwa mwitu

 Maisha na tabia za mbwa mwitu wa Africa

1.Mbwa mwitu wa Afrika ni hodari katika uwindaji na ustadi mkubwa  kwani wanauwezo mkubwa  wa kunusa, kuona hasa nyakati za usiku (japo hawawindi sana usiku), pia uwezo wa kusikia sauti mbali mbali. Mbwa mwitu wote huwinda sawa, maana wanaumoja wa hali ya juu sana.

2. Mbwa mwitu wa Africa wanaishi katika kundi ambalo baba na mama ( alfa male and female) huongoza familia yao. Mbwa mwitu hawana ndoa za mitala yaani mahusiano yao yanahusiana na baba na mama mmoja tu (monogamous).  Watoto wanaozaliwa , jike anaruhusiwa kuhama na kwenda kutafuta dume sehemu nyingine, huku dume anabaki kuendeleza ukoo au kundi(pack).

Pichani: Mbwa mwitu wa afrika wakiwa  katika Kundi, wamepumzika

3.Mbwa mwitu wa Afrika, hawana mipaka ya kuishi kwani hawana makazi ya kudumu, bali wanatulia sehemu moja pale tu mbwa jike akizaa ili kulinda watoto wanaishi katika bonde au eneo fulani ( den). Mpaka watoto wakue ndipo wataanza kuhama hama. Hawalindi mipaka kama ilivo kwa mbweha miraba na mbweha masikio

4.Mbwa mwitu wa Africa dume anahusika katika kulea watoto kwa kwenda kutafuta chakula ili jike aweze kunyonyesha watoto. Baada ya hapo   wanauwezo wa kucheua chakula walichokihifadhi tumboni ili kuwalisha wengine mfano watoto na wale wasiojiweza kuwinda kwa nyakati Fulani. Vile vile  wanauwezo wa kufukia chakula chini na kutumia chakula kwa muda mwingine na alama kama harufu ya mkojo hutumika kutambua alipofukia chakula.

Pichani: Mbwa mwitu akicheua chakula alichokihifadhi tumboni

5.Pia mbwa mwitu kila mmoja ana mpangilio wa kipekee wa rangi na madoa  ya ngozi zao hivyo kutambuliwa kirahisi kundini. Mbwa mwitu wa africa wanapojamiiana dume na jike wanageuziana mikia (tail to tail position)  hii kwa sababu dume huchelewa kutoa mbeguna hivyo kumfanya jike kubana uume wa dume mpaka akisha mwaga mbegu( uume wa mbwa una kirungu kinaitwa bulbourethral gland). Hivyo wakigeuziana mikia husaidia kujilinda na kumaliza tendo salama kwani hujamiiana mara moja tu.

6. Wanapiga kura kwa chafya ili kutoa maamuzi ya kulala, kupumzika, kuwinda, au kupambana na adui. Hivyo kwenye kundi  kiongozi ndiye atakae angalia idadi ya mbwa wengine waliopiga chafya ili kutoa maamuzi.Mfano  wakipiga chafya kwa wingi na kwa nguvu wakiona windo hii hutoa ishara ya kwenda kuwinda, hivyo kiongozi huamrisha kundi ili kuwinda mara moja na wote huvamia windo. (Jaribu kumchunguza hata mbwa wa nyumbani kukiwa na hatari huwa anafanya kama kupiga chafya, je hii ni kwaida ya mbwa au  ni lazima)

Pichani : Mbwa mwitu wakipiga kura kuchagua kuwinda au kupumzika Je ni kweli mbwa mwitu ni wawindaji katili ( cruel) ?

Fahamu kuwa mbwaa mwitu  ni muwindaji hodari na  ana ustadi mkubwa sana, kama ilivyo kwa wanyama jamii ya paka yaani samba (Lion), simbamangu (caracal), duma)Cheetah) , chui (Leopard), mondo (Serval) nk.  Watu wengi tunafikiria kuwa mbwa mwitu ni muwindaji katili, kwa sababu  huwa wanasabisha kifo chenye maumivu endelevu kwa windo lao.  Kwani wanauwezo wa kumla mnyama hata kama bado mzima, kwa kumtafuna na kung’ata sehemu nyeti za windo kama vile tumbo, korodani na miguu ili kufanya windo asiweze kutembea au kukimbia. Hali hiihusababisha windo kutoka damu nyingi na kupoteza nguvu hadi kufa.

Sababu zinazofanya Mbwa mwitu awinde kwa namna hii;

  •  Umbo dogo la walilonalo wanyama hawa hutumika  kumparua kidogo kidogo  kwa kumzingira mpaka mnyama (windo) kudondoka chini, Mfano swala, pundamilia na nyumbu na kisha kuanza kumla mnyama akiwa bado mzima, tabia hii ipo hata kwa fisi.
Pichani : Mbwa mwitu wa kila mnyama akiwa bado mzima

  •  Miguu yao ya mbele haina nguvu ya kumdondosha mnyam au windo kwani kucha zao haziwezi kushikilia vizuri windo lao. Hii ni tofauti na wanyama jamii ya paka kama simba ambae huwa wanang’ata shingo na kusababisha kifo kwa mnyama.
Pichani :mbwa mwitu wakiwinda Pundamilia.

Kutokana na sababu hizo watu wengi wamekuwa wakimuita mbwa mwitu muwindaji mkatili, lakini jibu nia HAPANA,  kwani anavyowinda na kuuwa windo lake ni sawa na wanyama wengine utofauti ni namna wanavyowinda.

 Mbwa mwitu wa afrika hatarini kupotea.

Baadhi ya athari ambazo mbwa mwitu wa Africa wanakumbana nazo na kusababisha idadi yao kuzidi kupungua na kupotea kwenye baadhi ya maeneo ni kama ifuatavyo;  Kupotea kwa makazi yao, kutokana na kutumia eneo kubwa kwa ajili ya uwindji na maisha yao ya  kwa kuhama hama.

  • Magonjwa kutoka kwa mbwa wa majumbani kama kichaa cha mbwa, canine distemper, kuhara damu (Parvo virus)
  • Uwindaji haramu, mfano kutega mitego ya waya ( snares)  Kwa ajili ya wanyama kama swala, lakini mbwa mwitu hunasa na kufa,Endapo ikitokea mmoja haonekani kundini basi mbwa mwitu hurudi kumtafuta hivyo kunasa tena kwenye mitego
  • Migogoro kati ya watu na wanyama, watu wanaamini kuwa mbwa mwitu ni wakatili hivo wakionekana katika maeneo karibu na makazi ya watu , wanawauwa kwa imani kuwa ni waharibifu wa mifugo na wakatili

Mwandishi wa makala:

KAMANGA SHADRACK ANDREA

 Mawasiliano: 0678577786

Email: bigstarshadrack@gmail.com