Habari rafiki, karibu tena leo tushukuru kwa jambo hili zuri lililofanywa na Clouds 360, lililofanyika kwenye hifadhi za Serengeti na Hifadhi ya Mamlaka ya Ngorongoro. Ni jambo zuri sana kuwahi kutokea hapa Tanzania hasa kwenye vivutio vya hifadhi zetu. Nilifurahia sana kipindi hicho ambacho nilijifunza mengi sana kutoka kwa watu waliokuwa wanahojiwa na Cloud pamoja na mahojiano mengine, hii ndio sababu iliyonifanya kukaa chini na kundika makala hii ili kupongeza kipindi hichi kilichorushwa na Clouds 360 ndani ya hifadhi zetu.
Katika kuhakikisha utalii wa ndani unakua hii ni njia moja wapo nzuri sana kutumiwa ili kutangaza uhifadhi na utalii wa ndani, tunaweza kukutana na wakuu wa mahoteli na wakuu wa hifadhi husika kwa ajili ya kuelezea kwa Watanzania umuhimu wa kutembelea hifadhi za Taifa, hii iendane sambamba na kutaja viingilio na sehemu za kulala na kula vyote vinatakiwa kuwa wazi kabisa kwa Watanzania ili wajipange kwenda kutembelea hifadhi za wanyamapori na maeneo mengine yenye vivutio. Hivyo walichokifanya Clouds na wadau wengine kwenye kuutangaza utajiri wetu kwetu wenyewe na kwa watu wengine imekuwa ni jambo bora sana, pia hata lugha iliyotumika ni lugha inayoeleweka kwa Watanzania wengi hivyo kwa wale ambao walitazama kipindi hichi walielewa na naamini walifurahia pia.
Nilipokuwa nasikiliza maongezi na mahojiano haya nilijifunza mengi ambayo Watanzania wengi hatuyajui, (mengi ya mambo hayo niliyaandika kwenye makala ya jana) ambayo tungeyajua mapema naamini tungebadilika jinsi tunavyochukulia mambo ya utalii nchini kwetu. Tumesikia mambo mengi sana ambayo tunatakiwa kuyafanyia marekebisho kwenye sekta hii ya utalii, kuna mambo ya miundombinu na masuala ya kodi yanatakiwa yawe ya moja kwa moja yafanyike kwa njia rahisi na isiyo na mizunguko inayokatisha tamaa.
Tanzania kuna hifadhi za taifa 16 ambazo nyingi hazijulikani kabisa na Watanzania wengi, hasa hifadhi za Kusini mwa Tanzania zimekuwa zikisahaulika sana kwenye kuzitangaza, naamini walichokifanya Clouds kwenye hifadhi za Serengeti na Ngorongoro watakifanya pia kwenye hifadhi hizi za Kusini ambazo ni Hifadhi ya Ruaha, Hifadhi ya Katavi, Hifadhi ya Gombe na hifadhi ya Uduzungwa. Hizi ni baadhi tu ya hifadhi nyingi za Kusini mwa Tanzania ambazo zina vivutio vingi sana na pia kuna utajiri mkubwa sana ambao watu hawajaujua. Mazingira mengi ya hifadhi hizi za Kusini hayajaharibiwa na pia n sehemu ambazo bado wanyamapori wake wanatabia za kiasili kabisa kutokana na kutotembelewa mara kwa mara na wageni.
Naamini safari hii Clouds 360 watafanya kazi kubwa sana kwenye hifadhi hizi za Kusini, kuzitagaza na kuwafahamisha Watanzania kuwa wao ndio wageni na walengwa wa kwanza kwa kutembelea hifadhi hizi, Watanzania wanatakiwa kuambiwa na kuelimishwa sana kuhusu uhifadhi wa wanyamapori na pia umuhimu wao kutembelea hifadhi hizi.
Natanguliza shukrani zangu za dhati kwa jambo hili muhimu la kutangaza hifadhi zetu kwa Watanzania wote, napenda kuwaambia kwamba kwa kufanya jambo hili ni uwekezaji mkubwa sana kwenye maisha ya Watanzania, na wala sio kupoteza pesa bali tunafanya jambo lenye manufaa makubwa kwa watanzania na nchi yetu kwa ujumla, kwani tunajenga na kuweka jambao hilinkwenye akili za Watanzania ili wawe na utamaduni wa kutembelea hifadhi na maeneo ya vivutio. Hivi ndio njia ya moja kwa moja ya Watanzania kushiriki kwenye ukuaji wa uchumi wa nchi kupitia utalii wa ndani. Timu nzima ya Clouds na nawadau wengine kwa kushirikiana na serikali hongereni kwa kazi hiinzuri mlioanzisha, tupambane mpaka tuikamilishe na tuifanye kwa ufanisi mkubwa.
Ashanteni sana, natamani na mimi ningekuwa mmoja wapo wa timu hii ya Clouds 360, hasa kwenye kipindi hichi cha kutangaza utalii wetu wa ndani. Naomba makala hii ya kushukuru iwafikie wote hasa serikali, mamlaka ya hifadhi za Taifa, timu nzima ya Clouds 360, na watanzania wote.
Hillary Mrosso
Wildlife Conservationist
0742092569/0683248681
hillarymrosso@rocketmail.com