Tunavyo Tegemeana Kwenye Mazingira
Lazimu tukubaliane na ukweli kwamba kila alichokiumba Mungu kipo kwa sababu maalumu, na kina faida kwa uwepo wake hapo kilipo. Hakuna ambacho hakina maana kwa viumbe hai wote walioumbwa na Mungu kila kitu kina maana yake ya kuwepo. Changamoto yetu kubwa ni kutokujua sababu ya uwepo wa kitu hicho, hivyo hupelekea matumizi na maamuzi yasiyosahihi kwa mtumiaji.
Uwepo wa maliasili zetu zenye thamani kubwa ni jambo ambalo kama nchi tunajisifia na kumshukuru Mungu kwa kuruhusu wanyama hawa na maliasili hizi kuendelea kukaaa hapa. Tunazungukwa na mandhari nzuri sana iliyopambwa na hali nzuri ya hewa na ya utulivu iliyochangiwa na uwepo wa misitu na mapori mengi sana yenye kuvutia na kuifanya nchi yetu kutokuwa kati ya nchi zisizoathiriwa na hali ya jangwa .
Kwa asilimia kubwa vitu hivi vinachangia kwa kiasi kikubwa muendelezo wa maisha ya binadamu hapa duniani. Kwa mfano mwadamu ili aweze kuishi anahitaji hewa ya Oksijeni ambayo hutolewa na uwepo wa miti ya kutosha kwenye maeneo yetu. Na ili mimea iendelee kukua na kujitengenezea chakula chake unahitaji hewa ya kabonidayoksaid ambayo hutolewa na binadamu na kutumiwa na mimea. Hivyo kuendelea kuwepo kwa wanyama wanaokula nyasi na majani unategemea binadamu. Vilevile jinsi ambavyo majani yanakuwa mengi na yakutosha yanavutia kwa kiasi kikubwa wanyama kama wa aina mbali mbali, wanaokula majani na wanao kula nyama.
Tunapotunza wanyama hatutunzi tu wanyamapori bali tunatunza na hata mazingira yanayosababisha uwepo wa wanyama hawa. Hivyo inakuwa tunaweza kutengeneza uwiano mzuri kati yetu na wanyama hawa. Tunataka serikali, wadau na wanajamii ya kuwa mradi huu ni muhuimu ni jukumu letu muhimu sana.
Sisi kama wadau wa mazingira na maliasili zote Tanzania tunatakiwa kujifunza tabia za hawa watu kwa kuishi nao karibu. Tuwaonyeshe namna ya kukaa na kuchukuliana na wenyema .
Makala hii imeandikwa na
Hillary Mrosso
0742092569

