Habari msomaji wa makala za blog za wildlife Tanzania, karibu kwenye makala ya leo ambapo tutajifunza mambo mazuri sana ambayo tunapaswa kuyajua kuhusiana na wanyamapori wetu. Wanayamapori wetu pamoja na rasilimali nyingine zilizopo kwenye hifdhi zetu zina faida na umuhimu mkubwa sana kwa nchi na dunia kwa ujumla. Leo nimekuandalia makala hii kuhusu CITES, inawezekana ni neno jipya sana kwako, hujawahi kulisikia sehemu yoyote ile, sasa leo utaelewa kabisa nini maana ya CITES, malengo yake, kazi zake, na ilianzishwa mwaka gani, na utajua nani ni washirika wake. Hivyo kwa kuanza ni vizuri tukaelewa moja kwa moja hapa.  CITES (Conversion on International Trade in Endengered Species of Wild Fauna and Flora). Hiki ndio kirefu cha CITES.

Nini maana ya CITES?

Kwa taarifa mbali mbali nilizosoma kwenye vyanzo mbali mbali vya habari, kama vitabu na kwenye majarida na makala mbali mbali, pia kwenye mitandao ya internet nimepata maana yake kama nitakavyoeleza hapa chini, CITES ni makubaliano, au mapatano ya serikali za nchi mbali mbali duniani kuhusu biashara ya kimataifa ya viumbe hai walio hatarini kutoweka, kama wanyamapori na mimea. Hivyo haya ni makubaliano baina ya serikali. Kwa kuwa biashara hii ya viumbe hai ni biashra inayovuka mipaka ya nchi moja kwenda nchi nyingine, hii ndio sababu kubwa ya kuwa na washiriki wengi watakaoweza kusaidia kwenye suala hili ili kunusuru viumbe hai hawa.

CITES ilianza lini?

CITES ilianza miaka ya 1960, kutokana na mikutano ya kimataifa inayojadili masuala mbali mbali ya kufanya marekebisho ya biashara ya wanyamapori kwa makusudi ya kuimarisha uhifadhi wa wanyama na mimea mingine iliyopo porini. Lakini ilianza kuingia kwenye utekelezaji rasmi ilipofika Julai 1 mwaka 1975

Malengo  ya CITES ni nini?

Kutokana na matukio mengi yenye viashiria vya kila aina ya kutoweka kwa viumbe hai ambavyo huchangiwa na bishara ya spishi za wanyama na mimea, ndio iliyopelekea kuanzishwa kwa makubaliano haya kwa nchi na serikali za nchi mbalimbili. Ili kwa pamoja washirikiane kudhibiti biashara  haramu za wanyama na mimea. Hivyo lengo kuu ni kushirikiana kulinda na kuhakikisha wanyama na maliasili nyingine muhimu zinzendelea kuweopo kwa vizazi vingi vijavyo. Hivyo mpaka sasa kuna nchi washiriki 183, ambao wamekubaliana kwa pamoja kudhibiti biashara ya viumbe hai isiyo na manufaa.

Kwa ripoti mbali mbali za kitafiti kuhusu biashara na usafirishaji wa spishi, wanyama na hata sehemu za wanyama kama vile ngozi, meno, pembe, kucha, na manyoya inakadiriwa kuwa ni zaidi ya mabilioni ya dola za Kimarekani ambayo inatokana na mauzo ya mamilioni ya rasilimali hizi. Kwa kuangalia jinsi biashara na mauzo yanavyokwenda kwa kasi nchi zote wanachama hukutana na kukubaliana baadhi ya mambo muhimu ya kuzingatia na kuepuka ili kunusuru kuendelea kupotea na kutoweka kwa wanyama na mimea. Hivyo kati ya maazimio walioyaweka ni kuidhibiti kabisa masuala ya usafirishaji au uuzwaji wa viumbe hai mwitu kwenye nchi zao na mipaka yao. Kwa sababu jinsi watu wanavyoongezeka, mabadiliko ya tabia nchi, kuharibika kwa kiasi kikubwa cha mazingira na makazi ya viumbe hai, tena ukichanganya na biashara ya viumbe hai, inatishia sana uwepo wa viumbe hawa. Hii ndio sababu kuu ya kuwa na nchi wanachama wengi ili kudhibiti hali hii isiendelee kushamiri kwenye makazi na hifadhi zetu.

Kutokana na hali hiyo ya nchi kutoa ushirikiano ili kulinda wanyama wasiendelee kusafirishwa bila kuwa na manufaa makubwa. Hadi sasa CITES wamezuia kabisa biashara na usafirishaji wa viumbe hai zaidi ya 35,000. Hii ni hatua kubwa sana ya kuhifadhi wanyamapori wetu. Wanyama kama tiger na tembo ambao ndio wameathirika zaidi kwa mujibu wa ripoti na za CITES, kwa sasa wanaweza kulindwa na nchi zote wanachama. Ili kuzuia kabisa biashara za ngozi, meno, kucha, nk.

Kwa nchi kujiunga na CITES sio lazima, na pia nchi zote zilizojiunga na CITES huitwa kwa kingereza Parties, au wanachama, nchi wanachama. Kwa kadri siku zinavyokwenda tutajifunza zaidi kuhusu wanayama na mimea ambayo ipo kwenye CITES na pia tutajifunza jinsi inavyofanya kazi. Ili kujua mambo haya kwa undani usiache kufuatilia mtandao wako wa wildlife Tanzania . Nyingi ya taarifa hizi unaweza kuzipata kupitia website yao www.cites.org

Asante sana kwa kusoam makala hii,

Hillary Mrosso

Wildlife conservationist

0742092569/083248681

hilllarmrosso@rocketmail.com

www.mtalaamu.net/wildlifetanzania