Habari ndugu zangu Watanzania, Nawashukuru kwa kusoma na kuwa wapenzi wa mambo yote yanayohusu Wanyamapori, Utalii, na mambo ya Kale. Napenda kuchukua nafasi hii kuwakaribisha katika ukurasa mpya wa Facebook wenye jina la Wildlife Tanzania. Nimeamua kuanzisha ukurasa huu ili kutoa elimu hii na maarifa mbali mbali kwa watu wengi zaidi. Kwa utafiti nilioufanya kwa muda wa miezi michache nimegundua watu wengi sana hasa Watanzania tunapenda mambo ya Wanyamapori mambo ya Utalii na vivutio mbali mbali. Hii imenipa moyo na hamasa ya kuyaweka maandisha haya kwa lugha ya kiswahili ili Watanzania wengi waelewe mambo yote muhimu kwenye sekta hii ya Maliasili na Utalii.

Lengo la ukurasa huu ni kutoa Maarifa, Elimu na kuhamasisha Utalii wa ndani sambamba na kupata taarifa muhimu ambazo zitatusaidia kwenye suala zima la uhifadhi wa mazingira na maliasili zetu. Ninaaminin kabisa kupitia elimu tutakayokuwa tuanaipata kupitia ukurasa huu tutaweza kujenga upya mitazamo yetu tuliyonayo kuhusu mambo yote ya utalii na vivutio.

Hivyo ninayofuraha kubwa kukukaribisha kulike na kucoment kwenye ukurasa huu wa Wildlife Tanzania. Nakuahidi utapata taarifa za kutosha na sahihi kila siku. Ili kwa pamoja tuwe kwenye msitari mmoja wa kukuza Utalii wetu na kupinga na kuzuia kabisa vitendo vya ujangili wa wanyama na maliasili nyingine.

Hiki ndio kitu ninachofurahia kukifanya siku zote, hivyo mshirikishe na mtu mwingine kuhusu ukurasa wetu wa Facebook unaoitwa Wildlife Tanzania. Huu utakuwa ndio ukurasa wa nyumbani, tutajifunza sana hapa, tutaulizana maswali na pia tutasoma makala zitakazo chapishwa kwenye ukurasa huu.

Karibuni sana marafiki zangu wote wa facebook, karibuni kwenye ukurasa huu, namkaribisa kila mtu. Karibu sana Watanzania, karibu sana Watu wote.

Ungana nami kuitangaza Tanzania

Ungana nami kupinga ujangili

Ungana nami kuhamasisha utalii wa ndani

Ungana nami kuhifadhi mazingira yetu

Kwa pamoja tujenge kizazi cha kizalendo.

Asanteni sana

Hillary Mrosso

Wildlife Conservationist

+255683 862 481/+255742 092 569

hillarymrosso@rocketmail.com

www.mtalaam.net/wildlifetanzania