Habari Rafiki, karibu  kwenye makala yetu ya leo, tunaangalia jinsi ambavyo serikali inavyoweka msisitizo kwenye baadhi ya maeneo, ili kuwe na uelewa wa mambo kwa watu wote. Dodoma ni kati ya mikoa yenye watu wengi kwa sasa, pia ni kati ya mikoa inayokuwa kwa kasi sana kwa miaka ya hivi karibuni hii ni kutokana na serikali kuweka maamuzi ya dhati ya kuhamia Dodoma. Pamoja na juhudi kubwa hizi Shirika la Hifadhi za wanyama TANAPA halikuwa nyuma kwenye juhudi hizi kubwa, wametoa ofa kwa wakazi wote wa mkoa wa Dodoma kutembelea hifadhi za Tarangire na Ruaha. Hii ni hatua nzuri sana ya kuwawezesha watu kuwa na uelewa na kutembelea hifadhi za wanyama za Tanzania.

Dodoma ni makao makuu ya nchi ya Tanzania, kuna mambo mengi sana ya kiserikali yanafanyika Dodoma, kuna mambo makubwa yanafanyika hapo na yanapangwa kufanyika kwa siku za baadaye. Ni mkoa ambao kwa sasa utakuwa na mchanganyiko mkubwa wa watu, kutoka kila kona ya nchi ya Tanzania. Wengi watapenda kuishi Dodoma sio kwasababu ya serikali kuhamia huko bali kwa sababu ya fursa ambazo zipo na zitakazojitokeza kwa ajili ya mwingiliano mkubwa wa watu. Hili ni jambo zuri sana kwa maendeleo ya nchi yetu.

Sababu ya kuandika makala hii ni kuwataka na kuwahamasisha Watanzania walioko Dodoma kuwa na kiu ya kutembelea maeneo ya vivutio vya kitalii. Hii itakusaidia sio kwa kufurahia tu kuona wanyama na vivutio vingine bali kuona FURSA ambazo zipo ndani ya sekta hii ya wnyamapori au sekta hii ya utalii. Hivyo kwa wale wanaopenda kujifunza ni vema wakapanga kuwepo kwenye safari hii ya kwenda kutembelea hifadhi za Tarangire na Ruaha. Kwa hifadhi nyingi za kusini mwa Tanzania bado hazijajulikana na hazina watalii wengi, hivyo ni sehemu nzuri ya kufikiria kuwekeza.

Hivyo kama unaangalia fursa kwa siku zijazo, anza sasa safari yako ya kitalii ili uongeze ufahamu wako kwnye uwekezaji kwenye eneo sekta hii. Hata kama huna mpango wa kufanya biashara kwenye maeneo haya, we nenda tu katembelee hifadhi hizi. Utajua na kujifuna mengi sana.

Wakazi wa doodoma msiwe nyuma kwenye hii fursa ya kutembelea hifadhi za Tarangire na hifadhi ya Ruaha, ni ofa iliyotolewa maalumu kwa ajili yenu. Mnatakiwa kuonyesha mfano kwa mikoa mingine kwenye hili jambo. Hivyo mnatakiwa kuonyesha hamasa na kiu ya kutembelea hifadhi hizi ili kwa siku za baadaye TANAPA warudie tena Ofa hii ya kutembelea hifadhi kwa mkoa wa Dodoma, hivyo jipange jiandae, mwambie na Rafiki yako au ndugu yako kuhusu fursa hizi. Kwa maelezo zaidi uliza kwenye banda la Maliasili na Utalii, kwenye maonyesho ya Nanenane, yanayoanza tarehe 28/07/2017 hadi 07/08/2017.

Karibuni sana hifadhini, USISAHAU KUCHUKUA KAMERA YAKO!

Hillary Mrosso

0742092569/0683248681

hillarymrosso@roketmail.com