Habari wasomaji wetu wa makala za blog ya wildlife Tanzania.
Tunamshukuru Mungu, tumevuka salama mwaka 2024. Sasa tupo mwaka 2025.
Napenda kuwashukuru sana wasomaji wetu wote wa makala hizi.
Napenda kushukuru wote mliotutumia jumbe zenye kututia moyo kwenye kazi zetu hizi za uandishi.
Napenda niwashukuru wote waliotoa mapendekezo ya namna ya uandishi wa makala zetu na pia kutuuliza maswali mbali mbali. Yote yamekua ni maoni mazuri ya kuborsha kazi zetu hizi za uandishi.
Mwaka 2024, tuliandika makala kadhaa ambazo zimekua na mchango kwenye kutoa elimu ya uhifadhi na utunzani wa mazingira.
Nawashukuru sana waandishi wote wanaoandika makala zao na kuchapisha katika blogu yetu ya wildlife Tanzania.
Tuna mambo mengi na makala nyingi nzuri tumeziandaa kwa ajili yam waka 2025. Hivyo usiache kufuatilia na kujifunza kupitia makala hizi.
Kuna mambo mengi yanatokea hapa duniani, kama vile mabadiliko ya tabia nchi, uharibifu wa mazingira, ujangili na kusambaa kwa mimea vamizi ambayo imekua ni janga kubwa kwenye uhifadhi wa maliasili zetu.
Kazi yetu kama waandishi ni kukujuza kuhusu mambo mbali mbali yanayotokea kwenye uhifadhi wa masliasili zetu. Kuna wanyama na viumbe hai wengi wanaendelea kupotea hata bila kujulikana kama wapo. Hii ni kwasababu za ukosefu wa taarifa na tafiti, uharibifu wa mazingira ya asili pamoja na uwindaji haramu wa wanyamapori na viumbe hawa.
Kwa upande wa ikolojia ya majini, bado kuna ukosefu wa taarifa nyingi, na hatujui mambo mengi kwababu ya tafiti chache na pia watu wanaopenda kujifunza mazingira ya majini na ikolojia yake ni wachache.
Kupitia blogu hii tutaenda kujifunza na kupata taarifa nyingi kuhusu uzuri na umuhimu wa hifadhi ya bahari na viumbe hai wengine wanaoishi majini.
Tanzania tubarikiwa kuwa na hifadhi nyingi, za majini kama vile maziwa, mito, bahari na maeneo ya ardhi oevu. Tunaweza kujifunza na kutoa elimu ya uhifadhi wa maeneo haya muhimu hapa hapa kwenye blogu yetu.
Karibu sana mwaka 2025, tuendelee kushirikiana na kujifunza mengi kuhusu uhifadhi, utalii, mazingira nk.
Asante sana, nawatakia kheri ya na baraka za mwaka 2025.
Hillary Mrosso