Kasa wa bahari ni reptilia wa order testidunes, familia ya chelonida. Kuna aina saba ya spishi za kasa wa bahari duniani ambazo ni flatback sea turtle, kasa wa kawaida (Green Sea turtle) ,kasa ng’amba (hawksbill sea turtle), kasa Leatherback Sea turtle), Kasa Duvi (loggerhead sea turtle), kemp’s ridley na Kasa Kigome(Olive ridley).

Kasa wa kijani; picha na Westend61 – Gerald Nowak/Brand X Pictures/Getty Images

Katika spishi hizo saba Tanzania tumebarikiwa kuwa na spishi aina tano isipokua flatback na kemps ridley. Flatback kasa anapatikana Australia na hivo kupewa jina kasa wa Australia na kemps ridley anapatikana katika bahari ya Atlantic na pia ni kasa wenye umbo dogo zaidi kuliko kasa wengine. Katika IUCN red list amechapishwa kua ni spichi ya kasa ambayo ipo hatarini kutoweka.

Kasa wamegawanyika katika makundi mawili ambayo ni kasa gamba gumu na kasa gamba laini, katika spishi saba za kasa, spishi sita wana gamba gumu na spishi moja ya kasa ina gamba laini (leathery-shelled sea turtle).

Kasa gamba gumu, chanzo cha picha; https://turtleowner.com/how-hard-is-a-turtle-shell/

Kwa spishi zote saba za kasa, jike na dume wana umbo sawa hivo sio rahisi kuwatofautisha jinsia kwa haraka. Kasa jike hua na mkia mrefu tofauti na kasa dume, pia kasa jike ana uwazi kwenye cloaca (cloacal opening)

Muonekano wa aina za Kasa gamba laini; Chanzo cha picha kutoka katika mtandao; https://reptilehere.com/turtles/species/types-of-softshell-turtles/

SIFA ZA KASA

Kasa gamba laini ana umbo kubwa kuliko kasa wote, ana urefu wa mita 1.4-1.8 na uzito usiopungua kilogramu 500, kasa wa kijani ni kasa wa pili kwa ukubwa, ana urefu wa mita 1-1.2 na uzito kuanzia  kilogramu 65-130, kasa Olive ridley ana  urefu wa  mita 0.6-0.7 na uzito wa kilogramu 36-49, kasa hawks bill ana urefu wa mita 0.8 na uzito wa kilogramu 45-68, kasa longerheadana urefu wa mita 0.9 na uzito wa kilogramu 113, kasa flatbackana urefu wa sentimita 76-96 na uzito wa kilogramu  70-90, kasa mdogo kuliko wote ni kasa kemp’s ana urefu wa sentimita 68-82 na uzito wa kilogramu 33-45.

Kasa wana patikana katika bahari zote isipokua bahari ya Antantika, hutaga mayai nchi kavu, ufukweni mwa bahari. Mayai yao huanguliwa baada ya siku 45-70, hutegemea hali ya hewa,tafiti zinaonesha kua jinsia ya kifaranga cha kasa hutegemea hali ya joto, joto kali kifaranga kinakua cha kike na hali ya ubaridi kifaranga hua na jinsia ya kiume.

 Baada ya kifaranga kutotolewa hurudi baharani;  na kasa wa miaka mitatu hadi mitano huishi juu ya magugumaji (seaweed) kwaajili ya kujipatia chakula, malazi pamoja na maji. Kasa akifika umri wa kutaga mayai husogea ufukweni mwa bahari, ambapo kasa jike hutaga mayai katika fukwe maalumu hutembea umbali mrefu baharini na kurudi katika fukwe ile aliyototolewa katika kipindi cha kutaga mayai (nesting season).

Vitoto vya kasa baada ya kuanguliwa kwenye moja ya fukwe za Tanzania; Picha hii imetolewa https://rove.me/to/tanzania/sea-turtle-hatchlings, picha imepigwa na Kelvin Lunham

Spishi tano za kasa zilizopo katika fukwe za Tanzania ni spishi mbili tu ambazo hutaga mayai yao katika fukwe za Tanzania,  kuanzia mwezi wa nne mpaka mwezi wa sita ambazo ni kasa wa kijani na kasa hawksbill                                                   

Ukomavu wa kuzaliana wa kasa hutofautiana kutokana na spishi zao Kemps na olive ridley hupevuka kuanzia miaka 10, loggerheads, hawksbill, flatbacks na green sea turtle hupevuka kuanzia miaka 20 hadi 50 na leatherback kuanzia miaka 15 ambapo kasa jike na dume hujamiana kuanzia umri huo.  

CHAKULA

Kasa longerhead, kemps ridley,olive ridley,na hawksbill  maisha yao yote hula majani na nyama kama vile nyasi za baharini, magugumaji, konokono ,minyoo na samaki.  Upande wa kasa wa kijani hubadili chakula kutokana na umri wakiwa wadogo hula majani na nyama, na akiwa na miaka 20 na hula majani pekee( herbivorous), leathery sea turtle hupendelea sana kula jellyfish pia  kupunguza .

KASA NA UTALII

Kwa nini kasa huvutia watalii?

  1.  Uzuri wa Kipekee: Kasa wana gamba la kuvutia lenye rangi na mifumo mbalimbali. Kutoka kwa kasa wa kijani wenye ganda la kijani kibichi hadi kasa wa ngozi wenye gamba la ngozi laini, kila spishi ina uzuri wake wa kipekee.
  2. Umuhimu katika Mfumo Ikolojia: Kasa ni sehemu muhimu ya mfumo ikolojia wa bahari. Wanasaidia kudhibiti idadi ya viumbe vingine baharini na kueneza mbegu za mimea ya bahari. Kufuatilia kasa kunatoa fursa ya kujifunza zaidi kuhusu afya ya bahari.
  3.  Uzoefu wa Kipekee: Kuona kasa wakiogelea baharini, wakijichimbia mchanga, au wakitaga mayai ni uzoefu wa kipekee ambao huwezi kupata mahali pengine.
  4. Uhifadhi wa kasa: Watalii wanaweza kushiriki katika shughuli za uhifadhi kama vile kusafisha fukwe, kuondoa mitego ya uvuvi, au kufuatilia kasa.

Watalii wakifurahia kuogelea na kucheza na kasa.

Faida za utalii wa kasa:

  1. Uhifadhi: Utalii wa kasa husaidia kuongeza ufahamu kuhusu umuhimu wa kulinda kasa na mazingira yao.
  2. Maendeleo ya jamii: Utalii wa kasa unaweza kuunda ajira na kuongeza mapato kwa jamii za mitaa.
  3. Utafiti: Fedha zinazopatikana kutoka kwa utalii wa kasa zinaweza kutumika kufadhili utafiti kuhusu kasa.

Changamoto za utalii wa kasa:

  1.  Usumbufu kwa kasa: Idadi kubwa ya watalii inaweza kusababisha usumbufu kwa kasa, hasa wakati wa kutaga mayai.
  2. Uchafuzi wa mazingira watalii wanaweza kuacha uchafu ambao unaweza kuathiri afya ya kasa na mazingira yao.
  3. Uvuvi haramu: Uvuvi haramu bado ni tishio kubwa kwa kasa.

Asante sana kwa kusoma makala hii. Makala hii imeandikwa na Perpetua na kuhaririwa na Hillary Mrosso, ukiwa na maswali, maoni au ushauri kuhusu makala hii, usisite kuwasiliana na mwandishi wa makala hii kwa mawasiliano hapo chini.

Makala hii imeandikwa na

Perpetua Nyagwaswa

perpetuanyagwaswa@gmail.com 

0763815640