Habari Rafiki, karibi kwenye makala zetu za kila siku kuhusu wanyamapori na uhifadhi wao , leo tutajifunza kuhusu Swali moja niliulizwa na mama mmoja aliyekuwa ni ofisa wa serikali, aliniuliza kwanini kusiwe na maduka maalumu kwa ajili ya kuuza nyamapori kwa watanzania ambao wanapenda nyama hizo? Ni swali ambalo lilinifikirisha sana na jinsi alivyokuwa anaelezea niliona kuna haja ya kufanya jambo kama hili kwa nchi ya Tanzania.
Tanzania ni moja ya nchi duniani zenye idadi kubwa sana ya wanyamapori wa kila aina, kutokana na kuwa na idadi kubwa ya wanyamapori serikali iliamua kutenga maeneo ya kutosha kwa ajili ya hifadhi ya wanyamapori hawa na mazingira yao. Maeneo tofauti toauti yalitengwa na Serikali kwa ajili ya kuhakikisha maeneo haya yanaendelea kuhifadhi wanyamapori na mimea maeneo haya yamegawanyika kwenye makundi mbali mbali, kuna maeneo ya hifadhi za Taifa, kuna maeneo ya mapori ya Akiba, kuna mapori Tengefu, kuna maeneo Oevu, na maeneo ya mapori ya wazi, pia kuna maeneo ya mapito ya wanyamapori (corridors) yote haya ni kwa ajili ya wanyamapori na yapo kweney usimamizi wa serikali kuu na serikali za vijiji au serikali za mitaaa.
Kutokana na hali hii kuna maeneo mengi ya hifadhi za taifa ambayo shughuli za uwindaji wa aina yoyote ile hauruhusi na wala haufanyiki, lakina maeneo mengine ambayo yapo chini ya Idara ya wanyamapori Tanzania kuna sehemu wanaruhusu uwindaji kwa mashrti na vigezo vya sharia za uwindaji Tanzania na sharia za uhifadhi wa wanymapori Tanzania.
Miaka ya nyuma serikali iliamua kupunguza idadi ya wanyamapori kwenye badhi ya hifadhi na kuamua kuwauzia wananchi kwenye maeneo maalumu. Kwahiyo ieleweke kwamba waliamua kuuza nyamapori kwa sababu ya kufanya pruning au kuwapunguza wanyamapori baada ya kuwa wamezidi kwenye maeneo yao na wengine hata kusababisha usumbufu kwa jamii. Kwa hiyo kulikuwa na siku na maeneo ambayo wanachi walipata kitoweo cha nyamapori kwa ajili ya afya zao. Yule aliyeniuliza swali aliniambia kwamba nchi kama Kenya na Nabibia wanafanya hvyo, kwamba wana maduka maalumu kwa ajili ya kuuza nyamapori, na hivyo kuwapa wananchi kitoweo.
Kuna siku za hapa karibuni niliongea na afisa mmoja wa siku nyingi kutoka Idara ya wanyamapori Tanzania, nikamuuliza swali hilo, akaniambia miaka ya nyuma jambo hili lilikuwa likifanyika kwa makusudi ya kupunguza wanyamapori kweneye baadhi ya maeneo ya hifadhi zao. Lakini kwa sasa jambo hili haliwezi kufanyika tena kutokana na kukithiri kwa UJANGILI kwenye maeneo ya hifadhi za wanyamapori. Hivyo serikali imeamua kusitisha na kutofanya jambo hilo kwa kuwa ni muhimu wanyamapori wakaishi kwa asili yao bila kubugudhiwa na aina yoyote ya shughuli za kibinadamu. Hili ni jambo zuri na la hekima kufnyika na serikali yetu ili kunusuru wanyamapori na rasilimali zetu.
Asante sana kwa kusoma makala ya leo, namini ume elewa, pia karibu kwa maswali, maoni, mijadala na maboresho kwenye jambo hili, niandikie hapo chini.
Ahsante sana!
Hillary Mrosso
Wildlife Conservationist
+255 683 248 681/+255 742 092 569
www.mtaalamu.net/wildlifetanzania