Kwa wale ambao tunafuatana vizuri leo ni sehemu ya tatu kwenye ichambuzi wa sheria hii ya wanyamapori ambapo tunaangali masuala mazima ya mpangilio na mfumo usimamizi au uendeshaji kwenye sekta ya wanyamapori (institutional Arrangement and Administration) kwa kufuata matakwa ya sheria hii. Hivyo karibu twende pamoja hatau kwa hatua tujue majukumu ya Mkurugenzi wa wanyamapori kwa mujibu wa sheria hii.
Kwa makala iliyopita tuliishia kifungu cha 6, leo tutaendelea na kifungu cha 7 hadi kifungu cha 8. Ambavyo vina mambo yafuatayo;
- Sheria hii inasema kutakuwa na Mkurugenzi wa wanyamapori ambaye atakuwa ni ofisa katika utumishi wa umma aliyeteuliwa kulingana na sheria ya utumishi wa umma.
- Mkurugenzi atakuwa ni mtumishi wa umma ambaye amekidhi vigezo vya kitaaluma na kuwa na maarifa ya kitaalamu katika sayansi ya wanyamapori. Hapa anamaanisha Mkurugenzi wa wanyamapori anatakiwa awe na elimu na maarifa ya kutosha kuhusu kazi ambayo ataifanya ya uhifadhi wa wanyamapori, hivyo anatakiwa kuwa ni mtalaamu wa sayansi ya wanyamapori.
- Mkurugenzi atakuwa ni ofisa ambaye atahusika na kusimamia Idara ya wanyamapori.
- Mkurugenzi atakuwa ndiye mshauri mkuu kwa serikali kwenye mambo yote yanahusiana na uhifadhi na usimamizi wa wanyamapori na rasilimali za wanyamapori na atasaidiwa na maafisa wanyamapori, wasimamizi wa wanyamapori na askari wanayamapori.
- Mkurugenzi atateua maafisa wanyamapori wanaofaa kuwa watoa lesseni kwa kusudi la sheria hii. Kipengele hiki kina maanisha kwamba Mkurugenzi anaweza kuteua mtu yeyote mwenye uwezo na anayefaa kwa mujibu wa sheria hii kuwa mtoa lesseni kwenye mambo mbali mbali atakayopangiwa na mkurugenzi.
- Mkurugenzi anaweza, kwa kutoa taarifa kwenye Gazeti la Serikali, au kwa maandishi, anaweza kuweza kuwa na wawakilishi kwenye majukumu yake ambao ni wasaidizi wake kwa , Kamanda wa Kikosi cha kuzuia Ujangali cha Kanda, Afisa wanyamapori wa Wilaya, Afisa wanyamapori mapori ya Akiba, msimamizi wa hifadhi na ofisa yeyote mwenye mamlaka. Hapa anamaanisha mkurugenzi anaweza kugawanya madaraka yake au majukumu yake kwa wasaidizi wake ambao watamsaidia kufanya majukumu hayo kwa mujibu wa sheria.
- Pale ambapo mtumiaji wa kifungu cha (6), baadaya ya kupewa madaraka ya kumwakilisha mkurugenzi kwenye majukumu yake, itatakiwa kuwe na ushahidi wa kutosha wa kupewa majukumu hayo, na pia na mtu huyo sahihi yake itaonekana na atafanya hivyo kwa sehemu ya mkurugenzi.
- Waziri anaweza, kwa kushauriana na mamlaka husika na kwa kufuata sheria zilizoandikwa, atasababisha kuanzishwa kwa mamlamka ya wanyamapori ambayo itakuwa huru na ambayo muundo wake na majukumu kwa kiasi kikubwa yataangalia ulinzi, usimamizi na uongozi wa rasilimali za wanyamapori nje ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro na Hifadhi za Taifa na itakuwa na uwezo wa kutekeleza na kutimiza masharti ya kimataifa yanayohusiana na uhifadhi wa wanyamapori kwa kuungana katika makampuni hayo kwa kusudi la sehemu hii.
Mamlaka ya wanyamapori inayozungumziwa kwenye kifungu cha 8 kwa sasa inaitwa “Tanzania Wildlife Management Authority (TAWA) au mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori Tanzania. Ambapo wanafanya kazi zao kwa mujibu wa sheria hii ya wanyamapori.
Haya ni mambo ambayo yapo kwenye sehemu ya tatu ya sheria ya wanyamapori, nimeamua kuishia hapa ili ili kifungu cha 9 na 10 nitavielezea kwenye makala ijayo. Asante sana kwa kwa kusoama makala hii mpaka hapa.
Hillary Mrosso
Wildlife Conservationist
+255 683 248 681/+255 742 092 569
www.mtaalamu.net/wildlifetanzania