Habari msomaji wa makala za Wildlife Tanzania, karibu kwenye makala ya leo ambayo tutachambua sehemu ya nne ya sheria hii ya uhifadhi wa wanyamapori namba 5 ya mwaka 2009. Katika sehemu hii ya nne ya sheria hii kuna vipengele vingi ambavyo nataka tuvichambue na kuvielewa vizuri ili tujue na sheria inaelekeza nini kwenye maeneo haya. Kwenye sehemu hii ya nne ya sheria hii mambo yaliyojadiliwa ni kuhusu uanzishwaji wa maeneo ya uhifadhi wa wanyamapori na mazuio ya kisheria katika maeneo haya. Hivyo tufuatane pamoja kila hatua ili tujue na tuelimike.

Mapori ya akiba (Game Reserves)

Mapori ya akiba au kama yanavyojulikana kwa lugha ya kingereza Game reserves, ni maeneo ya hifadhi ya wanyamapori ambayo yameanzishwa na kutambuliwa  kisheria kwa mujibu wa sheria hii na sheria nyingine za wanyamapori na uhifadhi. Maeneo haya ya mapori ya akiba ndio sehemu ambayo utalii wote wa aina mbili unafanyika, utalii wa picha na utalii wa kiwindaji. Tanzania tumebarikiwa sana kuwa na maeneo mengi ya aina hii, kwa takwimu za haraka tuna zaidi ya maeneo 28 yaliyotengwa kwa ajili ya kuwa Mapori ya Akiba.

Haya ndio maeneo yaliyoanziswa kisheria kwa ajili ya kuwa Mapori ya Akiba ya  hifadhi ya wanyamapori, kama linavyoonyesha jedwali hapo chini, ni jina la Pori la akiba, ukubwa wa eneo la pori, na mwaka iliyotangazwa kuwa pori la akiba.

 LIST OF GAME RESERVES (ORODHA YA MAPORI YA AKIBA TANZANIA)
No. Name of area (Jina la Pori la akiba) Area (sq. km), Ukubwa wa Eneo Year gazetted (Mwaka iliyoanzishwa)
1 Biharamulo                        1,300.00 1959
2 Burigi                        2,200.00 1972
3 Grumeti                           407.20 1993
4 Ibanda                           200.00 1959
5 Ikorongo                           558.50 1993
6 Kigosi                        7,000.00 1983
7 Kijereshi                           300.00 1994
8 Kimisi                        1,026.23
9 Kizigo                        4,000.00 1982
10 Liparamba                           570.99 2004
11 Luafi                        2,460.90 1993
12 Lukwati                        3,146.00 1997
13 Lukwika-Lumesule                           440.00 1995
14 Maswa                        2,200.00 1962
15 Mkungunero                           700.00 1996
16 Moyowosi                        6,000.00 1981
17 Mpanga-Kipengele                        1,574.25 2002
18 Msanjesi                           220.00 1995
19 Muhesi                        2,000.00 1994
20 Pande                             12.00 1994
21 Rukwa                        4,000.00 1995
22 Rumanyika                           800.00 1974
23 Rungwa                        9,000.00 1951
25 Selous                       47,000.00 1920
26 Swagaswaga                           871.00 1996
27 Ugalla                        5,000.00 1965
28 Uwanda                        5,000.00

 

Katika sehemu hii ya nne ya sheria ndio tunaona sheria ikitambua maeneo haya kuwa kama maeneo muhimu ya hifadhi za wanyamapori na maliasili nyingine. Kwa upande wa sheria kifungu namba 14, kifungu kidogo cha kwanza kinaelezea mwenye mamlaka ya kuanzisha maeneo haya kuwa mapori ya akiba.

Na kama tunavyosoma kwenye sheria hii kwamba mwenye mamlaka ya kuanzisha na kutangaza eneo kuwa pori la akiba au game reseves ni Rais wa nchi.  Sheria inasema Rais anaweza, kwa kushauriana na mamlaka husika za eneo hilo linalotaka kutangazwa kuwa pori la akiba, na kwa kutoa taarifa kwenye Gazeti la serikali anaweza kutangaza eneo lolote la nchi ya Tanzania kuwa Pori la Akiba.

Katika kifugu kidogo namba 2 cha sehemu hii ya uanzishwaji wa mapori ya akiba, kinaelezea masharti ambayo Rais atayaweka kwenye maeneo ambayo yametangazwa kuwa mapori ya akiba na pia kwa kutoa taarifa kwenye Gazeti la serikali masharti na vigezo vyote ambavyo vitatolewa vinatakiwa kutumika kwenye eneo hilo ambalo limetangazwa kuwa pori la Akiba. Na ukiukwaji wa masharti na vigezo vilivyowekwa kwenye eneo hilo ataadhibiwa kwa mujibu wa sheria.

Mazuio ya kuingia kwenye mapori ya akiba (Restriction To enter Game reserves)

15-(1)  Mtu yeyote isipokuwa anasafiki kupitia njia kuu  ambayo inapita kwenye mapori ya akiba au anasafiri  kwa njia ya maji ambayo inapita kwenye mapori ya akiba haruhusiwi kabisa kuingia kwenye mapori ya akiba isipokuwa kwa ruhusa ya kimaandishi ya mkurugenzi ambayo inaonyesha yeye kuingia na kupita kwenye maeneo hayo.

(2) Mtu yeyote atakayekiuka masharti ya sehemu hii, na kufanya tofauti na jinsi alivyoelekezwa na mamlaka husika anafanya kosa, na hilo kosa litamgharimu kulipa faini isiyopungua laki moja (100,000) lakini isiyozidi shilingi laki tano (500,000), au kifungo kisichopungua mwaka mmoja na kisichozidi miaka mitatu au vyote kwa pamoja.

Naamini kufikia hapa umepata maarifa muhimu katika uchambuzi huu wa sehemu hii ya nne, naamini maarifa haya yatasaidia watu wengi kutoa ushirikiano kwenye masula yote ya uhifadhi, pia watu ambao walikuwa hawajui masharti na sheria za maeneo haya wamepata maarifa muhimu kwa ajili ya kuelewa na kutii sheria za sehemu husika.

Mwiso, tukutane Kesho kwenye uchambuzi wa mwendelezo wa sehemu hii ya nne ya sheria ya uhifadhi wa wanyamapori. Asante sanakwa kusoma, mshirikishe na mwingine makala hii.

Ahsante sana!

Hillary Mrosso

Wildlife Conservationist

+255 683 248 681/+255 742 092 569

hillarymrosso@rocketmail.com

www.mtaalamu.net/wildlifetanzania