More

    Athari za Ukosefu wa Ajira na Uharibifu wa Maliasili.

    Leo nitazungumzia jinsi hali ya uchumi katika nchi yetu na hata nchi za jirani unavyoathiri maliasili zetu. Leo natamani tujifunze kwa pamoja jinsi hali ya mambo inavyokwenda kwenye nchi nyetu inavyoweza kusababisha uharibifu wa maliasili zetu na mazingira yote rafiki kwa mustakabadhi wa uwepo wa viumbe hai wetu. Tafiti nyingi sana za kisayansi zimefanyika na pia tafiti nyingi za kiuchumi zimefanyika na wataalamu mbalimbali zinzonyesha jinsi binadamu wanavyotafuta vyanzo mbadala vya kipato ili kujinasua na hali ya uchumi mbaya na umasikini walio nao.

    Hii imepelekea jamii kubwa ya watu hasa wasomi baada ya kumaliza elimu zao wanakosa ajira na hivyo kuona njia mbadala ya kutoka kweneye janga la kukosa ajira ni kujiajiri wenyewe kwenye sekta ya kilimo. Pamoja na  hayao msisitizo wa serikali kwa miaka zaidi ya kumi iliyopita ni kuwashawishi wananchi kuwekeza kwenye kilimo, hasa kilimo cha kisasa, ambacho ni cha kibiashara zaidi kimekuwa na mafanikio makubwa sana kwa miaka ya hivi karibuni.

    Hamasa ya kupata kipato cha ziada na kipato cha kawaida imekuwa ndio nguvu kubwa inayowasukuma watu kuingia kwa kasi kwenye kilimo. Kama tunavyojua asilimia kubwa ya kilimo hichi hutegemea maji ya mito au visima au mabwawa. Hii ndio hupelekea kuharibika kwa vyanzo vya maji na uchafuzi wa maji ambayo ni rasilimali muhimu kwa maisha ya watu wengi. Mwingiliano huu wa kilimo na kuharibika kwa mazingira ya asili imekuwa ni changamoto kubwa sana kwenye maeneo mbali mbali katika nchi yetu. Mfano mzuri ni mashamba makubwa ya mpunga yanayolimwa katika vyanzo vikuu vya mto Ruaha mkuu.

    Tamaa ya kupata mali na mafanikio ya haraka kupitia kilimo imechangia kwa kiasi kikubwa uharibifu wa misitu asili na maeneo mengine muhimu yenye kutunza vyakula na makazi ya viumbe hai katika mazingira yao ya asili. Watu huvamia sana maeneo haya kwa kuwa yana rutuba nyingi kwa kilimo na hufaa sana kwa kilimo bora ambacho hakiitaji gharama kubwa, kama mbolea madawa nk.

    Sisi kama wahifadhi tunatakiwa kuwa makini na hali kama hii inayoendelea kumaliza misitu yetu kwa sababu ya maslahi ya muda mfupi ukilinganisha na uwepo wa maliasili zenyewe kwenye maeneo hayo. Tunatakiwa kujua kwamba tukiaharibu maliasili hizi sio rahisi kuzirudisha kwenye hali ya asili ya kwanza . Hii ndio sababu kubwa ya mimi kuandika makala hii kuhusu shughuli za kibinadamu ambazo zinzweza kuathiri maliasili zetu muhimu. Tujifunze tuakae chini na kufikiri sana kwa umakini kuhusu jambo hili kwa kulinganisha faida na manufaa ya kudumu ni yapi kati ya kuendeleza shughuli za kibinadamu au kuhifadhi uasili wa maeneo yetu yaliyo muhimu kwenye ulinzi na muendelezo wa viumbe hai wetu kwa vizazi vya sasa na vya baadaye.

    Hivyo basi serikali na wadau wengine wa mazingira, mashirika binafsi na watu mbalimbali tusifumbe macho kwenye hili. Tunahitaji kutoa mwelekeo wa mambo haraka na ili hatua za makusudi zifanyike na kuokoa maliasili hizi muhimu. Tunahitaji kuwa wa moja kwenye hili, hii si vita ya mtu mmoja au wawili, ni vita inayohitaji umoja na nguvu kubwa kutoka pande zote za ndani na nje ya nchi.

    Nakukushukuru kwa kusoma makala hii iliyoandikwa na kuandaliwa na;

    Hillary Mrosso

    0742092569

    hillarymrosso@rocketmail.com

     

    Latest articles

    Related articles

    Leave a reply

    Please enter your comment!
    Please enter your name here