More

    Mabadiliko Ya Tabia nchi, Kuibuka kwa Kwa Magonjwa Mapya

    Habari ndugu msomaji wa makala hii,. Karibu tena leo tuangalie kwa jicho la mbali kidogo juu ya mabadiliko ya tabia nchi na athari za kuibuka kwa magonjwa mapya kwa wanyamapori na wanyama wa kufugwa.

    Ktika kujifunza kupitia tafiti nyingi na mwenendo wa dunia na hali ya hewa na mazingira kwa ujumla tuna mengi ya kujifunza na kutusaidia kuchukua hatua stahiki pale tunapoweza. Jinsi dunia inavyozunguka na jinsi majira yanapokwenda na mabadiliko ya kimazingira yanayoletwa na mambo mengi ya sayansi ya anga, lakini watalamu wa mambo wanatuambia kwa kiasi kikubwa mabadiuliko haya yanaletwa na shughuli za kibinadamu kama vile mapenduzi ya viwanda na teknologia, ukataji wa miti na misitu ovyo, uchomaji moto bila mpangilo hasa sehemu zenye idadi kubwa ya viumbe hai, maendeleo ya  kilimo cha kisasa na matumizi ya mbolea kwa kiasi kikubwa umechangia kwa kiasi kikubwa mwonekano tofauti wa dunia.

    Uchafuzi wa mazingira na kuongezeka kwa idadi ya watu na matumizi ya watu yamekuwa makubwa, mapinduzi ya kilimo cha kibiashara imechangia kwa kiasi kikubwa mabadiliko ya tabia nchi. Ufugaji wa kisasa na kuongezeka kwa upanuzi wa hifadhi nyingi katika maeneo ya watu hasa wakulima, kupungua kwa maeneo ya kulishia mifugo ya wafugaji. Haya ni mambo yanayotakiwa kuangaliwa kwa karibu sana kwa mustakabadhi wa afya ya mazingira ya binadamu na wanyamapori.

    Kuna dalili za haraka zimanza kujitokeza hapa kwetu, hasa kwenye hifadhi nyingi kutokana na muingiliano wa wanyamapori na mifugo ya watu waishio karibu na hifadhi. Baadhi ya vitabu na majarida mbali mbali ya kitafiti yanaonyesha kuibuka kwa ugonjwa ujulikanao kama” giraffe skin diseases”umesababishwa na mwingilano wa wa mifugo na wanyamapori hasa kwenye vyanzo vya maji. Tafiti zinaonyesha kwamba ugojwa uliowashika hawa twiga ni kutonana kunywa maji pamoja na mfugo ya wafugaji.

    Kama tulivyoona ianpokuja kwenye suala la mazingira tunategemeana sana, kukosekana kwa maeneo yenye chakula cha kutosha kwa ajili ya mifugo hii husababisha wafugaji kuchungia karibu na maeneo ya hifadhi au kuingiza mifugo yako jambo ambalo ni kinyume cha shera za hifadhi. Hivyo hupelekea kutokuwepo kwa mvua kwa wakati wote hivyo wanyama huangaika kupata eneo ambalo lina maji jambo ambalo huatarisha maisha ya wanyama.

     

    Makala hii imeandikwa na kuandaliwa na;

    Hillary Mrosso

    0742092569/0683248681

    hillarymorosso@rocketmail.com

     

    Latest articles

    Related articles

    Leave a reply

    Please enter your comment!
    Please enter your name here