Katika vipengele tunavyochambua leo tunazungumzia mambo mbali mbali yanayotokea kwenye kazi za uhifadhi wa wanyamapori. Hivyo kulingana na sheria na kanuni mbali mbali za uhifadhi wa wanyamapori, taratibu hizi lazima zifuatwe na kutekelezwa ili kila upande utendewe haki. Leo tunaendelea na sehemu ya saba ya uchambuzi wa sheria hii kuanzia kifungu cha 61.
61.-(1) Mtu yeyote ambaye amepewa lesseni, kibali au mamlaka ya kimaandishi kwa mujibu wa sheria hii atafanya –
(a) atabeba hiyo lesseni, kibali au mamlaka ya kimaandishi ya wakati anafanya majukumu sahihi aliyopewa; kwa ufafanuzi kidogo ni kwamba mtu ambaye ana lesseni , kibali au mamlaka ya kimaandishi ya kufanya jambo kwa mujibu wa sheria hii, atatakiwa kubeba hiyo lesseni au kibali au mamlaka ya kimaandishi ya kufanya jambo wakati wowote anapotaka kutekeleza majukumu yake aliyokabidhiwa.
(b) kunakili au kuweka kumbukumbu kwa Kiswahili au kingereza kwa maandishi yasiyofutika katika nafasi au sehemu nyingine inayofaa kuandika vizuri kila taarifa zinazohusiana na wanyama wote waliouwawa, jeruhiwa au kukamatwa na muhusika katika kutekeleza majukumu sahihi aliyopewa na hakuna mnyama aliyeuwawa au sehemu yoyote ya mnyama huyo itaondolewa kutoka kwa sehemu ilipo kwa mnyama huyo isipokuwa taarifa zote za kina zimeshanukuliwa na kuchukuliwa au kuandikwa kwanza;
(c ) kabla ya siku thelatini za kuisha kwa matumizi ya lesseni, kibali, au mamlaka ya kimaandishi, pale ambapo mwenye lesseni atapendekeza kuondoka katika nchi ambapo ndipo alipopata lesseni, kibali au mamlaka ya kimaandishi, inaruhusiwa kutumika kabla ya tarehe ya kuondoka anatakiwa kuwasilisha au kukabidhi leseni, kibali au mammlaka ya kimaandishi kwa ofisa anayehusika na utoaji wa lesseni ambaye ndie aliyempa lesseni hiyo na atasaini tangazo au azimio kuhakikisha usahihi wa kumbukumbu zilizoandikwa kwa wanyama waliouwawa, jeruhiwa au waliokamatwa mbele ya uwepo wa ofisa.
(2) kwa ofisa wa lesseni ambaye kila lesseni, kibali au vibali vingine vya maandishi vimesalimishwa atasaini tangazo hilo hapo kwenye nafasi iliyowekwa ajili ya kusaini. Ufafanuzi hapa ni kwamaba kwenye ofisi ya mtoa lesseni na vibali mbalimbali, vibali vyote vilivyoisha muda na vingine vinatakiwa kukabidhiwa kwa ofsia huyo na kutiliana saini kwenye nafazi sehemu hiyo inayohitaji kufanyiwa hivyo.
(3) Mtu yeyote atakayekiuka masharti na mapendekezo ya kifungu kidogo cha (1), atakuwa amefanya kosa na atakuwa na hatia kwa ya kulipa faini isiyopungua shilingi laki tano (500,000) lakini isiyozidi shilingi milioni moja (1,000,000) au anaweza kuhukumiwa kwenda jela kwa kifungo kisichopungua miaka miwilii na kisichozidi miaka mitano au vyote kwa pamoja.
- Mkurugenzi anaweza, kwa sababu au nia nzuri na kwa mara moja tu, kuongeza muda wa matumizi halali ya lesseni, kibali au maandishi yoyote ya kibali yaliyotolewa chini ya Sheria hii, kwa kipindi kisichopungua mwezi mmoja, baada ya kujiridhisha kwa maandishi kwamba mmiliki wa lesseni, kibali au kibali cha maandishi alizuiliwa kufanya kwa sababu nzuri majukumu sahihi aliyopewa. Hii ndio sehemu ambayo wale wenye vibali wameshindwa kutimiza matarajio yao kwa mujibu wa vibali vyao kuomba kwa mkurugenzi kuwaongezea muda wa kutumia vibali vyao kwa shughuli zilizoelezwa kwenye vibali na lesseni hizo, hayo ndio mamlaka aliyonayo Mkurugenzi wa wanyamapori.
63.- (1) Mtu yeyote atakaye muua mnyama aliyetajwa kwenye jedwali lolote la sheria hii kwa ajali, atafanya haraka iwezekanavyo mambo yafuatayo-
(a)kuondoa kutoka kwa mnyama huyo Ngozi, pembe, meno au nyara yoyote ;
(b)kutoa taarifa ya kweli kuhusu kilichopelekea kifo cha mnyama huyo kwa ofisa, wasimamizi wa wanyamapori na askari wa wanyamapori, msimamizi wa wanyamapori ndani ya hifadhi, askari wa wanyamapori au skari wanyamapori wa vijiji aliyekaribu ndani ya siku tatu za kzai;
(c ) ukabizishaji kwa afisa wanyamapori, wasimamizi wa wanyamapori, askari wanyamapori, na askari wa wanyamapori wa vijiji nyara ambazo zimetolewa kutoka kwa mnyama, nyara hiyo itakuwa ni mali ya Serikali na inatakiwa kutunzwa kama Mkurugenzi atakavyoelekeza; na
(d) inapohitajika huyo afisa wanyamapori, msimamizi wa wanyamapori, askari wa wanyamapori, askari wa kulinda misitu, askari wa hifadhi za taifa au askari wanyamapori wa vijiji onyesha sehemu ambapo mnyama husika aliuwawa. Hapa inamaanisha kwamba endapo wataalamu hao wa mambo ya wanyamapori na usimamizi watahitaji kujua na kuona sehemu ambayo mnyama husika amekufa au ameuwawa, watu ambao walikusanya nyara za mnyama huyo wanatakiwa kuwaonyesha askari au wafanyakazi kwenye sekta hii kama walivyotajwa hapo kwa mujibu wa sheria hii.
(2) Mnyama hatachukuliwa kuwa ameuwawa kwa ajali endapo mtu aliyemuua ni mmiliki wa lesseni, kibali au kibali cha maandishi cha kuwinda mnyama huyo au spishi hiyo ya mnyama. Ufafanuzi hapa ni kwamba mtu yeyote hatatoa taarifa za uongo kwamba mnyama amekufa au kuuwawa kwa ajali endapo mtu huyo ni mmiliki wa lesseni au kibali cha uwindaji.
(3) Mtu yeyote atakayeshindwa kufutata taratibu zozote za vifungu hivi vya sheria anafanya kosa na atakuwa na hatia ya kulipa faini ya thamani isiyopungua mara mbili ya thamani ya mnyama au kwenda jela kwa kifungo kisichopungua mwaka mmoja na isizidi miezi miwili au vyote kwa pamoja.
Naamini kufikia hapa tutakuwa tumepata mwanga mzuri kwenye kipengele hiki muhimu cha sheria tukutane tena Kesho kwa makala nyingine.
Ahsante sana!
Hillary Mrosso
Wildlife Conservationist
+255 683 248 681/+255 742 092 569
www.mtaalamu.net/wildlifetanzania