Habari mfuatiliaji wa makala za wildlife Tanzania, karibu kwenye makala yetu ya mwisho inayochambua sehemu ya Saba,  sehemu hii ya saba ya sheria hii ni sehemu iliyokuwa na mambo mengi sana ambayo yalinilazimu kusoma kwa makini sana na kuyatafsiri na kuyachambua pale ilipowezekana. Lakini mambo mengi kwenye sehemu hii ya saba yalikuwa yanaeleweka vizuri hivyo ilipelekea kuyatafsri tu kwa Kiswahili na kuyaweka kwenye lugha rahisi kueleweka na wengi yani Kiswahili. Katika kipengele cha mwisho kwenye sehemu hii ya kifungu cha 66 kinaelezea masharti yanayayohusiana na lesseni. Karibu twende pamoja kwenye uchambuzi wa sehemu hii.

66.-(1) Mkurugenzi, ofisa wanyamapori, au afisa wa lesseni anaweza kwa sababu nzuri au kwa nia nzuri-

(a) kukataa kumpa mtu yeyote cheti/hati chochote, lesseni, kibali, kibali cha maandishi au mamlaka yoyote ya kimaandishi chini ya Sheria hii; au

(b) kusitisha, kubadili, au kusimamisha kwa muda cheti/ hati yoyote, lesseni kibali, kibali cha maandishi au mamlaka nyingine za kimaandishi chini ya Sheria hii.

(2) Kulingana na kifungu kidogo cha (1), sababu nzuri kwenye kifungu hiki itajumuisha-

(a) udanyanyifu, ulaghai au hila;

(b) kughushi, kudanganya kwenye maandishi au maandishi yaliyogushiwa;

(c ) kuwasilisha isivyo au kutafsiri vibaya.

(d) ushahidi wa kuwa na hatia kwa mlalamikaji mbele ya mahakama ya sheria;

Ikizingatiwa kuwa kwa kesi yoyote ya kukataa, kusimamisha, kubadili au kusimamisha kwa muda inayotolewa na afisa wanyamapori, afisa wa lesseni wanatakiwa ndani ya siku kumi, kutoa au kuripoti mambo hayo kwa Mkurugenzi.

(3) Mtu yeyote ambaye hataridhika na kukataliwa, kusimamishwa, kubadili au kusimamishwa kwa muda chini ya kifungu hiki cha sheria anaweza, ndani ya siku thelathini za kupata/ kupokea kukataliwa/katazo,kusimamishwa, mabadiliko ya lesseni anaweza kukata rufaa kwa Waziri.

Kutokidhi masharti ya kupewa lesseni

  1. (1) Mtu yeyote –

(a) ambaye atakuwa amehukumiwa kuwa na hatia chini ya sheria hii, Sheria ya Hifadhi za Taifa, Sheria ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro, au sheria nyingine iliyoandikwa inayotumika kwa nchi yoyote na ambayo imeundwa kwa ajili ya ulinzi na uhifadhi wa wanyamapori kwenye hiyo nchi;

(b) ambaye lesseni, kibali, kibali cha maandishi au mamlaka yoyote iliyotolewa kwa maandishi chini ya sheria hii au sheria iliyorudiwa imesitisha, au kusimamisha kwa muda, atakuwa ameshindwa kukidhi vigezo vya kuwa na au kupatiwa lesseni, kibali, kibali cha maandishi au mamalaka mengine ya kimaandishi chini ya sheria hii, isipokuwa na mpaka kutokukidhi vigezo kwake kubatilishwe kwa maslahi ya umma na kwa kufanya maombi,kwa mkurugenzi na kuwe na cheti/hati na mkononi mwake.

(2) Mtu yeyote ambaye atashindwa kumjulisha Mkurugenzi au afisa yeyote wa wanyamapori au afisa wa lesseni  kwa muda wa kufanya maombi ya kuhitaji lesseni, kibali au kibali cha maandishi au mamlaka nyingine chini ya sheria hii na kwa kufuatana na kifungu kidogo cha  (1), anakosa vigezo vya kupatiwa au kumiliki lesseni, kibali au ruhusa nyingine ya maandishi au mamlaka nyingine chini ya sheria hii, anafanya kosa na atahukumiwa kwenda jela kwa kipindi kisichopungua mwaka mmoja lakini kisizidi miaka mitatu

68.-  (1) kila lesseni, kibali, au ruhusa ya maandishi au mamlaka ya maandishi  yaliyotolewa chini ya sehemu hii ya sheria inaweza kutolewa na kuibadili kulingana na masharti ya Mkurugenzi au afisa aliyeitoa, kwa faida ya umma na kwa maandishi masharti hayo yanatakiwa kutokea kwenye lesseni, kibali au ruhusa ya maandishi au mamlaka ya kimaandishi yanayotolewa. Hapa anaweka msisitizo kwamba masharti na vigezo vya sheria ambayo mkurugenzi ataviweka au kuambatanisha na lesseni au kibali  au ruhusa yoyote iliyotolewa na mamlaka au chini ya sheria hii.

Ukizingatia kuwa Waziri anaweza, kwa kufuata kanuni zilizotungwa za sheria hii, kuelezea masharti ya vigezo kwenye lesseni, kibali, ruhusa ya maandishi au

(2) Mtu yeyote atakayevunja vigezo na masharti yoyote ya lesseni, kibali, ruhusa ya maandishi au mamlaka ya kimaandishi anafanya kosa na atawajibika kutoa faini ya kiasi kisichopungua milioni moja (1,000,000) na isiyozidi milioni tano (5,000,000) au kifungo jela kisichopungua miaka mitatu na kisichozidi miaka mitano, au vyote kwa pamoja.

Naamini hadi kufikia hapa tumejifunza mambo mazuri ya sehemu hii ya sheria ya wanyamapori, makala hii ndio inayo malizia sehemu ya saba au (Part VII) ya sheria hii. Tuendelee kujifunza mambo haya ya kisheria ili tujiweke kwenye  upande ambao ni salama kabisa. Makala zijazo tutaichambua sehumu ya Nane ( Part VIII) ya sheria ya uhifadhi wa wanyamapori namba 5 ya mwaka 2009.

Ahsante sana!

Hillary Mrosso

Wildlife Conservationist

+255742092569/ +25568248681

hillarymrosso@rocketmail.com

www.mtalaamu.net/wildlifetanzania