Habari msomaji wa Wildlife Tanzania, napenda kukushukuru sana kwa kuendelea kusoma na kufuatilia makala hizi za kila siku. Kwa siku za hapa karibuni nimekua nachelewa kuweka makala kwa muda mzuri ambao ni asubuhi, hii yote ni kutokana na ratiba yangu kuwa na mambo mengi ya muhimu yanayonilazimisha kuyafanya na yanahitaji muda na utulivu kuyafanya vizuri na kwa ubora unaotakiwa. Nimeandika makala hii kuwashukuru na kuwapongeza marafiki zangu wote mnaosoma makala hizi. Najitahidi kila siku hata kwa kuchelewa niweke makala moja kwenye mtandao wetu wa Wildlife Tanzania. Hivyo nakuahidi mambo yatakaa vizuri sana mapema na tutakuwa tunapata makala hizi za wanyamapori kila siku mapema kabisa.
Pamoja na hayo yote kwa kipindi cha zaidi mwezi mzima nimekuwa naichambua sheria ya wanyamapori namba 5 ya mwaka 2009. Nimekuwa nachambua kipengele kimoja baada ya kingine, hadi kufikia siku ya leo tumeshachambua Sehemu Nane, za sheria hii ya wanyamapori. Nakuahidi tutaendelea na uchambuzi wa sheria hii hadi tuimalize, ndio maana najifunza na kuichambua ili yale nilijifunza na kuyaelewa kwenye sheria hii ya wanyamapori nakushirikisha hapa kwenye blogu hii ya wildlife Tanzania. Hivyo nimekuwa natumia muda mwingi kwenye sheria hii kwa ajili ya kuisoma kuielewa na kuichambua sheria hii ya wanyamapori.
Hivyo rafiki yangu, naamini kabisa kuna kitu unaongeza kwenye maisha yako ya kazi au kwenye sekta hii ya wanyamapori na sekta nyingine za maliasili kwa kusoma makala hizi. Mambo haya ninayoyaandika hapa kila siku kuhusu rasilimali zetu, kama ile utalii, wanyamapori, misitu, maeneo ya kihistoria, maeneo ya fukwe za bahari na maeneo yote yenye vivutio kwa watalii, nimekuwa nakushirikisha ili ufahamu na kupata maarifa haya muhimu, napenda kila mtanzania ajue utajiri wa rasilimali tulizo nazo na kuzienzi kwa njia ya kuzitunza, kuzitembelea na kunufaika na uwepo wa rasilimali hizi. Ndio maana sitachoka kuandika mambo haya, kutoa elimu kwa jamii, kutangaza maliasili zetu, hatimae utalii wetu wa ndani ukue na pato la taifa liongezeke na manufaa yawe makubwa kwa jamii nzima, ili kwa pamoja tushiriki kwa namna moja ama nyingine kwenye uhifadhi wa wanyamapori.
Pia msomaji na rafiki yangu, kazi yote tunayoifanya ni kutoa maarifa ambayo tunaamini yanamanufaa kwa jamii endapo watayajua, kama tunavyofahamu Tanzania ni nchi kubwa miongoni mwa nchi za Afriaka mashariki, yenye idadi kubwa sana ya watu, yenye idadi kubwa ya maeneo ya vivutio kwa wazawa wenyewe na hata kwa wageni waliotoka nchi mbali mbali. Kuna maeneo mengi sana ambayo watanzania wanaweza na wanatamani kufika na kuyaona, kuna vivutio vingi sana vya utalii ambavyo bila kuwajulisha na kuwahamasisha watu uwepo wa vivutio hivyo, vitakaa hapo chini na watu wengi kwenye nchi hii watakufa hawavijui vivutio hivyo na wala hawajawahi kutembelewa na wengi wa watanzania wenyewe.
Naamini kupitia elimu tunaoipata kutoka katika makala za blogu hii, itasaidia kwa sehemu kwenye kuongeza shauku, hamasa na ufanisi kwenye sekta ya wanyamapori na sekta nyingine za maliasili. OMBI LANGU, naamini unanufaika na elimu na maarifa unayoyapata kutoka kwenye blogu hii ya wildlife Tanzania, hivyo unaweza kuwashirikisha marafiki na watu wengine kadri uwezavyo. Naamini utafanya hivyo Rafiki yangu, katika uhifadhi wa wanyamapori. Tuendelee kufuatilia na kujifunza hapa, usisite kutoa maoni yako, ushauri, mapendekezo na maswali utakayokuwa nayo, karibu sana.
Ahsante sana!
Hillary Mrosso
Wildlife Conservationist
+255 683 248 681/+255 742 092 569