Habari Rafiki na Muhifadhi mwenzangu, karibu kwenye makala ya leo tujifunze kwa undani mambo ya kisheria kuhusiana na Nyara, Nyara zilizotengenezwa (manufactured trophy) na usajili wa nyara. Kwenye sehemu hii ya tisa (Part IX) ya sheria ya uhifadhi wa wanyamapori namba 5 ya mwaka 2009. Kuna mengi ya kufahamu kuhusiana na maliasili hizi, kuna mengi ya kujifunza kuhusu nyara na mambo yote yanayohusiana na nyara, kama utangulizi kwenye kifungu cha mwanzo kwenye sehemu hii kinavyoeleza kwa mujibu wa sheria maana ya nyara na maana ya nyara zilizotengenezwa. Karibu twende pamoja ndani ya sheria hii tuone maelekezo na masharti ya sheria hii.
- Kwa kusudi la Sehemu hii-
“Nyara” inamaanisha, meno ya ndovu, pembe za faru, meno ya kiboko, pembe za wanyama na Ngozi za wanyama wa kuwindwa; na
“Nyara zilizotengenezwa” (manufactured trophy) inamaanisha kitu chochote kilichotengenezwa na nyara yoyote au kutoka kwenye kucha, meno, ndovu, pembe,kwato, nywele, manyoya, mayai au sehemu yoyote ya mnyama yeyote.
78.-(1) Mtu yeyote atakayekuwa na nyara atatakiwa ndani ya siku thelethini, kuziwasilisha pamoja na lesseni, kibali au kibali kingine cha maandishi na silaha ambayo iliyumika wakati wa kuvuana nyara kutoka kwa offisa wa lesseni ambayo pia inaonyesha eneo na mpaka aliotakiwa kuwindwa kwa ajili ya usajili wa nyara na utolewaji wa lesseni ya umiliki.
(2) Mtu yeyote atakayekuwa na nyara zozote zilizotengenezwa atatakiwa ndani ya siku thelathini, kuwasilisha nyara kwa aifisa wa lesseni kwa usajili na utoaji wa cheti cha utengenezaji wa nyara.
(3) Usajili wa nyara au utengenezaji wa nyara chini ya sheria hii utaamuriwa au kuelekezwana na Waziri kwenye mapendekezo au kanuni.
(4) Pale ambapo afisa ambaye nyara au nyara zilizotengenezwa zimezalishwa hajaridhishwa kwamba nyara au nyara zilizotenenezwa hazikupatikana kwa misingi ya sheria au hazijapatikana kwa njia ya halali na mtu ambaye alikuwa anavuna hizo nyara kwa ajili ya usajili, anaweza kuzuia au kuzishikilia au kuzisubirisha kwa uchunguzi zaidi. Ufafanuzi hapa ni kwamba pale ambapo afisa wanyamapori anayesimamia shughuli ya uvunaji wa nyara au anayesimamia watu wanaovuna nyara, atakapoona hajaridhishwa au ameona zoezi la uvunaji wa nyara halijafuata kanuni na sheria zilizowekwa anaweza kuzuia au kusitisha usajili wa nyara hizo hadi pale uchunguzi utakapofanyika na kujiridhisha kwamba zoezi limeenda kwa mujibu wa sheria za uvunaji wa nyara.
Ikizingatiwa kwamba hakuna mashtaka au makaosa yoyote yaliyowasilishwa kuhusu nyara au nyara zilizotengenezwa ndani ya miezi miwili kuanzia siku zilipozalishwa kwa ajili ya uasajili, nyara au nyara zilizotengenezwa zitasajiliwa vizuri kabisa na cheti cha usajili kitatolewa kwa mmiliki wa nyara au nyara au nyara zilizotengenezwa.
79.-(1) Mtu ambaye atakuwa na nyara ya aina yoyote au nyara zilizotengenezwa na hana cheti cha usajili kwa mujibu wa nyara na nyara za kutengenezwa, anafanya kosa na atakuwa na hatia ya kilipa faini isiyopungua mara mbili ya thamani ya nyara au kifungo jela kisichopungua mwaka mmoja lakini kisichozida miaka mitano, au vyote kwa pamoja;
Ikizingatiwa kuwamba mashitaka yoyote ya makosa chini ya kifungu hiki mshitakiwa atahukumiwa kuwa na hatia ikiwa atairidhisha mahakama kwamba-
(a) Kwamba tangu ianze kutumika alikuwa ameshapata kisheria cheti cha usajili wa nyara au nyara zilizotengenezwa (manufactured trophy); au
(b) Kwamba kwa siku tisini hazijaisha matumizi kati ya tarehe ya kwanza aliyoipata au aliyopata nyara au nyara zilizotengenezwa na tarehe ambayo nyara au nyara zilzotengenezwa na kuruhusiwa na ofisa mwenye mamlaka kwa kesi ya uchunguzi ambayo ilipelekea kuendelea kwa utendaji, pale ambapo tarehe ya kwanza ilipotokea.
(2) Mtu ambaye atampa mtu mwingine yoyote nyara au nyara iliyotengenezwa kukiwa hakuna cheti cha usajili wa nyara wakati wa kupeana hizo nyara au nyara zilizotengenezwa anafanya kosa na atakuwa na hatia ya kulipa ya faini isiopungua mara mbili ya thamani ya nyara au nyara zilizotengenezwa au kwenda jela kwa kifungo kisichopungua mwaka mmoja lakini kisizidi miaka mitano au vyote kwa pamoja.
(3) Mtu atakayempa mtu mwingine yeyote nyara au nyara zilizotengenezwa bila kumkabidhi kwanza mpokeaji wa hizo nyara cheti cha usajili kuhusiana na usajili na uhamishaji wa nyara, na ikiwa mpokeaji wa hizo nyara atazipokea bila kupata kwanza cheti cha usajili wa nyara au nyara zilizotengenezwa anafanya kosa na atahukumiwa adhabu ya kulipa faini isiyopungua mara mbili ya thamani ya nyara au nyara zilizotengenezwa au atakwenda jele kwa kifungo kisichopungua mwaka mmoja lakini kisichozidi miaka mitano au vyote kwa pamoja.
Hadi kufikia hapa naamini tumejifunza mengi ya kisheria kuhusu usajili wa nyara na mambo mengine ya kufahamu kuhusu nyara na uhamishaji wa nyara, vyeti na muda unaotakiwa kusajili. Tuendelee kuwa pamoja kwa makala zijazo ambapo tutajifunza zaidi kutoka kwenye sheria hii mambo mengi sana kuhusu wanyamapori na sheria zinazoendesha sekta hii nyeti.
Ahsante sana!
Hillary Mrosso
Wildlife Conservationist
+255 683 248 681/+255 742 092 569
www.mtaalamu.net/wildlifetanzania