Habari Rafiki karibu kwenye makala ya leo, tunachambua sehemu ya kumi na saba ya shria ya wanyamapori ya mwaka 2009. Sehemu hii ya sheria inaelezea mambo mengi ya masharti, adhabu, na faini na mambo ya ushahidi mahakamani. Sehemu hii ya sheria ina mambo mengi sana.mambo haya nitayachambua kidogo kidogo ili tuelewe na tujue msingi wake.
100.(1) Hatua zozote za kisheria zitachukuliwa kwa makosa yanayohusiana na uwindaji usiozingatia sheria, uuaji, uakamataji wa wanyama kinyume na mapendekezo ya sheria hii, atakayewajibika kudhibitisha kwamba mnyama amewindwa, kuuwawa, au kukamatwa, na kulingana na vigezo na masherti ya lesseni iliyotolewa, kibali au mamlaka yaliyotolewa chini ya sheria hii yatakuwa juu ya mtu anayetuhumiwa au anayeshitakiwa. Ufafanuzi hapa ni kwamba mtu atakayehusika na kufanya makosa yaliyotajwa kwenye kifungu hiki cha sheria ndiye atakayewajibika kuthibitisha mahakamani kuhusiana na makosa aliyoyafanya chini ya kifungu hiki.
(2) Pale hatua zozote zitakapochukuliwa kuhusu makosa chini ya kifungu cha 85 zinatakiwa kuonyesha au thibitisha na kuiridhisha mahakama-
(a) nyara ya serikali ambayo ndio jambo mtu ameshitakiwa kwalo imepatikana kwenye jengo, nyumba, au sehemu yoyote ya jengo, au jengo linalomilikiwa na mtu anayeshitakiwa au mtegemezi wake haijalishi kwamba mtuhumiwa yupo pale wakati nyara inapatikana ; au
Hapa anamaanisha kwamba kwa mtu ambaye anatuhumiwa au anashitakiwa kwa kuwa na nyara za serikali, na hiyo nyara ikaonekana kwenye eneo lolote ambalo lipo kwenye umiliki wake, kwa mfano jingo, nyumba au ardhi au sehemu yoyote iliyo chini ya umiliki wake, atatakiwa kudhibitisha mahakamani kuhusiana na nyara hizo kwenye eneo lake.
(b)kwamba nyara ya serikali imepatikana kwenye gari yoyote, mizigo, vifungashio au imefungwa kwenye karatasi kwa ajili ya kubeba au inamilikiwa na mshtakiwa au wakati mshtakiwa alikuwa navyo hadi wakati nyara inapatikana, isipokuwa imethibitishwa, mahakama itafikiria au itachukulia kwamba kwamba nyara hiyo ni itakuwa ni ya mshitakiwa.
Kipengele hiki kinaeleza endapo mshtakiwa anakabiliwa na kutunza au kuwa na nyara za serikali au nyara za serikali zimekutwa kwenye gari, mifuko au kwenye mizigo yake moja kwa moja mahakama itadhania na kuchukulia kuwa aliyekamatwa na nyara hizo kwenye mizigo yake au kwenye kitu chochote alichonacho huo ndie mtuhumiwa na kwa mujibu wa sheria hii atakuwa na kesi ya kujibu mbele ya mahakama.
(3) Hatua zozote za kisheria zitakazochukuliwa chini ya kifungu cha 85 zinatakiwa kuthibitisha kwamba-
(a) umiliki wa nyara za serikali ulikuwa wa kihalali na wa kisheria;
(b)kuuza , kununua au biashara nyingine inayohusisha nyara za serikali ilikuwa ya kihalali na ilifuata sheria
( c) mshtakiwa atachukulia kumiliki nyara ili kuendana na matakwa ya vifungu vya 85 na 86; au
(d)nyara ilikuwa sio nyara ya serikali, itakuwa juu ya mtu anayeshitakiwa.
Sheria ya wanyamapori ina kesi nyingi sana ambazo bado zipo mahakamani, hii ni kutokana na umakini na kukosa ushahidi. Ni kati ya kesi zinazosumbua sana na kuchukua muda mrefu kuisha. Hivyo kwako Rafiki yangu unayesoma makala hii naamini hutajiingiza kwenye vitendo vya kijangili na kushirikiana kwa namna yoyote ile kuhujumu au kufanya mambo ambayo sheria hii ya wanyamapori na sheria nyingine zinazosimamia sekta hii zinakataza. Jiepushe na matatizo, kesi nyingi huwa haziishi na adhabu zake ni kali sana. Hivyo basi ili kuepuka usumbufu kwenye maisha yako achana na mambo ya ujangili au hata uharibifu wa mazingira. Tujifunze kuwa wazalendo kwenye rasilimali zetu.
Ahsante sana!
Hillary Mrosso
Wildlife Conservationist
+255 683 248 681/+255 742 092 569
www.mtaalamu.net/wildlifetanzania