Habari msomaji wa makala za wildlife Tanzania, karibu kwenye makala ya leo ambayo tunaendelea kuichambua  Sheria ya wanyamapori namba 5 ya mwaka 2009. Tukiwa tunaelekea mwishoni mwa uchambuzi wa sheria hii, nataka ujue wanyama na ndege waliotajwa sana kwenye baadha ya sehemu za sheria hii. Wakati tunaanza uchambuzi wa sheria hii kuna vifungu vingi sana vinataja wanyama ambao wapo kwenye majedwali ya sheria hii. Sasa leo tutaona jedwali la kwanza na wanyama waliopo kwenye sehemu hii ya jedwali. Kwenye sheria ya wanyamapori wametumia majina matatu kwa lugha ya Kiswahili, kingereza na jina la kisayansi wakati wa kuwataja wanyama na ndege hawa.

Jina la kiswahili Jina la kingereza Jina la Kisayansi
Babakoko sanje Sanje Mangabay Cercocebus sanjei
Choroa Oryx Oryx beisa callotis
Chui Leopard Panthera Padus
Duma Cheetah Acinonyx jubatus
Faru Black Rhinoceros Diceros bicornis
Kipunji Highland Mangabey Lophocebus kipunji
Mbuzi mawe (Nguru) Klipsgringer Oreotragus oreotragus
Mbwa mwitu Wild dog Lycon pictus
Mindi Abbotts Duiker Cephalophus Spadix
Nyati (Mbogo) Buffalo Snycerus caffer caffer
Nzohe Sitatunga Limnotragagus spekeii
Pahalahala rosaveti Rosavelt Sable Hipotragus niger rosalvetii
Pimbi Hyrax Heterohyrax/Procavia
Pundamilia Zebra Equus burchellii
Sengi Giant Elephant Shrew Rynochocyon uduzungwensis
Sheshe Puku Kubus vardoni
Simba Lion Panthera leo
Simbamangu Caracal Felis caracal
Swala robati Robart Gazzele Gazella granti robartsi
Swalatwiga Gerenuk Litocranus walleri
Tandala mdaogo Lesser Kudu Strepsiceros imberbis
Tembo (Ndovu) African Elephant Loxodonta Africana
Tohe- mlima Mountain Reedbuck Redunca fulvorufula
Korongo nyangumi Shoebill (Whale headed stock) Balaeniceps rex
Korongo usomwekundu Watle Crane Bugeranus carunculatus
Kozi kipanga Peregrin Falcon Falco peregrinus
Kwale uduzungwa Uduzungwa Forest Patridge Xenoperdix uduzungwaensis
Ninga Green Pigion Treron
Mamba Slender Snorted Crocodile Crocodilus crataphractus
Chura wa Kihansi Kihansi Spray Toad Nectophrynoides asperginis

Hivyo Rafiki naamini kabisa utakaposoma makala au seheria wakitaja wanyama waliopo kwenye majedwali basi nadhani utaelewa vizuri kabisa. Leo nimetaja tu wale wanyama na ndege wanaopatikana kwenye Sehemu ya kwanza ya Jedwali na jedwali la kwanza. Karibu kwa maswali na maoni, bila kusahau ushauri.

Ahsante sana!

Hillary Mrosso

Wildlife Conservationist

+255 683 248 681/+255 742 092 569

hillarymrosso@rocketmail.com

www.mtaalamu.net/wildlifetanzania