Habari msomaji wa Wildlife Tanzania, Karibu kwenye makala ya leo ambayo ni kukupongeza na kukushukuru kwa kusoma makala zote za uchambuzi wa sheria ya wanyamapori Tanzania. Tangu tuanze kuchambua sheria hii ya wanyamapori nimejifunza vitu vingi sana ambavyo nilikuwa sivijui, na ambavyo nimeviandika kwenye makala ambazo nilikuwa nawashirikisha kila siku. Kwa kuwa sheria hii ilikuwa na mambo mengi ya kujifunza niliamua kuandika na kuchambua kila sehemu, kila kifungu na kila vipengele; na kila nilichokiona tunahitaji kukifahamu na kukielewa niliwashirikisha kupitia mtandao huu wa Wildlife Tanzania.
Katika uchambzi wa sheria ya wanyamapori ya mwaka 2009, sheria hii yenye Sehemu 19. Nimeichambua na kuandika makala zaidi ya 50 ambazo nimeelezea na kuchambua kila kipengele cha sheria hii. Kwa msisistizo zaidi ningekushauri kama unajua kusoma kwa lugha ya kingereza unitumie email yako nikutumie sheria hii ambayo nilikuwa naichambua. Ni vizuri ukaipitia mwenyewe tena ili uelewe vizuri zaidi. Pia katika uchambuzi wa sheria hii nilkuachia kazi ya kufanya ambayo ipo kwenye sehemu ya kumi na saba, nilikuachia usome hapo wewe mwenyewe ingawa nilichambua kidogo.
Sheria hii ya wanyamapori imeandikwa kwa lugha ya kingereza hivyo kwenye uchambuzi wa sheria hii ilihitajika nguvu nyingi na muda mwingi ili kuichambua kwa lugha ya Kiswahili na kwa maneno yanayoeleweka kwa wasomaji wengi. Hivyo ifahamike kuwa makala zote zinazohusu uchambuzi wa sheria hii ya wanyama pori, ni baada ya kusoma na kutafsiri na kuchambua na kuweka makala hii kwa lugha ya Kiswahili. Hivyo basi kuna baadhi ya maneno na misamiati ya kingereza iliyokosa maneno ya Kiswahili mazuri ya kuelezea, pamoja na hayo nimejaribu kuangalia kwenye kamusi mbali mbali za Kiswahili na kingereza ili kupata maana ya misamiati hiyo na kueielezea, pia sehemu nyingine nimeyaweka maneno hayo ya kingereza kama yalivyo kwenye uchambuzi kwa kuyafungia kwenye mabano.
Nia yangu na shauku yangu tangu mwanzo kabla sijaanza kuandika makala hizi ni kutaka mambo haya ya maliasili na wanyamapori yeleleweke vizuri kwa watanzania na umma wote. Lengo langu kuu ni kutoa elimu ya hifadhi kwa watanzania na watu wengine kwa lugha ya Kiswahili ambayo inaeleweka kwa watanzania na watu wengine. Naamini kupitia maarifa na elimu tunayoipata kupitia makala hizi tutakuwa na idadi kubwa ya watu wenye uelewa na ufahamu kwenye masula ya uhifadhi wa maliasili na mazingira kwa ujumla. Na hii ndio itasaidia sana kwenye vita dhidi ya ujangili, na kutoa ushirikiano kwenye mambo mbali mbali yanayohusu uhifadhi wa maliasili na faida zake.
Katika zama hizi za taarifa nimeamua kutumia nafasi hii na fursa hii kuwekeza kwenye mitandao ya internet na mitandao mingine ya wasap, nimekua naandika makala mbali mbali za mafunzo na kuwashirikisha watu kwenye makundi mbali mbali kama vile facebook, wasap, emal na linken. Hivyo kwa wanaotaka kujua na kujifunza mambo mbali mbali kwenye sekta hii watakapoona makala husoma na kufahamu zaidi kuhusu maliasili zetu. Hivyo kwa wale wanaopenda kujifunza na kunifuatilia kwenye mitandao ya kijamii huwa natumia Jina la Hillary Mrosso, kila ninachojifunza na kuona kinafaa huwa nawashirikisha wenzangu kwa njia hizo.
Kwa namna ya kipekee niwashukuru wote walioniandikia kwa ushauri maswali na hata mapendekezo, wengine wamenitia moyo, yote hao yananipa hamasa zaidi ili kuendelea kujifunza vitu mbali mbali na kuwashrikisha. Pia namshukuru sana Sadick Kashushu ambaye ni mwandishi mzuri sana wa makala za kuelimisha kuhusu wanyamapori, amekua anaandika makala zenye mvuto na zenye maudhui muhimu sana kwenye uhifadhi wa wanyamapori; kweli kupitia mtandao huu wa wildlife Tanzania watu wanapata elimu na maarifa ya uhifadhi. Pia tumekua tunawashirikisha watanzania na watu wengine wanaotaka kuwekeza kwenye sekta hii ya wanyamapori kama vile ushauri, fursa na hatua za kuanza kuchukua.
Pia nitoe nafasi kwa watu wenye uzoefu, wenye uelewa na maarifa mbali mbali anayofikiri ni muhimu kwenye uhifadhi wa wanyamapori, kukuza utalii au kuhamasisha watanzania kuwa na utamaduni wa kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo Tanzania. Kama upo tayari kuwa mwandishi na kuchangia uzoefu na maarifa uliyonayo, basi usisite kuwasiliana na mimi ili tujenge na kuimarisha maliasili zetu. Nawakaribisha sana kama unaweza andika makala ya jambo lolote kuhusu wanyamapori, utalii, utunzaji wa misitu, au vivutio vya asili au mambo ya kale karibu sana kwenye mtandao huu wa wildlife Tanzania uweke makala zako. Makala zako zitapostiwa na kusambazwa ili elimu uliyoitoa iwafikie wengi. Kama upo tayari tuwasiliane kwa namba hizi. 0683248681 au 0742092569. Au kwa email hillarymrosso@rocktmail.com. Karibu tufanye kazi kwa pamoja.
Nakushukuru sana kwa kusoama makala hii, karibu tuhifadhi kwa pamoja, uhifadhi ni jukumu letu wote.
Ahasante sana!
Hillary Mrosso
Wildlife Conservationist
+255 683 862 481/+255 742 092 569
www.mtaalamu.net/wildlifetanzania