Habari msomaji wa mtandao wa wildlife Tanzania, karibu sana leo tujuzane yaliyojiri katika sekta hii ya Maliasil na Utalii. Kuna vitu ambavyo hatauwezi kupuuza au kuacha kusema neno vinapotokea, hii ni kwa sababu vitu hivyo vinagusa moja kwa moja maeneo muhimu kwenye maisha ya kila mtanzania. Ndio maana kwa kujua hilo nikaamua kukaa chini ili kuandika makala hii ya kumpongeza Dr. KigwangalLa kwa kuteuliwa kuwa Waziri wa maliasili na utalii Tanzania. Hivyo tunakupongeza kwa kupata nafasi hiyo ya kusimamia Wizara ya Maliasili na Utalii.
Siku chache zilizopita Rais wa Jamhuri ya Muungano Dr. John Pombe Magufuli alifanya mabadiliko makubwa kwenye baraza la Mawaziri hasa Wizara ya Maliasili na Utalii baada ya kumteua Dr. Hamis Kigwangalla kuchukua nafasi ya aliyekuwa Waziri kwenye sekta hiyo Profesa Jumanne Maghembe. Kwa vyoyote vile hatau kubwa zinapochukuliwa kwenye sekta hii nyeti naamini zinaweza kuzaa matunda mazuri na makubwa kwenye maliasili zetu. Hivyo karibu sana Dr. Kigwangalla kwenye sekta hii.
Tangu kuteuliwa kwa Dr. Kigwangalla, tumeona mabadiliko makubwa sana kwenye mfumo mzima wa utendaji hasa kwenye matumizi ya maliasili. Lakini kubwa zaidi nimependa jinsi ambavyo mheshimiwa Waziri alivyoanza kazi baada ya uteuzi wake, alifanya vikao na wadau wote wa sekta ya maliasili na utalii pia alitoa nafasi kwa wadau wengine kuwasilisha michango yao kwa njia ya maandishi na kuahidi michango na mawazo yao yatasomwa na kufanyiwa kazi, hili ni jambo zuri na ni namna nzuri sana ya kuanza kufanya kazi.
Wizara ya maliasili na utalii inasimamia sekta pana sana ya maliasili ambayo imekuwa na changamoto kwenye baadhi ya maeneo. Sekta hii ni moja ya sekta yenye mwingiliano mkubwa sana na sekta nyingine. Mfano sekta ya maliasili na utalii inaingiliana na sekta ya kilimo, sekta ya uvuvi, sekta ya mazingira, skta ya maji, sekta ya ardhi nk, hizo ni baadhi ya sekta ambazo zinzingiliana sana na sekta ya maliasili na utalii. Kutokanana na kutokuwepo kwa vikao vya kisekta na kufanyia kazi maamuzi na mapendekezo yanayotolewa na wadau wa sekta hizi kumekuwa na migogoro isiyoisha kwenye baadhi ya maeneo ya hifadhi za wanyama na wakulima na wafugaji. Hivyo vikao vya kisekta na wizara tofuti zinazoingiliana ni muhimu sana kwa ajili ya kutafuta suluhisho la kudumu kwenye migogoro inayoendelea kwenye sekta hizi.
Pamoja na mambo mengine baada ya uteuzi wake mheshimiwa waziri kwa mamlaka aliyopewa amefuta vibali vyote vya uwindaji nchini. Na pia ametaka vitalu na maeneo yote yenye migogoro kushughulikiwa haraka sana hasa maeneo ya Lolionda na manegine. Naamini hatu hizi zitaweka mambo sawa kwenye utoaji wa vibali na lesseni za uwindaji, ili kuwe na sintofahamu kwenye utendaji kwenye utalii wa uwindaji Tanzania.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dr. Hamisi Kigwangalla alipotembelea makao makuu ya Hifadhi za Taifa Tanzania Leo hii na kutoa maelekezo yafuatayo: (maelekezo haya nimeyachukua kutoka katika ukurasa wa facebook wa Utalii Tanzania)
-
# Jitihada za makusudi ikiwa ni pamoja na ubunifu unahitajika katika kufikia lengo la watalii milioni mbili ifikapo mwaka 2020.
# Spidi ya utendaji kazi lazima iongezeke na kuwa kasi kubwa zaidi.
# Bado utajiri wa vivutio vya utalii haujatumika ipasavyo kuvutia watalii wengi zaidi nchini.
# Wananchi lazima washirikishwe katika uhifadhi wa rasilimali tulizonazo.
# Tuwe na mbinu za kisasa za kuzuia ujangili kabla haujatokea badala ya kupambana nao wakati mnyama ameshapoteza maisha.
# Tuwekeze zaidi katika eneo la intelijensia ili kupata taarifa za uhalifu mapema zaidi.
# Tuwekeze katika kuongeza mapato ya utalii pamoja na kuziba mianya yote ya upotevu wa mapato lwa kutumia mifumo ya kielektroniki.
# Tuwekeze zaidi katika kutatua migogoro baina ya hifadhi na wananchi.
# Tuzidi kuimarisha uhifadhi ili hifadhi zetu ziweze kuwepo kwa muda mrefu ujao.
# Ubunifu unahitajika katika kuitangaza vema nchi yetu kiutalii.
# Shirika lipanue wigo wa vivutio vya utalii ili kuwafanya wageni kukaa muda mrefu sana nchini.
# Wananchi wanapaswa kufaidika na uwepo wa sekta ya utalii nchini.
# Ukanda wa kusini lazima ufunguke kuvutia watalii wengi zaidi.
# Kuimarisha mfumo wa jeshi usu.
# Kurekebisha mfumo wa viwango vya wahudumu wa sekta ya utalii wawe na viwango bora na usajili ili waweze kutoa huduma stahiki kwa watalii wanaotembelea nchi yetu.
# Uzalendo, uadilifu na uwajibikaji ni muhimu katika utekelezaji wa majukumu ya umma.
Haya ndio baadhi tu aliyoyasema na kuagiza kufanyika kwenye sekta hii ya utalii. Naamini kila mtu akiangalia hapo kwenye maelekezo ana nafasi yake ya kufanya ili kuutangaza utalii wa Tanzania na maliasili zake. Tukifanya kazi kwa bidi kwenye sekta hii tutafikia malengo yaliyoweka na kuzidi.
Mwisho, nakupongeza sana Dr. Kigwangalla kwa nafasi hii uliyopata kusimamia wizara ya maliasili na utalii. Sisi kama wadau na watanzania wengine tunaonga mkono juhudi zote za kizalendo kwenye maliasili zetu. Wewe ni kijana, bado una uwezo mkubwa sana wa kufanya mapinduzi makubwa kwenye sekta hii naili kuwa sekta bora kabisa kwa manufaa ya nchi na wananchi wote. Karibu sana Mheshimiwa Dr. Kigwangalla.
Ahasante sana!
Hillary Mrosso
Wildlife Conservationist
+255 683 824 681/+255 742 092 569
www.mtaalamu.net/wildlifetanzania