Siku zote katika kujifunza njia mbali mbali hutumika, ikiwemo ya kuingia darasani na kujifunza au kwenda kujifunza kwa watu wengine na njia nyingine ya kujifunza ni kusafiri. Na hapa ninapozungumzia kusafiri na maanisha kuenda sehemu ambayo hujawahi kufika. Sehemu ambayo hakuna anayekujua, sehemu ambayo kitu kitakushangaza, sehemu ambayo utakutana na vitu vipya ambavyo vitaongeza ufahamu wako na ujuzi wako wa vitu.
Kuna msemo mmoja wa kingereza wanapenda sana kuusema kwamba utakua hivyo hivyo ulivyo kama ulivyo sasa kwa miaka mitano ijayo isipokuwa watu unaokutana nao au vitabu utakavyo soma. Sasa kuna ukweli mkubwa sana kwenye sentensi hii, na hapa anazungumzia ukuaji wa maisha ya binadaumu, kukua kiakili na kiufahamu, sio kukua kwa mwili. Kwenye ukuaji wa akili ni tofauti kabisa na ukuaji wa mwili. Ili akili ikue lazima mwili uumie na ndio maana juhudi zote za kuisaidia akili ya binadamu ikue zinakuwa na upinzani mkubwa sana. Mwili hautaki uteseke, lakini cha muhimu ni akili yako ipate maarifa na taarifa au chakula cha kukuza ufahamu wako. Juhudi za makusudi zinahitajika sana ili kuboresha na kuikuza akili ya mtu. Ndio maana wengi hawapendi kusoama kwa sababu wanautii sana mwili.
Maisha aliyotupa Mungu tuyaishi hapa duniani sio maisha ya kuishi kama miti au minazi kwamba umepandwa hapa ni hapo hapo hakuna kuhama wala kusogea sehemu nyingine. Bindamu tumeumbwa tofauti na wanyama wengine na mimea mingine. Kwa sabau sisi tumepewa na Mungu utashi na uwezo wa kuchagua chochote tunachopenda, tunapenda ndio maana tunachagua, hivyo basi naamini tutatumia nguvu hii aliyotupatia Mungu kuamua mambo mazuri na yenye tija kwenye jamii. Sisi tuanweza kukaa sehemu moja na pia tunaweza kuondoka na kwenda sehemu nyingine.
Ni jukumu letu wenyewe tumepewa kila kitu kizuri kwa ajili ya kukifurahia na maua na kukijua. Hivyo basi natoa rai kwa watanzania wenzangu tujenge utamaduni wa kutembelea sehemu zenye vivutio vya wanyama na pia sehemu nyingine na vivutio vingine vingine. Dunia ni kama kitabu kama hausafiri huwezi kujua kilichoandikwa kwenye ukurasa unaofuata. Mambo mengi yameandikwa kwenye vitabu na majarida mbali mbali, lakini sio kila kitu kimeandikwa. Hivyo suala kuamua kutembelea na kuona wanyamapori na vivutio vingine ni jambo kubwa na la msingi sana. Ee mtanzania mwenzangu anza sasa kutembelea na kusafiri kwenda kwenye sehemu unzaopenda kwenda. Epuka kukaa sehemu moja miaka nenda miaka rudi. Jifunze hata unapopata nafasi ya kusafiri sehemu mbali mbali. Chukua jukumu hili mtanzania mwenzangu. Utajiri uliopo huko porini usikubali uusikie tu, nenda ukaone mwenyewe. Panga safari tembea, fanya kila kitu kwa ajili ya kufurahia na kujifunza.
Karibu sana porini. Asante sana!
Hillary Mrosso
Wildlife Conservationist
+255683 862 481/+255742 092 569