Habari msomaji wa makala za mtandao wako wa Wildlife Tanzania, karibu kwenye makala ya leo ambayo nimeiweka kwenye mfumo wa swali. Naamini umekuwa kwa kiasi kikubwa ukifanya kazi karibu mwaka mzima, wengine walikuwa wanafanya kazi zao kwa matarajio ya kupata likizo zao na kuzitumia kusherekea pamoja na familia zao, wengine wamepanga kwenye mapumziko yao kuwatembelea ndugu zao, wengine wamepanga kwenye mapumziko yao kutembelea sehemu mbali mbali zenye utulivu na wengine wamepanga kutembelea mbuga za wanyama, wengine hawajui waende wapi.
Ni vizuri ukaamua kweye muda wako wa mapumziko kwenda kupumzika wapi, au unaweza kwenda kutalii sehemu gani, kwa wale walioko Dar eselaam wanaweza kwenda kwenda hifadhi ya Mkumi, Uduzungwa, Saadani hizi ndizo zipo karibu na kama unataka kwenda kutembelea na kukaa kwenye fukwe za bahari pia kwa nchi ya Tanzania tumejaliwa kuwa na fukwe nyingi sana, Pwani yote ya Tanzania ina fukwe nzuri sana, pia unaweza kwenda Zanzibar ambako kuna vivutio vingi sana vya baharini na tamaduni mbali mbali.
Kwa wale walioko mikoani wanaweza kupanga kutembelea vivitio vilivyopo karibu na maeneo yao, unaweza kwenda hata sehemu za kihistoria, makumbusho, au mbuga za wanyama. Kuna wengine kipindi hiki cha sikukuu wanapenda kwenda kwenye kumbi za starehe, disko. Unaweza kubadili mwaka huu usifanye hivyo, na kuamua kwenda sehemu tofauti na kufanya vitu tofauti na miaka mingine, nenda sehemu kwa nia ya kujifunza, kufurahia .
Maisha yetu yana mambo mengi sana unaweza ukafikiri umeshajua kila kitu kumbe hujui sehemu kubwa sana ya maisha iliyobaki, na hii haitatokea kwa kuendelea kukaa sehemu moja pekee. Unatakiwa kuwa na utamaduni wa kutembelea maeneo mapya pale inapowezekana na unapopata muda wa kufanya hivyo.
Hivyo basi unaweza kutaka kwenda kutembelea maeneo yenye vivutio na hujui pa kuanzia, karibu kwa ajili ya maswali maoni na mapendekezo. Kama unataka kujua utaratibu wa kutembelea sehemu za vivutio wasiliana nami moja kwa moja, au nitumie ujumbe kwa njia ya barua pepe au kwa kuacha komenti mwisho wa makala hii.
Ahsante sana!
Hillary Mrosso
Wildlife Conservationist
+255 683 862 481/+255 742 092 569
www.mtaalamu.net/wildlifetanzania