Hakuna kitu chochote hapa duniani kinachofanyika kwa ufanisi bila kuwepo kwa taarifa sahihi kwa muhusika wakati wa kufanya jambo. Elimu ni muhimu sana kwa maisha ya binadamu yeoyote, mtu ambaye amekosa elimu anakuwa msumbufu sana kwenye maisha yake na maisha ya wenzake. Na hapa kwenye elimu nataka kuzungumzia elimu zote, elimu ya darasani na elimu isiyo ya darasani au elimu mtaani. Nimeona mambo haya kwenye sekta nyingi sana, watu wanaonewa kwa sababu ya kukosa elimu nzuri, watu wa wanafaidika na kunufaika kwasababu ya elimu zao.
Ukosefu wa elimu hasa elimu ya msingi upo kwenye maeneo mengi ya vijijini. Ni jambo ambalo linafanya maisha ya watanzania wengi yawe magumu na yasiyotabirika. Elimu ya kujitambua nayo imekosekana sana kwenye maeneo mengi, elimu ya mazingira nayo imeadimika kwa wananchi wengi hasa waishio vijijini. Ili tufike mbali hatuna budi kushughulikia tatizo hili mapema sana iwezekenavyo.
Ukosefu wa elimu umechangia kuongezeka kwa rushwa, kwa sababu ya wananchi hawajui kinachoendelea kwenye maeneo yao, mikataba na hata mambo mengine ya kitaalamu. Kwenye usimamizi wa malisili jambo hili limekuwa changamoto kubwa sana. Na kwa kuwa jamii haijui kinachoendelea hawawezi hata kuhoji, kuuliza na hata kufuatilia. Kimsingi watu wengi hatujui haki na wajibu wao kwenye jamii. Tunaamini kwamba viongozi tuliowachagua au walioteuliwa watafanya kwa uaminifu na kusimamia mali ya umma kwa uadilifu na kwa uwazi.
Uwepo wa miradi mingi kwenye masuala ya uhifadhi wa wanyamapori unasaidia sana katika suala la utoaji wa elimu mbali bali hasa elimu ya mazingira lakini ni miradi michache sana iliyojikita kuwaelimisha wananchi, hasa walio vijijini masuala ya kisheria yanayohusu usimamizi wa rasilimali za nchi kama vile wanyamapori na misitu. Athari za ukosefu wa elimu hii umechania kwa kiasi kikubwa kukosekana kwa uwazi, uwajibikaji na usimamizi mbovu wa maliasili za nchi yetu.
Sababu kubwa ikiwa ni watu kutojua kuwa wanawajibu wa kufuatilia na kuhoji kwenye masuala haya ya rasilimali zao, watu wengi wanaogopa kuwahoji viongozi na hawajui mambo mbali mbali ya matumizi ya fedha zinazopatikana kwenye Kijiji chao kupitia maliasili zinavyotumika na kuwanufaisha jamii nzima. Lakini jambo jingine baya sana ni watu wenyewe kutokuwa na muda wa kufuatilia na kujifunza mambo mbali mbali ya kimaenedeleao kwenye Kijiji chao, wanapotezea mafuunzo muhimu hata hawataki kujihusisha wala kushiriki kwenye masuala haya nyeti yanayomgusa kila mtu, kwa kizazi cha sasa na baadaye.
Ahsante sana!
Hillary Mrosso
Wildlife Conservationist
+255 683 862 481/+255 742 092 569
www.mtaalamu.net/wildlifetanzania