Hongera sana rafiki yangu na msomaji wa mtandao wa Wildlife Tanzania, karibu tena kwenye mwanzo mwingine wa mwezi, huu ni mwezi wa mwisho kabisa kwa mwaka 2017. Nakukaribisha na hizi ndio salamu zangu za mwezi mpya wa kumi na mbili, mwezi Disemba
Mwezi desemba unapofika huwa unapokelewa na hisia tofauti tofauti, na watu wengi hupenda sana mwezi huu kwa sababu ni mwezi wa mwisho ili kumaliza mwaka lakini pia ni mwezi ambao huwa na sherehe na siku nyingi za mapumziko. Ni mwezi ambao una matukio mengi mazuri na ya kusisimua . Kwa wengine wanatumia mapumziko ya mwezi huu kuwatembelea ndugu zao, wengine hutumia mapumziko ya mwezi huu kukaa na kutulia pamoja na familia zao, wengine huenda sehemu mbali mbali za utulivu na kufurahia mapumziko yao.
Kwa kweli mapumziko ni sehemu ya maisha ya binadamu yoyote, kila mtu anahitaji muda wa kupumzika na kufurahi na kuatafakari maisha yake ili apata nguvu za kurudi tena kwenye mapambano ya maisha. Ndio maana hata kwenye sheria za kazi wametaja kipengele hiki muhimu cha siku za mapumziko ambazo mtu anapewa kwa ajili ya kujipumzisha ili ufanisi uongezeke kwenye utendaji wa kazi zake za kila siku.
Makala hii fupi niliyoandika siku ya leo ni kwa ajili ya salamu na kukupongeza lakini pia kukusaidia kujua kuwa kuna maeneo mengi sana ya mapumziko kipindi hiki cha msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka. Kulingana na matamanio yako mwenyewe, unapenda kwenda kutembelea wapi na unataka kuona nini unapotembelea maeneo hayo. Tanzania ina maeneo mengi ya mvuto na yenye hadhi nzuri ambayo yatakufanya ufurahie na kuyaona maisha kwa upande mwingine.
Kulingana na uwezo wako uneza kuwenda sehemu zozote nzuri kwa ajili ya kupata mapumziko, unaweza kupanga sehemu ya kwenda wa ajili ya mapumziko yako, pia unaweza kupanga kwenda na familia yako, watoto wako na hata unaweza kwenda na rafiki yako au mwenza wako. Itapendeza zaidi utakapopanga ukienda sehemu hizo na rafiki yako au mwenza wako.
Ahsante sana
Hillary Mrosso
Wildlife Conservationist
+255 683 862 481/+255 742 092 569