Habari msomaji wa makala za wildlife Tanzania, karibu kwenye makala ya leo, ni makala ambayo nimepanga kukushukuru na kukutakia kila la kheri kwenye mapumziko haya ya sikukuu za Krismasi. Najua katika kipindi kama hiki watu wengi wapo majumbani kwao na familia zao, wengine bado wanaendelea kupambana na shughuli za kila siku. Lakini yote katika yote nawatakia mapumziko mema na mazuri katika kipindi hiki cha msimu wa sikukuu.
Kuna wengine wamepanga kutembelea maeneo ya vivutio na mbuga za wanyama kwenye msimu huu wa sikukuu, kuna wengine wapo nyumbani na familia zao, yote ni mema. Nami nawapongeza na kuwaakia kila la kheri. Makala ya leo haitakuwa na mambo mengi sana, ni makala ya kuwatakia kila la kheri kila msomaji wetu na kila mtanzania.
Naamini umekuwa ukisoma makala zetu kwenye blog ya wildlife Tanzania, ambapo tunaandika makala mpya kila siku na kuzichapisha huko, makala hizi ni kwa ajili ya kuhamasisha utalii na uhifadhi wa wanyamapori, pia makala hizi ni kwa ajili ya utunzaji wa mazingira, hivyo kwa kiasi chake naamini umepata maarifa na taarifa muhimu, na kujifunza mambo mbali mbali ya wanyamapori.
Pia nataka kukufahamisha kuwa uandishi wa maswala haya ya wanyamapori ni jambo ambalo napenda kulifanya na pia napenda kuandika habari nyingi zenye kuleta hamasa na maarifa kwa watanzania na kwa kila mtu kuhusu uhifadhi na utalii wa ndani. Naamini katika njia hii itasaidia na kutoa mwanga kwa watanzania wenzetu wasio na uelewa wa mambo haya, lakini pia kupitia makala hizi watu watawajua wanyama, watawapenda na watakuwa tayari kuwatunza na kuwahifadhi.
Nakushukuru kwa kuendelea kufuatilia na kuwa msomaji wa makala za mtandao wetu wa www.mtalaam.net/wildlifetanzania . Nakuahidi mambo mazuri yanakuja mambo ya kuelimisha na kufahamu zaidi hifadhi zetu na vivutio mbali mbali. Karibu tuendele kuwa pamoja kujifunza, kufurahia na kutembelea, mambo mengi mazuri yanakuja.
Asante sana kwa kusoma makala hii, karibu kwa makala nyingine.
Hillary Mrosso
Wildlife Conservationist
+255 683 862 481/+255 742 092 569