Habari msomaji wa makala za wildlife Tanzania, karibu tena kwenye makala ya leo ambapo nitakujuza mambo mbali mbali kuhusu uhifadhi Hifadhi za wanyamapori Tanzania. Leo tutaangalia Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro. Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro ni moja ya hifadhi maarufu sana Tanzania na duniani kwa ujumla. Ni eneo lililopo kati ya Serengeti na Ziwa Manyara. Eneo hili lilipo kwenye kwenye mkoa wa Arusha lina ukubwa wa kilomita za mraba 8,292. Ni eneo linalosemekana kuwa na idadi kubwa sana ya uoto na tabia nyingi za kiasili kama vile miinuko na mabonde yaliyosababishwa na milipuko ya volkano, maziwa, misitu na maeneo muhimu ya kihistoria.
Pia eneo hili la Ngorongoro linatambulikana duniani na Shirika la UNESCO kama eneo la Uridhi wa Dunia kwa kuwa na eneo kubwa la kaldera (Caldera), pia uwepo wa shimo la creta imechangia kuwepo kwa idadi kubwa sana ya wanyama wa aina mbali mbali.
Hivyo basi kwa uchache nikushirikishe baadhi ya maeneo unayoweza kuyaona unapotembele hifadhi hii ya ajabu, inayotajwa kama inaweza kuwa ni ajabu la nane la dunia kati ya yale maajabu saba ya dunia. Hii ni hifadhi yenye upekee sana, ni moja ya hifadhi nilizowahi kutembelea nakujione haya yote niliyoyandika kwenye makala hii. Hivyo nimeamua kukushirikisha haya machache ili upate kufahamu uzuri na upekee wa eneo hili kubwa. Hivyo fuatana nami ili nikutazamishe mambo yote ya msingi kwenye eneo hili.
- Mwonekano mzuri wa eneo la Kreta
Uwepo wa shimo hili panda na refu sana linaloitwa “Kreta” au “Crater”lenye urefu wa kimo cha mita 610, na ukubwa wake ukifikia zaidi ya kilomita za mraba 260. Ukubwa na mwonekano huu wa kipekee ndio kivutio kukuu sana kwa wageni kupenda kutembelea hifadhi hii ya kipekee. Kutokana na hali ya hewa ya eneo hili imepelekea kuwa na uoto unavutia na kuwafanya wageni kuwa ndio kituo kikuu cha kuangalia mandhari nzuri ya eneo hili la kreta, wakati wa jioni na asubuhi hizi ndio saa nzuri kuangalia mandhari nzuri ya eneo hili la kipekee.
- Uwepo wa idadi kubwa sana ya wanyamapori katika eneo hili la kreta
Katika eneo hili la kreta pekeee lina idadi kubwa sana ya spishi za wanyma ambao wanapatikana katika hifadhi za Afrika Mashariki. Tafiti zinaonyesha eneo hili la kreta pekee lina zaidi ya wanyamapori 25,000 wakubwa ikiwa ni pamoja na wanyama kama Faru weusi ambao wapo hatarini kutoweka kabisa katika uso wa dunia, endapo juhudi za makusudi hatachukuliwa mapema kuwahifadhi. Katika shimo hili la kreta hakuna fensi wa la ukuta, hivyo wanyama huingia na kutoka, lakini muda mwingi hukaa ndani ya kreta kwasababu ya uwepo wa maji na chakula cha kutosha.
- Olduvai Gorge (Oldupai)
Hapa ni sehemu yenye miteremko iliyosababishwa na bonde la ufa. Hilo bonde linloitwa Oldopai ni neno la kimasai linalomaanisha mmea wa katani. Ni hapa Oldupai ambapo mabaki ya kihistoria ya binadamu wa kwanza inaposemekana yalikuwapo na kugundulika na watafiti maarufu waliojulikana kama Dr. Louis na Mary Leakey, zaidi ya miaka 50 iliyopita. Hapa ndipo sehemu amabyo unaweza kupata kwa kina historia zote za binadamu wa kale. Hivyo hapa pamekuwa ndio sehemu inayovutia zaidi wageni mbali mbali kutoka ndani na nje ya nchi.
- Watu na tamaduni
Hifadhi ya eneo la Ngorongoro ni tofauti kabisa na hifadhi za nyingine za Taifa, kwenye hifadhi za Taifa hawaruhusu kabisa shughuli zozote za uzalishaji au shughuli nyingine za kibinadamu, kama kulima, kulisha mifugo ndani ya hifadhi nk. Lakini maajabu ya Ngorongoro bado ni makubwa sana kwa sababu, watu jamii za kifugaji hasa wamasai wapo ndani ya eneo hili na kufanya shughuli zao za maendeleo na kuishi na wanyama bila wasi wasi, eneo hili Kingereza linaitwa (multiple land use), yani eneo lenge matumizi mengi. Zaidi ya miaka 200 iliyopita wafugaji wa Kimasai walikuepo na kulitawala eneo hili, na kutokana na mfumo wa maisha yao ya kitamaduni ulikuwa rafiki kwa maziingira ya uhifadhi wa wanyamapori, hivyo ndio sababu wpo ndani ya hifadhi hii ya Eneo la Ngorongoro. Hadi kufikia sasa eneo hili lina idadi kubwa sana ya wafugaji wa kimasai. Sababu nyingine ya wamasai kuendelea kuwepo hapo ni kutokana na utamaduni wa kuvutiwa wa Kimasai ambao ndio kivutio tena kwa wageni mbalimbali.
- Uoto wa aina mbali mbali
Ngorongoro ni sehemu iliyojaliwa kuwa na utajiri wa uoto wa asili ambao mara nyingi huonekana kijani, kutokana na hali nzuri ya hewa pamoja na upatikanaji wa maji kwenye eneo hili. Kuna aina nyingi sana za miti na mimea ya asili,pi uwepo wa nyasi fupi, mabwawa ya maji na yenye unyevu nyevu uanostawisha mimea na kuifanya kijani wakati wote wa mwaka. Uoto huu wa kipekee umekuwa kivutio kwa wageni wa kitalii na wale watafiti wanaopenda kijifunza zaidi kuhumsu mimea mbali mbali.
- Ziwa Ndutu na Masek
Maziwa haya muhimu kwa hifadhi hii hayana kina kirefu lakini maji yake yana chumvi hivyo hayafai kwa matumizi ya binadamu. Kwa ziwa kama Ndutu ambalo hutumiwa zaidi na wanyama kama sehemu ya kunywa maji na kupumzika baada ya wanyama kuhama, na pia ni sehemu nzuri zenye wanyama kama kiboko na mamba, hivyo wageni hutumia nafasi hii kama sehmu ya kuwaona wanyama.
- Mchanga naotembea (Shifting sand)
Huu mchanga unaaonekana hapa ni majivu yaliyorushwa na mlipuko wa volkano, mchanga huu unaosifika kwa kuwa na umbo kama la mwezi, umekuwa kivutio kikubwa kwa watu wote wanopenda kutazama maajabu haya ya hifadhi hii ya Eneo la Ngorongoro.
Kufikia hapo naamini umepata mwanga wa kukusaidia kukuelimisha kwa uchache mambo ya msingi na ya kuvutia kwenye hifadhi hii ya kipekee ya Eneo la Ngorongoro. Ni sehemu ambapo hutajuta kwenda, utafurahiya kila utakachokiona. Hivyo nichukue fursa hii kukukaribisha kutembelea Eneo la Hifadhi ya Ngrorongoro.
Ahsante sana kwa kusoma makala hii;
Hillary Mrosso
Wildlife Conservationist
0742092569/0683862481