Joto limekuwa likiathiri vitu vingi Ulimwenguni ikiwemo jinsia za viumbe vya aina mbalimbali kama vile watoto wa Mamba, Kasa, Samaki na baadhi ya Mijusi. Kihistoria kuna aina saba Kasa ambao walikuwepo yapata miaka millioni 110.Wakiishi katika maji chimv au baridi. Toafuto na kobe ambao wanaishi nchi kavu Kasa hawezi kurudisha kichwa chake ndani ya gamba lake kwa kuwa ni laini na miguu ya wavuti inayomsaidia kuogelea kwa kasi majini .Kasa anauwezo wa kubana pumzi takribani masaa 5 akiwa majini. Chakula chao kikubwa ni mimea ya ya Baharini kama vile plankton, yavuyavu, mwani ,kaa, kamba na matumbawe.
Kasa ni viumbe amabo wapo katika kundi la Reptilian a ametajwa kuwa ndio kiumbe mwenye kumbukumbu kubwa katika kundi lake. Kasa Jike anauwezo wa kurudi wa kurudi katika Fukwe za Bahari ile ile aliyototolewa licha ya kuwa husafiri bahari moja na nyingine ila muda wa kuzaliana unapofika yeye hurudi kwenye fukwe zile zile ili na yeye atage mayai. Kama ilivyo kwa reptilia wengi kasa hawezi kuatamia mayai yake bali huchimba kiota na kufukia mayai yake mpaka yatakapototolewa. Uwiano wa joto katika kiota ndi hupelekea jinsia Fulani ya kasa wanapototolewa. Mfano nyuzi joto 31 kushuka chini hupelekea kuanguliwa kwa madume na nyuzi joto 34 kwenda juu hupelekea kuanguliwa kwa majike.
Pamoja na kuwa na maajabu yote hayo, bado aina hii ya reptilia inapata changamoto za aina mbalimbali kama vile(i) Kasa hutaga mayai 7000 katika maisha yake na kwa kila msimu Kasa mmoja anaweza kuwa na viota vinne mpaka sita ambapo huwa na mayai 80 mpaka 180. Pamoja na kutaga mayai mengi kiasi hicho, ni kasa wachache sana wanaweza kuangaluiwa , wakukua na kuzaliana tena kwa sababu zifuatazo;
- Binadamu huweza kuwinda mayai ya kasa nkwa ajili ya chakula
- Upungufu wa Oxygeni baharini unaochangiwa na uchauzi wa bahari kama vile mafuta
- Virafanga vya kasa kunaswa na taka ngumu pindi wanapoanguliwa na kutaka kuingia baharini.
- Mifuko ya plastiki inapokuwa baharini Kasa huifananisha na Yavuyavu (jellyfish) hivyo wanapokula huziba mfumo wa umeng’enyaji chakula na kufa.
- Mabadiliko ya Tabia ya nchi, ambao huathiri uwiano wa jisnia za kasa ◇Shughuli holela zifanywazo ufukweni,ambapo huathiri uwezo wa kasa kutengeneza viota kna njia ya kwenda baharini wakishatotolewa. Hivyo fukwe yenye shughuli nyingi humtisha Kasa kutoka kuja kutaga mayai.
FAIDA ZA KASA
♤Kasa ni kivutio kizuri kwa watalii ambao hupenda kutembelea maeneo ya fukwe kama vile hifadhi ya taifa Saadani ambako viota vya kasa hupatikama.
♤Kasa ni viashiria vya biolojia kwa huonyesha hali ya mazingira hasa ya majini
- vilevile hutumika katika shughuli za utafiti na kujifunza.
♤Kasa husaidia katika mzunguko wa chakula baharini.
HITIMISHO
Serikali na wizara husika inawajibu wa kuhakikisha fukwe zinaachwa wazi kwa ajili ya Kasa kuja kutengeneza viota. Pamoja na hilo ni ni wajibu wa kila mmoja wetu kuhakikisha fukwe zetu zinakuwa huru na safi ili kusaidia kasa kuzidi kuzaliana na kuacha kabisa shughui ambazo zinahatarisha maisha yao.
Shukrani za pekee ziende kwa Alphonce Msigwa, Mwikologia Hifadhi za Taifa Tanzania, kwa kuhariri makala hii ili iwe katika viwango na ubora.
Ahsante sana!
Makala hii imeandikwa na;
Maureen FN Daffa
maureen.nick08@gmail.com
+255 626 331 871.
[/et_pb_text][/et_pb_column] [/et_pb_row] [/et_pb_section]