Tembo ni mamalia wakubwa wa jenasi Elephas na ‘Loxodonta’ za familia ya ‘Elephantidae, na pia ndio mnyama mkubwa mla nyasi kuliko wote ulimwenguni.

Kama inavyoonekana katika picha, hizo ni spishi tatu za tembo, tembo wa Asa, tembo wa Savana, na tembo wa misituni.

Kuna spishi tatu tu za tembo zinazoishi mpaka leo ambazo ni

✅Ndovu-nyika au tembo wa vichakani wa Afrika (Africani Bush Elephant), ambao ni mkubwa kuliko wengine.

✅Tembo wa misituni wa Afrika (African Forest Elephant) na

✅Tembo wa Asia (Asian Elephant). Wanafanana lakini hawazaliani.

Ndovu-misitu alitazamwa muda mrefu kama nusu-spishi ya Ndovu wa Afrika lakini wataalamu wamethibitisha ni spishi tofauti. Hufikia kimo cha mita 2 tu; anaishi hasa katika misitu ya Kongo. Spishi nyingine zote za tembo zimekoma.

Tembo ndiyo mamalia wa nchi kavu wakubwa kuliko wote sasa. Ana jumla ya meno ishirini na 28 pamoja na ndovu zake. Ndovu zote mbili za tembo zinakadiliwa kua na uzito wa kilo 200. Ana uwezo wa kukimbia hadi speed ya 40km/h (25mph).

Mkonga wake unakadiliwa kua na misuli ipatayo 1200, hivyo kupelekea kuvunja hata miti mikubwa. Mkonga wa tembo huweza kuvuta maji hadi lita 14 kwa wakati mmoja. Kwa siku tembo hula chakula (Nyasi) hadi kilo 300. Na hunywa maji hadi lita 200 kwa siku

Uume wa tembo ni kilo 27, ukimwona akiwa anafanya mating uweza sema ana miguu mitatu. Manii ya tembo yanakadiliwa kufikia hadi lita 5!!! Tembo akitembea kishindo chake hakisikiki kutokana na kua na ponge like nyayoni kwake na iliyojaa layer ya mafuta.

Tembo hubeba mimba kwa miezi 22, muda mrefu kuliko wanyama wote wa ardhini. Ndama wa tembo akizaliwa huwa na uzito wa kilogramu 120. Tembo huishi kwa miaka 50-70, lakini tembo aliyevunja rekodi aliishi miaka 82.

Tembo mkubwa kupata kuishi alikuwa huko Angola na kupigwa risasi mnamo mwaka 1956. Tembo dume huyu alikuwa na uzito wa kg. 12,000, akiwa na kimo mpaka mabegani cha mita 4.2, mita moja zaidi kuliko tembo wa sasa wa Africa. Tembo wadogo, kama saizi ya ndama, au nguruwe mkubwa, waliishi zamani sana, huko visiwa vya Crete.

Tembo wametokea sana kwenye tamaduni za dunia. Ni ishara/alama ya hekima huko Asia na ni maarufu kwa uwezo wao wa kumbukumbu na akili, ambapo hufanikiwa kukaribiana na jamii ya binadamu wa kale. Mwanafalsafa Aristotle aliwahi kusema ndiye “mnyama pori anayewapiku wengine wote kwa hekima na akili”*. Hili linathibitishwa katika chuo kikuu cha dodoma (udom) ambapo tembo wameonekana kukatiza mara kadhaa katika maeneo hayo ikiwa kama ndio njia au mapito yao ya kale kabla shughuri za binadamu hazijaanza.

Picha hii imepigwa na Patric Hozza, ikionyesha tembo na meno yake yakiwa yametokea mbele.

Jina la tembo kwa Kiingereza lina asili ya neno la Kigiriki lenye maana ya *meno/pembe za ndovu. Tembo wakubwa hawana wanyama wanaowawinda ingawa simba huweza kuwashambulia ndama wa tembo na tembo wadhaifu. Japokuwa hutushiwa sana na kuwa hatarini kutokana na mwingiliano na binadamu na ujangili. .

Kadiri ya sensa ya mwaka 2007, tembo wa Afrika walikuwa kati ya 470,000(laki 4 elfu sabini) au 690,000(laki sita na elfu tisini). Tembo hulindwa duniani kote. Hii ni sambamba na maeneo maalumu ya kuwakamata, matumizi ya nyumbani na biashara kwenye mazao yake kama vile vipusa. Mataifa kadhaa yameripoti kupungua kwa tembo wao mpaka kufikia theluthi mbili, na hata wale walio kwenye maeneo tengefu nao wako hatarini kutoweka kutokana na kuongezeka kwa ujangili kwa zaidi ya asilimia 45% kupelekea hata takwimu za sasa kutokuwepo.

Asante sana kwa kusoma makala hii hadi mwisho, makala hii imehaririwa na Hillary Mrosso na kuandikwa na;

Ramadhan Msangi Yunus

Mob ;  +255 62 150 9606

Email ; ramahsucre@gmail.com