Ziwa nyasa  ni miongoni mwa maziwa matatu makubwa yanayopatikana  Kusini mwa Afrika na Afrika Mashariki, neno nyasa limetokana na lugha ya chichewa (malawi) ikiwa na maana ya ziwa. Ziwa Nyasa ni ziwa la nane kwa ukubwa duniani na la tatu kwa kina kirefu kuanzia 264-700M.

Ziwa Nyasa linatumika na nchi tatu yaani Malawi, Tanzania na Msumbiji, ikiwa sehemu kubwa ipo nchini Malawi. Ziwa Nyasa lina ukubwa wa 29600km2    lenye maji safi (fresh water).Lina  jamii ya samaki zaidi ya 1000 na sifa kubwa lina asilimia tisini na tano (95%)  ya samaki ambao wanapatikana ziwa hili tu ni ( ziwa lenye endemic species  wengi duniani.

Ajabu ya maji ya ziwa Nyasa ni kuwa juu yana hali ya joto (24-29) lakini sehemu ya chini  (bottom) maji ni baridi(22), hali hii ya utengano wa jotoridi la maji (thermocline) hutokeaa kuanzia kina 40-100M.

Samaki wapo wa aina nyingi wakiwepo (cichlid na non- cichlid), kambare, tilapia akiwepo na kampango (bagrus meridionalis) . Pia ziwa hili hupokea maji kutoka katika mito mingi kama vile vile  mto Ruhuhu, Songwe,  na Dwangwa.

Zijue sifa samaki kampango

Ndugu msomaji wa makala hii pengine umewahi kufika ziwa Nyasa (wilaya ya Nyasa mkoa wa Ruvuma) au wilaya ya Kyela, je,  umewahi kumuona samaki anaitwa Kamapango ( scientific name: bagrus meridionalis).  Jina Kampango ni jina la asili samaki huyu anapatikan ziwa Nyasa tu  na ana sifa kubwa sana ambayo pengine umewahi  kuona au kusikia kwa viumbe wengine.

 Hebu tuone bagrus meridionalis au Kampango kama anavyofahamika na wengi ana sifa  zipi ambazo zinampa upekee wake katika ziwa Nyasa na jamii ya Kampango.

Samaki kampango (bagrus meridionalis)
  1. Ni samaki pekee wanao lea watoto wao  kwa pamoja (wazazi wote)  yaani baba na mama mpaka wafikie  12cm (wakubwa) .(bi parental care).  Jee ni samaki gani mungine huwa  anafanya hivi? ( Basi kama una mfahamu  toa maoni  hapo chini)
  2. Kampango hukua kufikia urefu wa 45cm kwa kawaida lakini pia hukua mpaka 1- 1.5M)
Samaki kampango akiwa na watoto.
  1. Kampango huzaliana kipindi cha Januari mpaka Machi kila mwaka ambapo  Kampango dume yeye hujenga kiota (nest) na jike hutaga  mayai katika kiota. Mayai yasiyorutubishwa  hutumika kama  chakula kwa watoto baada ya kutotolewa, ambapo Kampango dume huenda kukamata wanyama wadogo wadogo (micro vertebrae or zooplankton) kwa ajili ya kuwalisha watoto wao Baba na mama wanahusika vema kuwalea watoto). Nukuu: Sifa ya kutumia mayai yake kama chakula pia awe na upekee sana.
  2. Kampango hufanya mahusiano na viumbe wengine (mahusiano chanya,) kwamba yeye anauwezo wa kulinda mayai ya samaki wengine watakao kuja kutaga katika kiota chake na kulinda mayai mpaka watoto wakue.lakini pamoja na hayo yale mayai ambayo hayata rutubishwa hutumika kama chakula kwake na watoto wake.(brood parasitism)
  1. Kampango hupatikana sana usiku au anaweza kufanya kazi sana usiku katika kujitafutia chakula (nocturnal). Hupendelea sana kwenye mapango ya mawe, sehemu zenye matope, pia kina cha kawaida 50M  ambapo Oksijeni inakuwa rahisi kupatikana.

 Vitisho dhidi ya samaki kampango

Samaki kampango ni miongoni mwa samaki waliopo hatarini kupungua au kupotea kwa sababu ya mambo yafuatayo;

  • Uvuvi haramu,
  • Uvunaji uliopitiliza,
  • Uchafuzi wa maji hivo kupelekea kukosekana kwa hewa safi kwenye maji. 

Matumizi ya samaki Kampango kiutamaduni ziwa Nyasa.

Samaki kampango hutumika kama chakula. Mfano ukienda maeneo ya ziwa Nyasa (wilaya ya Nyasaa, eneo Mbamba Bay) samaki huyu hupikwa au kumchoma na huliwa na ugali wa muhogo. (Kampango +ugali wa muhogo). Pia samaki Kampango hutumika sana msimu wa ngoma za asili za jamii ya Wanyasa kama chakula cha heshima kwa wageni.

MAONI YANGU.

Rai yangu kwa serikali za nchi zinazotumia ziwa Nyasa zinatakiwa kuchukua hatua juu ya kuboresha mazingira mazuri ya uvuvi. Kwa upande wa tanzania, Wizara husika kupitia taasisi yake ya utafiti wa samaki yaani, Tanzania Fisheries Research Institute (TAFIRI) na Tanzania Department of Fisheries, zinatakiwa kuweka mikakati na kuangalia ziwa Nyasa kama sehemu yenye rasilimali nyingi za viumbe wengi kama samaki hawa. Pia niombe wizara kutoa nafasi za watalaamu kufanya utafiti wa kina kwenye ziwa hili ili tuweze kunufaika na rasilimali za Ziwa hili. Lakini kwa sasa Malawi ndio nchi pekee ambayo inawafaidisha sana wanainchi wake kupitia rasilimali za ziwa Nyasa.

Asante sana kwa kusoma makala hii hadi mwisho, usisite kuwasiliana nasi kwa maoni, ushauri na hata maswali, tumia mawasiliano ya mwandishi wa Makala hii hapo chini kuwasiliana nasi.

.

Kamanga Shadrack Andrea.

Phone: 255 678 577 786

Email: bigstarshadrack@gmail.com