Habari msomaji wa makala za wanyamapori na utalii, karibu kwenye makala ya leo ambayo nimejikita kwenye kufahamu baadhi ya tozo mbali mbali ambazo zipo ndani ya Hifadhi za Taifa. Tozo nilizoelezea hapa ni maalumu kwa hifadhi ya taifa ya Arusha. Lakini naamini hifadhi nyingi huwa na tozo kama hizi, zinafanana sana. Hivyo nimeanza na hifadhi ya taifa ya Arusha, makala zijazo tutaelezea tozo na utaratibu wa hifadhi nyingine.
Tozo hizi ni kwa mujibu wa uongozi na usimamizi wa hifadhi za taifa na TANAPA, hivyo zinaweza kubadilika muda wowote serikali na uongozi wa hifadhi utakapoona unafaa.
Karibu sana.
Tozo mbali mbali
- Tozo ya uhifadhi:
- Zaidi ya miaka 16 waafrika Mashariki 10,000 na watoto mika 5 -15 ni 2,000 na watoto chini ya miaka 5 ni bure. Hii ni kwa wageni wote wanaotoka Afrika Mashariki.
- Wasio wa Afrika mashariki, zaidi ya miaka 16 Dola 45 na watoto kuanzia miaka 5 – 15 ni dola 15 na chini ya miaka 5 ni bure. Hii ni kwa wageni ambao sio wa Afrika Mashariki.
- Kupanga mahema – Maeneo ya Jumuiya
- Zaidi ya miaka 16 shilingi 5,000, watoto kuanzia miaka 5 – 15 ni shilingi 2500 na watoto chini ya miaka 5 ni bure. Tozo hizi ni kwa ajili ya wageni wanaotoka Afrika Mashariki.
- Kwa wageni ambao sio wa Afrika Mashariki kuanzia miaka zaidi ya 16 watalipa dola 30, na watoto kuanzia miaka 5 – 15 watalipa dola 5. Watoto chini ya miaka mitano ni bure.
© Kupiga mahema – maeneo maalumu
- Zaidi ya miaka 16 watalipa shilingi 10,000 na watoto kuanzia miaka 5 – 15 watalipa shilingi 5,000. Wtoto chini ya miaka 5 ni bure. Tozo hizi ni kwa wageni waliotoka Afrika Mashariki.
- Kwa wageni ambao hawajatoka Afrika Mashariki, zaidi ya miaka 16 watalipa dola 50, na walio na miaka kuanzaia 5 – 15 watalipa dola 10, na watoto chini ya miaka mitano ni bure. Tozo hizi ni kwa wageni wote ambao hawajatoka Afrika Mashariki.
(d)Kupiga mahema- kambi za kuhama
Flying camp 5,000 kwa walio wa Afrika Mashariki na dola 50 kwa wageni wasio wa Afrika Mashariki.
( e) Tozo za malazi
- Vituo vya Miriakamba na Saddle shilingi 2,000 kwa walio wa Afrika Mashariki na dola 30 kwa wageni wasio wa Afrika Mashariki
- Vyumba vya kulala wageni walio wa Afrika Mashariki ni shilingi 15,000 na wasio wa Afrika Mashariki ni dola 30.
(f) Tozo za Hosteli, kwa walio wa Afrika Mashariki ni shilingi 5,000 kwa wageni ambao sio wa Afrika Mashariki ni dola 10.
(g) Tozo za kupiga makasia ziwani
(i) Kwa mtu mzima ni shilingi 5,000, kwa watoto ni shilingi 2,000. Tozo hizi ni kwa wageni wote ambao wanatoka Afrika Mashariki.
(ii) Kwa wageni ambao sio wa Afrika Mashariki, mkubwa anatoa dola 20 na watoto watatoa dola 10.
(h) Tozo wa utalii wa kupanda Farasi, kwa wageni wanaotoka Afrika Mashariki watalipa shilingi 50,000 na wageni wasiotoka Afrika Mashariki watalipa dola 50.
(i) Tozo za kupiga picha za kibiashara kwa mtu kwa siku ni Dola 250 (Hii inajumuisha tozo ya uhifadhi, kambi na upigaji picha).
(j) Faini za ajali ndani ya hifadhi (magari ya aina zote) ni shilingi 200,000.
(k) Tozo za kutembea kwa miguu
(i) Matembezi mafupi (saa 1 hadi 4), zaidi ya miaka 16 ni shilingi 5,000 na watoto miaka 12 -15 shilingi 2,500. Tozo hizi ni kwa wageni waliotoka Afrika Mashriki.
(ii) Matembezi mafupi kwa wageni ambao sio wa Afrika Mashariki watalipa dola 20 na watoto miaka 12- 15 watalipa Dola 10.
- Matembezi marefu (zaidi ya saa 4) kwa wageni kutoka Afrika Mashariki kuanzia miaka 16 watalipa shilingi 10,000 na watoto miaka 12 -15 watalipa shilingi 5,000.
- Wageni wasiotoka Afrika Mashariki kuanzia miaka 16 watalipa Dola 25, na watoto kuanzia miaka 12 – 15 watalipa Dola 15.
(l) Tozo za mwongoza wageni/huduma ya askari mwenye silaha (kwa kundi)
(i) Mwongoza wageni (mtumishi wa hifadhi) atalipwa shilingi 5,000 na wazawa, na wageni watatoa Dola 20.
(ii) huduma ya askari wakati wa kupanda mlima Meru shilingi 10,000 kwa wazawa na Dola 15 kwa wageni ambao sio kutoka Afrika mashariki.
(m) Tozo ya uokoaji, kwa wazawa ni shilingi 2,000 na kwa wageni ambao sio wa Afrika mashariki ni Dola 20.
(n) Tozo ya utalii wa kula chakula (hot meals), kwa wazawa ni shilingi 5,000 na kwa wageni ambao sio wa Afrika Mashariki ni Dola 5.
(O_) Tozo ya watoa huduma watanzania (crew) kwa siku ni shilingi 3,500 (Hii ni kwa ajili ya waongoza wageni, wapangazi, na wapishi. Hii inajumisha gharam za uhifadhi shilingi 1,500 na gharama ya kambi/banda shilingi 2,000.
(p)Faini ya mwendokasi uliovuka kiwango hifadhini hii ni kwa magari yote ni shiingi 50,000.
(q) Viingilio vya magari zenye usajili wa Tanzania
(i) Pungufu au sawa na kg 2,000 ni shilingi 20,000, na Dola 40 kwa magari yasiyo na usajili wa Tanzania.
(ii) kati ya kg 2001 – 3000 ni shilingi 35,000, na Dola 150 kwa magari yasiyo na usajili wa Tanzania.
(iii)Kati ya kg 3001 – 7,000 ni shilingi 60,000, na Dola 200 kwa magari yasiyo na usajili wa Tanzania
(IV)Kati ya kg 7001 – 10000 ni shilingi 150,000 na Dola 300 kwa magari yasiyo na usajili wa Tanzania.
(V)Magari ya wazi yatatozwa asilimia 50 zaidi.
(r) Tozo kwa wanafunzi watanzania kutoka vyuo/ shule za Tanzania baada ya kuomba kibali na kupata kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu/ Mkuu wa Hifadhi ni shilingi 1,000. Na wanafunzi ambao sio watanzania watatozwa Dola 10. Kibali kitahusu tozo za hifadhi tu, tozo nyingine zitalipwa kama zilivyo.
(s) Kibali maalumu kwa Wakurugenzi wa makampuni ya utalii (Director’s pass) ni Dola 100.
(t) Tozo kwa watanzania wanaosafiri/ kupitia hifadhini kwa magari ya kubeba abiria ni shilingi 2,000.
(u) Tozo kwa watanzania wanaosafiri kupitia hifadhini na magari binafsi ni shilingi 5,000.
NB: TOZO HIZI NI BILA VAT 18%.
TOZO HIZI ZINAWEZA KUBADILIKA MUDA WOWOTE
MALIPO YANAFANYIKA KWA KADI ZA TANAPA ZINAZOTOLEWA NA BENK YA CRDB PIA KAD ZA VISA NA MASTER ZINATUMIKA.
WAKURUGENZI WA MAKAMPUNI WENYE VIBALI HAWARUHUSIWI KUONGOZANA NA WAGENI.
WAGENI WAKAZI (EXPATRIATE WANAWEZA KULIPA KWA FEDHA ZA KITANZANIA (TSH).
KITAMBULISHO NI MUHIMU KABLA HUJAINGIA HIFADHINI
TOZO ILIYOLIPWA HAIWEZI KURUDISHWA,
Nawashukuru sana kwa kusoma makala hii hadi mwisho, tuendelee kujifunza na kufahamu utaratibu wa hifadhi nyingine za Taifa; kwa maoni na ushauri zaidi kama unataka kutembelea hifadhi ya Taifa ya Arusha usisite kuwasiliana na uongozi kwa msaada zaidi. www.tanzaniaparks.go.tz au simu 255 767 536 136.
Karibuni sana Hifadhi ya Taifa ya Arusha.
Asante sana!
Hillary Mrosso
+255 683 862 481
www.mtalaamu.net/wildlifetanzania