Habari rafiki msomaji wa mtandao wako wa Wildlife Tanzania. Kuna vitu vingi sana nimepanga nivifanye kwenye mtandao huu, kuna mambo mengi sana nataka tuyajue kuhusu wanyamapori, hifadhi za Taifa na masuala ya utalii. Kwa kuanza nitaanza na hifadhi zote nilizotembelea, baadaye nikushirikisha pia hata zile ambazo sijazitembelea. Hii ni habari njema sana kwako msomaji wangu. Nataka upate ufahamu wa kutosha kuhusu hifadhi zetu na hatimaye ujue ni hifadhi gani nzuri kwako kuitembelea. Kazi yangu hapa itakuwa ni kukupa maarifa na taarifa za kila hifadhi za Tanzania. Hivyo nimejifunza mambo mengi sana na ninataka nikushirikishe wewe pia upate ufahamu kuhusu wanyamapori, hifadhi za taifa na masuala yote ya utalii kwa nchi yetu. Hivyo nakukaribisha ufuatane nami kwa siku kumi zijazo ili ujue kwa undani niliyokuandalia karibu.
Nimepanga kwa siku zisizo pungua kumi nikushirikishe maswala yote kuhusu hifadhi mbali mbali za taifa, na vivutio vyake vyote, vitu muhimu vya kwenda kutembelea na pia nitakushirikisha historia fupi ya hifadhi husika. Najua mambo mengi ya utalii yameandikwa kwa lugha ya kingereza ambayo haiwalengi watanzania moja kwa moja ingawa vitu vyote vinapatikana hapa kwetu. Kwenye kila makala niliyoandika nimetumia lugha ya Kiswahili ili ieleweke na wengi.
Watanzania wana uwezo mkubwa sana, watanzania wana pesa watanzania wanapenda wanyama, watanzania wanapenda utalii; hivyo kama watalamu kwenye mambo hayatunatakiwa kuwa msitari wa mbele kuwahamasisha watanzania kuwa na utamaduni wa kutembelea hifadhi za taifa na sehemu zenye vivutio.
Kwenye makala zijazo nimepanga kukushirikisha kwanza zile hifadhi zote ambazo nimetembelea mimi mwenyewe, kwa kuanza nitaanza na hifadhi ya taifa ya Manyara, hii ni hifadhi nzuri na ya ajabu sana, ina vivutioa vingi sana na, baada ya kuifahamu hutasubiri tena au kuhairisha tene kwenda kuitembelea, nitaichambua na kuielezea kwa namna rahisi na nyepesi kabisa ili kila mtu anayesoma apate kuielewa sawa sawa.
Makala hii ni makala ya ukaribisho na ya kukupa taarifa ili uzidi kufuatilia mfululizo huu mzuri wa kuzielewa hifadhi za taifa zilizopo Tanzania. Hivyo kwenye makala ya leo sitaeleza kila kitu kuhusu hifadhi ya manyara.
Ombi langu ni kwamba, unaposoma makala hizi usisite kuwashirikisha wengine ili kwa pamoja tuweze kujenga nchi yetu kwa kuongeza mapato ya nchi kupitia utalii wa ndani, na pia kwa kujenga tabia za kizalendo kwa nchi yetu.
Hivyo rafiki kwa leo sitakuwa na mengi ya kukwambia zaidi endelea kufuatilia makala hizi kilasiku, na nakuahidi kila siku kutakuwa na makala mpya kwenye mtandao wako wa wildlife Tanzania.
Karibu tuzifahamu Hifadhi zetu, karibuni hifadhini.
Hillary Mrosso
Wildlife Conservationist
0742092569