Habari msomaji wa makala zetu za wildlife Tanzania, karibu tuendelee na uchambuzi wa sheria ya uhifadhi wa wanyamapori ya mwaka 2009. Leo nitajibu swali la Rafiki yetu Kasekwa Maisha alilouliza jana baada ya kusoma makala ya jana ambayo niliandika kuhusu wanyama wa taifa wanaoruhusiwa kuwindwa. Niliandika tu bila kutaja hata mmnyama mmoja. Hivyo niliona kuna umuhimu wa kuwataja wanyama hao ambao nilieleza kuwa ni wanyama wa taifa wa kuwindwa. Kwa mujibu wa sheria ya wanyamapori kifungu cha 25. Kinaelezea tamko la Waziri wa maliasili na utalii kutamka wanyama wa taifa wanaoruhusiwa kuwindwa au wanyama wa taifa wanaowindwa.

Ili tuelewane vizuri nitawataja wanyama wote waliopo kwenye sheria hii ambao ni wanyama wa taifa wa kuwindwa. Katika kuelewa vizuri mpangilio wa sheria ii kwenye upande wa wanyamapori. Sheria hii imepangwa kwa Majedwali, ambapo kuna Jedwali la Kwanza ambalo linaelezea vifungu vya 18, 27 na 52 vya sheria hii na pia wanyama waliotajwa kwenye sehemu ya kwanza. Katika mpangilio huo wameandika jina la Kiswahili, jina la kingereza (English Name) na Jina la Kisayansi (scientific Name).

Hivyo tutakuwa tunaelezea wanyama wote waliopo kwenye majedwali husika ambao ni wanyamapori waliopo kwenye sheria hii, kama unayo sheria ya wanyamapori namba 5 ya mwaka 2009, basi unaweza kuona mwishoni mwa sheria hii kuna majedwali mbali mbali yanayoelezea wanyama waliopo. Hivyo basi kwa leo tutaweka WANYAMA WA TAIFA (NATIONAL GAME) hapa ili kila mtu awajue na kuwaelewa.

Orodha ya Wanyama wa Taifa (NATIONAL GAME). Hawa ni wanyama ambao wametajwa kwenye Jedwali la Kwanza Sehemu ya III ya sheria hii.

Jina la Mnyama -Kiswahili Jina la Mnyama- Kingereza Jina la Mnyama- Kisayansi
Fisi maji African Clawless Otter Aonynx capensis
Fisi Maji Spotted Necked Otter Lutra maculicolicollis
Kiboko Hippopotamus Hippopotamus amphibious
Korongo Roan Antelope Hippotragus aequinus
Kuro-ndogoro Waterbuck-Common Kobus ellipsiprymnus (Ogillby)
Kuro- singisi Waterbuck-Defassa Kobus defasa (Reppell)
Mamba Nile Crocodile Crocodylus niloticus
Mbuni Ostrich Struthio camelus (Linnaeus)
Nyamera Topi Damaliscus korrigum (Ogilby)
Palahala (Mbarapi) Sable Antelope Hippotragus niger (Harris)
Pofu (Mbunju) Eland Taurotragus oryx (Pallas)
Tandala Kubwa Greater Kudu Strepsiceros strepsiceros (Pallas)

 

Pia ikumbukwe kuwa wanyama hawa wanaweza kubadilishwa kutokana na hali ya mwenendo wao wa ikologia, au endapo mabadiliko ya sheria. Majina hayo ya wanyama wa taifa niliowataja kuwa ni wanyama wa taifa ni kwa mujibu wa sheria ya uhifadhi wa wanyamapori namba 5 ya mwaka 2009. Hivyo endapo mabadiliko ya sheria yatatokea au endapo kutakuwa na mabadiliko yoyote yale kwenye orodha ya wanyama hawa tutawajulisha hapa. Hivyo endelea kufuatilia na kutoa maoni yako kupitia mtandao huu wa wildlife Tanzania. Pia kwa mujibu wa sheria hii ya wanyamapori ya Tanzania sijaona ndege wakitajwa kuwa ni wanyama wa taifa isipokuwa mbuni (Ostrich), ambaye ndiye ndege mkubwa kuliko wote wa ardhini.

Pia wapo ndege wengi wanaoruhusiwa kuwindwa (Game Birds) ambao tutawaorodhesha hapa kwenye makala ijayo. Hivyo ni ndege wanaowindwa lakini sio ndege wa taifa. Aidha wapo wanyama wengine wengi wa kuwindwa wakubwa kwa wadogo, kuna wapo amphibia na reptilia ambao wanaruhusiwa kuwndwa. Wapo kwenye majedwali ya sheria hii.

Nakushukuru kwa kusoma na kufuatalia blog hii. Nakukaribisha kwa ushauri, maswali na mapendekezo. Lengo letu ni kutoa elimu hii ya wanyamapori kwa watanzania ili kwa pamoja tushiriki kwenye uhifadhi wa maliasili zetu.

Hillary Mrosso

Wildlife Conservationist

+255 683 248 681/+255 742 092 569

hillarymrosso@rocketmail.com

www.mtaalamu.net/wildlifetanzania