Habari msomaji wa makala hizi za wildlife Tanzania, karibu tena siku ya leo tjifunze jambo muhimu ili kuendeleza na kufanya kazi zetu kwa weledi sana. Elimu na maarifaa ni jambo muhimu sana kwenye nyanja yoyote ile, ili tuweze kufanya kazi vizuri kwenye sehemu yoyote ile, taarifa sahihi ni muhimu kuliko vyote. Kwenye makala hii nitazungumzia umuhimu wa kuwa na maarifa na kujifunza zaidi ili kufanya kazi sawa, naamini katika kujifunza mara kwa mara naamini katika kupata elimu sahihi ili watu waweze kufanya kazi kwa weledi na ufanisi mkubwa.

Jinsi siku zinavyokwenda mabadiliko yanayotokea yanatulazimu na sisi tubadilike mapema ili tusiachwe nyuma, kila mabadiliko yana faida zake. Kwa sekta ya wanyamapori ni muhimu sana tukajifunza kufanya kazi kwa ufanisi kwa kutumia mabadiliko haya vizuri. Kila kitu kinaweza kuboreshwa zaidi, na kumbuka hakiwezi kuboreshwa zaidi kama sisi hatutajifunza mara kwa mara. Kujifunza mambo mapya ndio kunaleta mabadiliko.

Katika sekta ya wanyamapori lazima tujifunze na kupata maarifa mbali mbali kwenye sekta hii. Siku hizi kila kitu kipo wazi sana, kama unataka kujua kitu fulani unaweza kukijua ndani ya muda mfupi. Ujio wa simu za kisasa umechangia sana kukua kwa taarifa na kuzipata kwa urahisi sana. Ni vizuri tukatumia fursa hii sana kama wahifadhi na watu wengine wanaofanya kazi kwenye sekta hii muhimu, unaweza kutumia simu yako kuangalia na kujifunza mambo ambayo huyajui, na hapo sio lazima uingia darasani lakini popote pale ulipo unaweza kujifunza ili kuboresha ufahamu wako na kazi yako pia.

Kuna watu wengine kwenye sekta hii tangu amalize masomo yake ya chuoni hajawahi kusoma hata kitabu na unakuta mtu huyo yupo kwenye sekta hii nyeti. Yani tangu mtu apate kazi kwenye hajwahi kujifunza au hata kusoma kitabu au majarida mbali mbali kuhusu hifdhi na mambo mengine ya wanyamapori. Ni muhimu kuwa na nidhamu ya kusoma na kujifunza kupitia njia mbali mbali. Kama kusoma vitabu, kusoma makala kama hizi kwenye hii blog, au makala nyingine za kitafiti zilizofznywa na watu mbali mbali kwenye sekta hii, hii itatupa ufahamu na uelewa mzuri na kufahamu kinachoendelea kwenyesekta hii.

Katika sekta hii kuna mambo mengi hatuyajui kuhusu wanyama, mimea, na watu wanaozunguka hifadhi au maeneo yaliyohifdhiwa, hivyo kama utakuwa mvivu kujifunza vitu mbali mbali utaachwa nyuma sana na pia utakosa taarifa muhimu sana. Hivyo nakushauri sana rafiki na msomaji wa makala hii, soma soma, jifunze jifunze jifunze, jiwekee utaratibu wako binafsi wa kusoma na kujifunza vitu vipya. Ijue kiundani kazi yako na mambo yote yanayoendelea kwenye kazi yako.

Hata kama hujapata kazi na unataka kufanya kazi kwenye sekta hii, jifunze, jifunze sana, hata kama upo nyumbani endelea kujifunza endelea kupata maarifa usijisahau, soma makala, soma majarida soma tafiti za kisayansi, soma vitabu. Pitia notsi zako za nyuma, jikumbushe vitu muhimu ulivyojifunza ukiwa shule au chuoni, pata maarifa. Vile vile kwenye sekta hii tunakutana sana na wageni wengi wanaoongea kingereza, hivyo na wewe usiwe nyuma kwenye hilo, jifunze lugha ya kingereza na pia jifunze ili uweze kuwasiliana na watu wengine,vile vile kama utajiongeza jifunze lugha nyingi uwezavyo utajiweka mahali pazuri sana, jifunze sana .

Nakutakia kila la Kheri kwenye kazi yako;

Hillary Mrosso

Wildlife Conservationist

0742092569/0683248681

hillarymrosso@rocketmail.com