Wadudu ni aina wanyama wadogo wasio na uti wa mgongo, wanyama waitwao wadudu wana miguu kwa kawaida na baadhi yao wanamabawa (kama vile nyuki, nyigu, kumbikumbi, kipepeo n.k) na baadhi hawana mabawa (kama vile buibui, jongoo, nng’e, tandu n.k). Moja ya mambo ya kuvutia zaidi kuhusu wadudu ni utofauti wao, kwani ni zaidi ya 80% ya viumbe hai vyote Duniani. Kuna zaidi ya spishi milioni moja za wadudu zinazojulikana na wanasayansi, wanakadiria kuwa kunaweza kuwa na hadi milioni 30 zaidi ambazo hazijagunduliwa bado, kwani wadudu waliopewa majina ni sehemu ndogo tu ya wadudu walio katika asili (ikolojia).
Wadudu wanaweza kupatikana karibu kila mahali kwenye sayari ya dunia, hata kwenye bara la baridi yaani Artic. Jamii nyingi za wadudu wanaishi ardhini, lakini wengine wanaishi katika maji safi (maji yasiyo na chumvi/maji baridi), na wachache wanaweza kupatikana wakiishi katika bahari. Juu ya ardhi wadudu wanaweza kupatikana juu ya miti, ndani ya udongo, wachache hupatikana hewani wakiruka mchana na usiku,au kutambaa juu ya ardhi .
Wadudu wanakula karibu kila kitu hata vitu ambavyo tunaweza kudhani haviwezi kuliwa! Wadudu huweza kula chochote wanachoweza kupata katika mazingira yao, na wakati mwingine hulazimika kuhama mazingira kwa ajiili ya kujipatia chakula. Hii inaweza kujumuisha nekta, chavua, matunda, majani, kuni, na hata wadudu wengine. Wadudu wengi huishi kwa mlo unaojumuisha hasa mimea na matunda. Baadhi ya wadudu kama vile vipepeo, nondo, nyuki n.k, wanakula kutoka kwenye mimea huku wengine wakipendelea nekta tamu au utomvu wa sukari. Wadudu wengine hulisha wadudu wengine kama vile aphids na viwavi, baadhi ya wadudu pia hufurahia vyakula vya kufurahisha kama vile umande wa asali kutoka kwa wadudu wadogo au mealybugs ambao mara nyingi wanaweza kupatikana katika bustani au mashamba. Ingawa milo mingi ya wadudu hujumuisha hasa mimea, kuna jamii za wadudu wanaokula nyama na baadhi hula chochote wanachokipata mfano wake ni chungu(ant).Wadudu hutumia mbinu mbalimbali kujipatia riziki yao kama vile kufyonza majani na mashina ,kutafuta nyufa ili kupata vitu vilivyofichwa na wengine hutumia mbinu mbalimbali za uwindaji ikiwa ni pamoja na kuvizia mawindo kwa mielekeo ya haraka ya umeme au hata kunyemelea.Wadudu wanauwezo mkubwa wa kuzaliana na kuongezeka kwa wingi na haraka, hii husaidia marekebisho kutokea na kuwepo katika ikolojia kwa wakati wote.
Picha na Rodrin: Picha kuonyesha aina mbalimbali za wadudu
Wadudu ni moja kati ya makundi muhimu Zaidi katika ulimwengu wa asili kwani wanaathiri maisha na ustawi wa wanyama, mimea na binadamu kwa njia nyingi tofauti ingawa baaadhi ya makundi machache ya wadudu yanamadhara kwa maisha ya viumbe wengine vilivyopo katika uso wa nchi, hata hivyo aina hizo hazijathibitishwa kuwa ni hatari, lakini kuna aina za wadudu ambazo hazijulikani kuwa na faida au hatari katika mfumo wa ikolojia.
Miongoni mwa faida chanya za wadudu ni:
- Chakula kwa viumbe mbalimbali kama binadamu, ndege, kakakuona n.k. Wadudu wametumika kama chanzo cha chakula cha watu kwa miaka mingi sasa na bado ni desturi inayofanywa katika sehemu mbalimbali na jamii nyingi kama Kabila la Wahaya kutoka nchini Tanzania; hawa hutumia senene(jamii ya panzi) kama chakula cha utamaduni wao. Wadudu wana umuhimu sana kwa baadhi ya wanyamapori na ndege, kwani huwategemea kama chakula chao kikuu mfano; kakakuona hutegemea sana uwepo wa chungu na mchwa kwaajili ya kuishi. Asali Kama tunavyojua, hii ni tunu tamu iliyotengenezwa na nyuki wa asali kutoka kwa nekta ya mimea. Nyuki wa asali ni wadudu wanaofanya kazi kwa bidii sana kutengeneza na kuhifadhi asali kwenye sega katika mzinga wao. Asali hiyo Inatumiwa kwa chakula na jamii karibu zote ndani na nje ya Tanzania. Pia matumizi ya mdudu chili(kriketi) kama chakula cha heshima kwa baadhi ya tamaduni mbalimbali zilizo nje ya Tanzania.
Picha ya baadhi ya jamii wanazotumia chili(kriketi) kama chakula
2.Udhibiti wa Kibaiolojia; Udhibiti wa kibaiolojia ni matumizi ya wadudu na vimelea kupunguza idadi ya wadudu waharibifu. Wakati kundi fulani la wadudu wanatishia na kuharibu mazao, jamii nyingine ya wadudu hawa wenye manufaa wanaweza kutolewa kula wadudu waharibifu na kudhibiti uharibifu kwa njia ya asili. Katika baadhi ya maeneo yaliyoendelea kwa kutumia njia za asili kudhibiti uharibifu kwa mazao, mfano, matumizi ya chungu maji ya moto kudhibiti wadudu wanaopaa waharibu matunda kwa kuwatumia kama chakula. Pia baadhi ya wadudu wanaokula magugu fulani wanaweza kuwekwa katika eneo la uhifadhi au shamba ili kuzuia magugu kuenea
3. Uchunguzi wa vifo vya wanyamapori au binadamu : Wahusika wakuu ni wadudu aina ya Inzi ,hawa huwa wa kwanza kufika kwa mnyama aliyekufa, na wao ndio wa kwanza kukamilisha ukuaji na kuondoka. Spishi nyingine hufuata baada ya muda katika mlolongo unaoweza kutabirika kadri mwili unavyooza. Mabadiliko haya katika muundo wa spishi za uchakataji wa mwili uliooza huitwa mfululizo wa wanyama. Mfululizo huu unaweza kusaidia Wataalamu wa Wadudu na uchunguzi kubainisha wakati wa kifo mwili unapopatikana.
4. Wadudu na kemikali zinazotolewa kutoka kwa baadhi ya wadudu zimetumika kusaidia katika matibabu; kuna namna nyingi wadudu husaidia katika kutibu baadhi ya magonjwa kama matumizi ya asali inayotokana na nyuki hutumika kutibu michubuko ili kuzuia maambukizo, au kutuliza koo. Inatumika pia katika bidhaa za urembo, na kama nyongeza ya nishati asilia kwenye ngozi na nywele. Tiba ya sumu ya nyuki; Sumu ya nyuki ni muundo tata wa vimeng’enya, protini na asidi ya amino, ambayo huiga kutolewa kwa cortisol (homoni ambayo mwili huweka wakati unasisitizwa). Uchunguzi unaonyesha kuwa sumu ya nyuki inaweza kuboresha afya kwa wenye dalili za maambukizi katika mfumo wa upumuaji.
Picha na Stefan stangaciu: Baadhi ya faida za nyuki (asali,uchavushaji na matibabu)
5. Ushonaji wa majeraha ya kukatwa kwa kutumia wadudu aina ya chungu (ant); wakati ngozi imekatwa sana, mishono huhitajika ili kufunga jeraha. Katika tamaduni fulani chungu walitumiwa kushona majeraha kwakushikilia ngozi pamoja; chungu mwenye taya kubwa (kama vile jeshi au chungu mkata majani) hukamatwa na kuweka mdomo wake kwenye kidonda na kungoja aume , kisha mwili utolewa na kichwa kikiachwa na mdomo wa chungu huyo ukibana ngozi pamoja.
Picha: 1. Namna chungu huwekwa kwenye jeraha; 2. Chungu walivyotumika kufunga jeraha
6. Wasafishaji wa mazingira wa asili; Kuna wadudu wengi ambao hula rasilimalii, hii inajumuisha majani yanayoanguka kutoka kwenye mti, wanyama waliokufa, mimea na kinyesi huzivunjavunja na kuzichakata kuwa virutubisho vinavyosaidia mimea kukua. Kuna jamii nyingi za wadudu zinazokaa kwenye udongo na kuni ambazo hupasua majani au handaki kwenye miti iliyokufa, hii husaidia mimea kuoza haraka na baada ya muda hufanyika aina ya udongo wenye virutubisho kwaajili ya ukuaji wa mimea. Kwa wadudu wanaokula wanyama waliokufa (mizoga) na kula nyama iliyooza wakiwemo mende, nzi, nyigu na mchwa n, k; hujitokeza na kula mzoga kwa muda mfupi na kusaidia kuzika kwa haraka nyama inayooza.
7. Uchavushaji; Zaidi ya 75% ya mimea yote inayotoa maua, na 75% ya mazao yetu hutegemea wanyama kubeba chavua kutoka ua moja hadi jingine na wengi wa wachavushaji hawa ni wadudu. Wengi wetu hufikiria nyuki tunaposikia neno wachavushaji, lakini, sio tu nyuki wa asali ambao huchavusha mimea, bali hata vipepeo, nondo, mende, na nzi pia hufanya kazi hii muhimu.
Picha ya baadhi ya wadudu wakichavusha maua ya mmea
Mbali na kuwa na faida hizi za muhimu kwa kuchangia viumbe wengine wanaishi, bado wito na mwamko wa kuhifadhi wadudu katika jamii nyingi ni mdogo na kupelekea viumbe hawa kutoweka kwa wingi katika ikolojia(asili) kwa kasi. Hivyo, ni wito wangu kwa wadau, wanajamii na mashirika mbalimbali ya uhifadhi kuweka nguvu katika kuzitambua aina za wadudu zinazo patikana katika mazingira ya asili na kujua namna ya kuhifadhi wadudu hawa kwaajili ya kizazi hiki na vinavyokuja.
Imeandikwa na; Marylove Shoo; Email;marylovegasper478@gmail.com; Simu:0783-682765.