Habari rafiki, karibu kwenye makala yetu ya leo ambayo tutakwenda kujifunza na kuijua Hifadhi ya Eneo la wanyamapori la Pole. Katika kujifunza na kufuatilia kwenye mitandao maeneo yote ya hifadhi ya wanyamapori nimegundua vitu vingi sana ambavyo hatuvijui kuhusu utajiri na maliasili tulizo nazo. Unaweza kusema Tanzania tuna maliasili na maeneo mengi ya wanyamapori lakini unaweza kuambiwa udhibitishe hilo ukashindwa kwa sababu unaweza ukawa unajua tu kuhusu Serengeti, Manyara, Mikumi na Kilimanjaro ukaishia hapo ukafikiri umemaliza, kumbe kuna maeneo mengine mengi sana kuliko unavyofahamu. Maeneo ambayo ni muhimu sana kwa ajili ya hifadhi ya wanyamapori na misitu. Karibu twende wote uone mambo ambayo huyajui.
Tanzania ina jumla ya maeneo ya asasi ya jamii au maeneo ya hifadhi ya jamii, au maeneo ya usimamizi wa wanyamapori au kwa kingereza yanaitwa Wildlife management Areas, maarufu kama (WMAS) 38. Maeneo haya yapo karibu kila mkoa wa Tanzania, kama ukiangalia kwa makini utaona tuna hifadhi nyingi sana ya maeneo ya wanyamapori kuliko mikoa yote ya Tanzania. Lakini katika idadi hiyo ya maeneo ya usimamizi wa wanyamapori 17 ndio yaliyo hai, nikimaanisha yanafanya kazi kama inavyotakiwa na sheria ya uhifadhi wa wanyamapori namba 5 ya mwaka 2009.
Kuanzishwa kwa maeneo haya kulilenga kuendeleza uhifadhi wa wanyamapori na rasilimali nyingine muhimu kwa kuwapa wananchi au jamii jukumu hilo la kusimamia na kutunza wanyamapori hawa. Na kwa kuwa maeneo mengi ni maeneo ya vijiji au ardhi ya vijiji ambavyo vimetoa sehemu ya ardhi yao kwa ajili ya kuunda jumuiya ya pamoja ya uhifadhi wa wanyamapori katika maeneo yao. Hivyo basi maeneo haya ya wanyamapori yanakuwa na majina kulingana na eneo la hifadhi hiyo au jina linaweza kuwa ni muunganiko wa vijiji wanachama wa jumuia hiyo nk.
Kwenye makala hii tutaelezea kidogo kuhusu Asasi ya jamii ya Ipole ambayo ipo katika mkoa wa Tabora, Wilaya ya Sikonge. Hii ni moja kati ya maeneo yaliyoendelezwa na kuhakikisha faida inayopatikana kutokana na shughuli za utaliii zinazofanyika kwenye eneo hili zinarudi moja kwa moja kwenye jamii na kuinufaisha jamii hiyo kwenye sekta mbali mbali za maendeleo ya vijiji wanachama.
Enao la hifadhi ya jamii ya Ipole lipo katika Wilaya ya Sikonge kilomita 96 kutoka Manispaa ya mkoa wa Tabora, eneo hili lenye ukubwa wa kilomita za mraba 2,540 limeundwa na vijiji vinne ambavyo ni Ipole, Msuva, Idekamiso na Itimula. Kabla ya kuanzishwa kwa eneo hili hapo mwanzo miaka ya 1954 lilikuwa ni Pori la Akiba na eneo la hifadhi msitu wa Akiba.
Mnamo mwaka 2006, eneo hili lilitangazwa kuwa eneo la hifadhi ya jamii ya Ipole hii yote ni kuifanya jamii kushiriki kwenye uhifadhi wa wanyamapori na kupata faida za moja kwa moja kutokana na mapato ya shughuli za utalii zinapatikana kwenye hifadhi ya eneo hili. Hivyo hata sasa jumuiya hii ya Ipole imeundwa na msitu wa akiba na pia eneo la hifadhi ya wanyamapori.
Eneo hili linalosifika kwa shughuli kuu ya utalii ikiwa ni ufugaji wa nyuki na asali, mamlaka za eneo hili zimaetoa ushiriki kwa wanajamii kufanya shughuli hizo ndani ya eneo lao. Pia shughuli za urinaji na ufugaji wa nyuki kwenye WMA hii umeipatia sifa kubwa na mvuto wa wageni kwenye hifadhii hii ili kuja kuona shughuli hii ambayo inawaingizia kipato wanajamii wa enbeo hili. Pia shughuli nyingine kuu ya utalii kwenye eneo hili ni Uwindanji wa kitalii. Shughuli za uwindaji zinaendehwa ndani ya WMA hii ambayo ndio imekuwa ikichangia mapato kwenye mfuko wa jumuiya hii ya Ipole. (ingawa kwa siku za karibuni Waziri wa Maliasili na Utalii Dr.Hamis Kigwangalla amesitisha vibali vyote vya uwindaji kwenye maeneo yote ya uhifadhi wa wanyamapori, tunaamini watakuja na mfumo mwingine mpya na mzuri zaidi kwenye jambo hili, hivyo shughuli za uwindaji wa kitalii zitakuja kuendelea). Pia moja ya mipango ya baadaye ya Hifadhi ya Ipole ni kuacha kabisa uwindajin wa kitalii na kukuza na kuendeleza utalii wa picha.
Hifadhi ya Ipole pia imepakana na Pori la Akiba la Mto Ugalla, upande wa kusini imepakana na Iyonga wakati upande wa mashriki imepakana na Pori Tengefu la Iyonga na Msitu wa akiba wa Iyonga, pia kwa upande wa Mashariki imepakana na Msitu wa Akiba wa Mpembazi. Hivyo ni eneo ambalo limepakana na maeneo mengine yaliyohifadhiwa kwa ajili ya wanyamapori na misitu. Pamoja na mambo mengine yaliyopo kwenye WMA ya Ipole kuna wanyamapori wengi sana kama vile tandala,simba,twiga, swala, tembo, chui, ngiri, fisi, muhanga, nyani, kima, korongo, palahala, kongoni nk.
Jinsi ya kufika katika eneo hili unatumia barabara kutoka Tabora hadi Sikonge ni kilomita 87, na kutoka Sikonge hadi Ipole ni kilomita 24. Pia unaweza kufika Ipole kwa kutumia barabara ya Mbeya Kitunda kwenda Ipole na pia unaweza kupitia Sumbawanga unapita Wilaya ya Mpanda hadi Iyonga kwenda Ipole. Vile vile kuna uwanja wa ndege wa Pori la Akiba la Ugunda kama kilomita 35 na Kalulu Kilomita 60. Kwa taarifa zaidi unaweza kutembelea website yao hapa http://www.twma.co.tz.
Ingawa kuna mambo mengi ya kuandika kuhusu Ipole, lakini nimehakikisha umepata yale ya muhimu sana kuhusu eneo hili la hifadhi ya jamii, naamini kupitia makala hii umefahamu baadhi ya mambo ambayo uliukuwa hujui, lakini pia kwa siku zijazo tutaendelea na kujifunza maeneo mengine mhuhimu ya uhifadhi wa wanyamapori. Hivyo endelea kufuatilia makala hizi na nyingine zijazo kwa mafunzo zaidi. Pia katika kujifunza mambo haya utaona kuna furasa nyingi sana za uwekezaji na biashara kwenye maeneo haya. Kwa kweli mimi sijawahi kufika kwenye hifadhi ya jamii ya Ipole, nimeisoma tu na kukushirikisha. Hivyo kwa wale walioko Tabora na mikoa mingine ya karibu wataelewa zaidi tuliyojifunza kwenye makala hii.
Kwa maoni, maswali, ushauri na mapendekezo usisite kuwasiliana nami kwa mawasiliano hapo chini
Hillary Mrosso
Ahsante sana!
Wildlife Conservationist
+255683 862 481/+255742 092 569