Kwenye kila kazi njema kuna baraka, kwenye kila kazi njema kuna thawabu. Kila tendo jema linalofanywa hapa chini ya jua kuna thawabu yake, hakuna jambo jema linalofanyika au tunalofanya hapa litapotea au kusahaulika. Kila tunachofanya kinaandikwa sehemu hakitapotea kamwe. Maisha yetu yanatakiwa kushuhudiwa wema kwa kila tendo jema. Uhifadhi na utunzaji wa maliasili zetu ni jukumu la kila mtu. Kuisha na kuendelea kupotea kwa wanyamapori na maliasili nyingine muhimu ni kutokana na sisi kukaa kimya kwenye mambo ambayo tulitakiwa kuyazungumza na kuyasema.
Kama vile alivyosema Mwanasayansi na Mwanamahesabu mkubwa duniani, Albert Eistain kwamba dunia inaharibiwa sio kwasababu ya watu wabaya lakini kwasababu ya ukimya wa watu wema. Katika Sehemu hii ya Kumi na Nane ya uchambuzi wa sheria ya wanyamapori namba 5 ya mwaka 2009. Mambo mengi sana yanaelezwa na sheria hii ambayo kila mtu anaweza kuyafanya kwa sehemu yakena pia kushirikiana na mamlaka husika ili ipatikane taarifa ya kukamatwa kwa wahalifu. Sambamba na hilo zawadi nzuri hutolewa kwa mtu atakayetoa taarifa hizo. Nisiseme sana ngoja tuone sheria inavyoelekeza, karibu.
117.-(1) Pale ambapo hatua za kisheria zitachukuliwa chini ya sheria hii na mkosaji kupatikana, mahakama inaweza, baada ya kupokea mapendekezo ya kimaandishi kutoka kwa Mkurugenzi, kutoa zawadi ya kiasi cha fedha kwa mtu ambaye ametoa taarifa zilizopelekea kukamatwa kwa mkosaji;
Ukizingatia kwamba-
(a) Kiasi cha fedha kinachotolewa kama zawadi kwa mtu yeyote au jumla ya kiasi hicho cha zawadi kitolewa kwa mtu zaidi ya mmoja kwa kila mtu moja hatatakiwa kuzidi-
- Asilimia kumi ya faini au jumla ya makusanyo ya faini iliotajwa au kuwekwa; au
- Asilimia kumi ya thamani ya nyara au nyara ambazo zimenyang’anywa na serikali kutokanana vitendo vya makosa; au
- Shilingi milioni tano (5,000,000),
Ufafanuzi kwenye sehemu hii muhimu ni kwamba, endapo mtu yeyote atakayetoa taarifa zitakazopekea kukamatwa na kushitakiwa na kukutwa na makosa ya kiuhalifu chini ya chini ya sheria hii ya wanyamapori. Sheria hii imetaja kiasi cha asilimia ya fedha ambayo itatolewa kama zawadi kusaidia kutoa taarifa hizi muhimu.
(b) Zawadi haitalipwa hadi baada ya kuisha kwa matumizi ya kipindi ambacho mshitakiwa au mtu aliyekuwa na hatia atakata rufaa dhidi ya hatia yake; au
(c) Licha ya mapendekezo ya kifungu (b), zawadi inaweza kulipwa mapema iwezekanavyo kwa kila kesi ambayo imeamuriwa na chini ya sheria hii itakapokuwa imetolewa na mahakama na kama Mkurugenzi atakavyopanga.
(2) Mkurugenzi anaweza kuruhusu malipo ya zawadi kwa mtu aliyetoa taarifa zilizopelekea kupatikana kwa nyara, ukamataji au kumtia hatiani mwenye makosa chini ya sheria hii.
(3) Kutegemeana na mapendekezo ya kifungu kidogo cha (2), Waziri anaweza kwa kutumia kanuni na kuchapisha kwenye Gazeti la Serikali, kurekebisha kiasi na malipo ya zawadi. Ufafanuzi wa sehemu hii ni kwamba Waziri anaweza kurekebisha na kuweka malipo ya zawadi au kumtia hatiani mtu mwenye hatia chini ya sheria hii.
119.-(1) Waziri, baada ya kushauriana na Waziri anayehusika na mambo ya ndani, na baada ya kutoa taarifa na kuchapishwa kwenye Gazeti la serikali, ataelezea njia na utaratibu maalumu wa kufuata na usajili wa mtu ambaye mwanzo alikuwa na hatia ya makosa dhidi ya wanyamapori.
(2) Baada ya kuchapisha taarifa chini ya kifungu kidogo cha (1), Mkurugenzi ataamuru jina la mtu yeyote aliyekuwa na hatia ya makosa yoyote kusajiliwa chini ya sheria hii pamoja na taarifa zinazohitajika kwa usaili kwa kila mmoja wao.
120.-(1) Pale ambapo mtu atakuwa na hatia ya kosa chini ya sheria hii, linalohusisha
(a) uwindaji, ukamataji au uuaji wa wanyama bila ruhusa ya maandishi kutoka kwa Mkurugenzi;
(b)uwindaji wa mnyama aliyetajwa au aliyepo kwenye jedwali bila lesseni au kibali kilichotolewa chini ya sheria hii;
(c)kumiliki kinyume na sheria au kuwathibiti kinyume na sheria, kufuga au kutunza mnyama au nyara, na mtu amehukumiwa kwenda jeala kwa kipindi cha miaka miwili au zaidi, Mkurugenzi atachukua na kusajili mtu huyo aliyehusika mambo yafuatayo-
(i) jina lake
(ii) picha zake za passpoti ambazo amepiga ndani ya mwezi huo kabla ya kuwa na hatia;
(iii) alama za mkono yake (finger prints);
(Iv) anuani yake kama anayo,au sehemu anayoishi ndani ya Jamhuri ya Muungano;
(v) aina ya silaha aliyotumia kufanyia uhalifu, kama anayo;
(vi) aina na asili ya kosa alilofanya; na
(vii) faini, kunyanganywa, usabiliaji au penalti au adhabu nyingine aliyopewa.
(2) Kila mtu atakayeendesha mashitaka kwa mtu ambaye ana hatia ya kosa lolote na kuhukumiwa kwa vigezo vya kifungu kidogo cha (1), atamtaarifu Mkurugenzi au mwakilishi wake hatia na mambo mengine kama Waziri atakavyoelekeza, baada ya kushauriana na Waziri anayehusika na mambo ya ndani ya nchi na baada ya kutoa taarifa kwenye Gazeti la serikali.
(3) Mkurugenzi ataendelea kutunza na kuhifadhi usajili ambao umenakili au kuandika jina la kila mtu ambaye anahatia na kwa makosa yoyote na kuhukumiwa kwa viwango vilivyoanishwa kwenye kifungu kidogo cha (1), pamoja na mambo yote yaliyotakiwa kusajiliwa chini ya kifungu hiki kwa kila mtu mwenya makosa.
(4) Licha ya mapendekezo na masharti yaliyoandikwa kwenye sheria hii, Waziri anaweza kupendekeza, kwa Waziri anayehusika na mambo ya ndani ya nchi, kusababisha mtu aliyepatikana na kuwa na hatia yoyote na kuhukumiwa kwa kufuatana na kifungu cha (1) na ambaye sio raia wa Jamhuri ya Muungano, kutangaza zuio la kusafiri kuja nchini na kufukuzwa mara moja nchini. Ufafanuzi kwenye kipengele hiki ni kwamba Waziri anaweza kutoa tangazo la kuzuia na kumfukuza raia wa kigeni anayeshikiliwa na kukabiliwa na makosa kwa mujibu wa sheria hii ya wanyamapori, Waziri wa Maliasili na Utalii atafanya hivyo tu baada ya kushauriana na Waziri wa mambo ya ndani ya nchi.
- Waziri anaweza kutunga kanuni kuelezea au kutamka mashrti kwenye jambo lolote linalohusiana na ;
(a) uhifadhi, usimamizi na matumizi ya wanyamapori;
(b)njia au kanuni za ukamataji wa wanyama chini ya sheria hii;
(c)fomu ya kufanya maombi kwa ajili ya lesseni, vibali, hati/ vyeti na nyaraka nyingine ambazo zinaweza kutolewa au kupewa chini ya Sheria hii.
(d)mambo yanayohusu CITES;
(e ) ada ya lesseni, vibali, vyeti na nyaraka nyingine ambazo zinaweza kutolewa au kupewa chini ya Sheria hii; na
(f)njia bora ya kutumia mapendekezo ya Sheria hii.
Hii ni sehemu nzuri sana inayotoa mkono wa shukrani kwa mtu yeote ambaye anatoa taarifa za kusaidia kupatikana kwa mwalifu, nyara na maliasili nyingine za serikali. Naamini kabisa kupitia makala hii umejifunza na kujua jinsi sheria hii ya wanyamapori inavyotambua mchango wa jamii kwenye vita dhidi ya ujangili na uharibifu wa maliasili.
Kwa upande wetu jamii, tunatakiwa kutoa ushirikiano na kufichua vitendo viovu vinavyofanywa na watu wenye nia mbaya dhidi ya maliasili zetu. Tukishirikiana kwa pamoja tutafika mbali na tutakuwa wazalendo wa kweli kwenye nchi yetu na maliasili zetu.
Ahsante sana!
Hillary Mrosso
Wildlife Conservationist
+255 683 248 681/+255 742 092 569
www.mtaalamu.net/wildlifetanzania