(The extinction of one species will lead to the extinction of other species)

Habari msomaji wa wildlife Tanzania, karibu kwenye makala ya leo ambapo tunaangalia mfumo wa ikologia ambao unaunganisha viumbe hai kwa kutoa mazingira mazuri na makazi yake. Mfumo wa maisha katika ikologia ya wanyamapori na msitu umetengenezwa kwa namna ya kutegemeana. Katika hali ya kutegemeana kwenye mazingira hakna aliye bora kuliko mwenzake wala hakuna kiumbe hai aliye dahifu kuliko wenzake, tukiangalia mfumo wa kutegemeana kwenye mazingira utakuta mpaka binadamu anahusika kwa kiasi kikubwa kuboresha au kuharibu mazingira ya viumbe hai.

Kama kichwa cha habari hapo juu kinavyoeleza, kutoweka kwa spishi moja kutapelekea kupotea kwa spishi nyingine, na hapa ni kwa kila kiumbe hai nikimaanisha mimea na wanyama. Hivyo kwenye maswala mazima ya uhifadhi wa wanyamapori mambo ya msingi yanayotakiwa kufundishwa hata kwa jamii yetu ni namna viumbe hai wanavyotegemeana kwenye mazingira. Na jamii nzima ikiwa na ufahamu wa namna hii wataweza hata kuwaelimisha watu wengine kwenye suala zima la uhifadhi wa mazingira na faida zake.

Sisi wenyewe ni mashahidi wa mambo haya hapa duniani, pale ambapo watu wamechoma misitu mikubwa ya hifadhi ya viumbe hai, pale ambapo tumeacha mazingira kuharibika kwa kutokuwa na mfumo mzuri wa uhifadhi wa mazingira na pia  moshi wa viwandani hivyo kusababisha mabadiliko ya tabia nchi. Kuna nchi za Ulaya ambapo mvua nyenye asidi hunyesha na kuua kabisa viumbe hai na kuharibu mazingira yake. Kunyesha kwa mvua ya asidi ni kutokana na uchafuzi wa hewa ambayo ndo husaidia kutengeneza mawingu yanayotoa mvua.

Kwa upande mwingine matumizi ya madawa ya viwandani na madawa ya shambani ambayo huelekezwa kwenye vyanzo vya maji au kwenye makazi ya viumbe hai imekuwa inasababisha uharibifu mkubwa sana kwenye makazi na mazinira ya viumbe hai. Tukae tukitambua kwamba kupotea kwa spishi moja au kiumbe hai moja kutapelekea kutoweka kwa viumbe hai wengine. Hii ni kutokana na ukweli wa asili ambao uliwekwa na Mungu mwenyewe. Endapo utaratibu wa kutegemeana kwenye mazingira utaharibiwa maisha na mifumo ya ikologia itaharibika na kusababisha viumbe hai kukosa mahitaji yao ya msingi na kuanza kutoweka.

Mfano endapo swala watapungua wanyama wanaotegemea kuisha kwa kula swala nao watapungua na kusababisha maisha yao kuwa magumu, hivyo uwezekano mdogo wa kuendelea kuishi miaka mingi hupungua na atimaye kutoweka kabisa na janga hilo kuendelea kutokea hadi pale mfumo utakapokuwa mzuri na imara.

Kazi ya msingi inabaki kwetu ambao tumepewa dhamana hii kubwa ya kuhakikisha usalama na uhifadhi wa viumbe hai unaendelea kuwepo kwa vizazi vingi vijavyo ili Tanzania iwe sehemu salama ya kuishi sio wat utu bali hata viumbe hai wengine.

Ahsante sana!

Hillary Mrosso

Wildlife Conservationist

+255 683 862 481/+255 742 092 569

hillarymrosso@rocketmail.com

www.mtaalamu.net/wildlifetanzania