Huyu ni mnyama aina ya tembo ambaye kwa historia fupi ndiye mnyama mkubwa kuliko wote ambao wanaishi nchi kavu. Kuna aina tatu za Tembo ambazo ni ;Tembo wa Asia (Asian elephant),Tembo wa msituni(African forest elephant) na Tembo wa Nyika au vichakani (African Bush elephant). Aina hii ya tatu ya Tembo ndio kubwa kuliko nyingine na jina lake la kisayansi ni Loxodonta Africana. Tembo hawa hupatikana katika nchi zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara ikiwemo Tanzania na wanaurefu wa pata futi 8 mpaka 13, anauzito wa wastani Kilo2500 mpaka 7000 na wana uwezo wa kuishi hadi miaka 70.
Chakula
Kwa siku Tembo anauwezo wa kula kilo zisizo pungua 136 ambazo zina mchanganyiko wa mizizi, majani,magome ya miti na matunda.,
Kuzaliana
vilevile jike hubeba mimba kwa muda wa miezi 22 na kuzaa ndama mwenye kilo yapata 120 kilogramu.
Uongozi
Kama ilivyo kawada ya maisha ya viumbe hai mbalimbali, ikiwemo binadamu katika sualazima la uongozi, vile vile familia ya Tembo huongozwa na huongozwa na Tembo Jike ambaye ni mkubwa kiumbo na umri . Miongoni mwa kazi za tembo huyu kiongozi ni pamoja na kuliongoza kundi katika kutafuta chakula maji, n.k wakati wote wa maisha yao. Vile vile huyu ndio kiongozi wa misafara misafara ya tembo kutoka sehemu moja kwenda nyingine ambayo hupita katika shoroba mbalimbali.
Tembo jikee akiongoza familia (Picha na national Geographic)
Sababu za Tembo kuitwa Mhandisi wa mfumo wa Ikolojia
- Tembo hutumia meno yake mawili yaliyotokeza nje ya mdomo kuchimba kwenye mito iliyokauka ili kupata maji ambayo huwanufaisha wao pamoja na wanyama wengine .
- Kinyesi cha Tembo ni chakula kwa wanyama wa aina mbaimbali kamavile jamii ya nyani na ndege. Mende Miwa(dung beetle)
- Kinyesi cha tembo mara nyingi huwa na mchanganyiko wa mbegu za aina mbalimbali ambazo huweza kuota sehemu ambayo amejisaidia na hivyo kusaidia kusambaza au kuotesha mimea ambayo haikuwepo eneo hilo.
- Tembo hung’oa miti kwa ajili ya chakula ambayo vile vile husaidia wanyama wengine kama Pundamilia ambao hupenda kula kwenye mazingira ya wazi.
- Wanyama hawa husaidia kufungua njia kwa kuangusha vichaka na hivyo kuwafanya wanyama wengine wapiti kwa urahsi.
- Mahali ambapo Tembo hukanyaga huacha alama za miguu mithili ya mashimo ambayo huwahifadhi viumbe wadogo kama chura ,haswa wakati wa mvua kwa kuyatumia mashimo hayo kwa kujisitiri na wkati mwingine kuzaliana. .
Vifaa ambavyo Mhandisi Tembo hutumia
- Mkonga
Tembo hutumia kiungo hiki katika kupiga kelele ambazo huashiria mambo mbalimbali kama vile salamu, kufarijiana kama ilivyo mkono kwa binadamu, Kunusa, kupumua,kushikia vitu haswa chakula, kuchota maji ya kunywa na kuogea! Mhandisi Tembo huoga maji,vumbi au matope ikiwa na lengo la kujipoza na kujikinga na miale Mikali ya jua.
- meno
Haya ni meno mawili ambayo hayaachi kukua na hutumika katika kuchimba maji wakati wa kiangazi, kumegua magome ya miti kama mbuyu, kupigana hususani kwa tembo dume katika kipindi cha kuzaliana
HITIMISHO
Tembo ni miongoni mwa viumbe walio mbioni kutoweka kutokana na Ujangili na kukosekana kwa makazi yao ambayo yamesababishwa na binadamu kufana shughuli zao za maendelea kama vile mashamba, barabara, nyumba n.k. Ongezeka la mahitaji haya ya binadamu ikiwa ni pamoja na idadi ya watu kumechangia kuongezeka kwa migogoro baina ya tembo na binadamu hususani pale wanyama hawa wanapoharibu mazao yao kama vile migomba, mahindi, matunda na kuhatarisha maisha ya wananchi .
Shukrani za pekee ziende kwa mhariri wa makala hii Alphonce Msigwa (Mwikologia hifadhi za Taifa Tanzania)
Ashasanteni sana!
Maureen FN Daffa
maureen.nick08@gmail.com
+255 626 331 871.