Habari msomaji wa makala za wildlife Tanzania, karibu  kwenye makala ya leo, tunaelekea elekea ukingoni kabisa mwa uchambuzi wa sheria hii ya wanyamapori ya mwaka 2009. Leo tunaangalia majedwali yaliyopo kwenye sheria hii, ambayo yana wanyama walioainishwa kwa makusudi mbali mbali. Jana tulichambua na kuangalia wanyama wa jedwali la kwanza la sehemu ya kwanza tulijifunza wanyama  na ndege wote waliopo kwenye jedwali hili, ambapo wamegawanyika kuna, amphibia, reptilia na ndege. Kwa wanyama tuliowachambua jana ni tofauti na waleo wanyama wa jana sio game animal, yaani sio wanyama wa kuwindwa. Katika jedwali la pili linaonyesha wanyama wa Taifa (National game) ambao wanaruhusiwa kuwindwa kwa kibali maalumu.

Kuna makala ya nimewahi kuandika kuhusu wanyama wote wa Taifa na kuwaelezea kidogo, hivyo basi katika makala ya leo sitaeleza wanyama wa sehemu ya pili, bali nitaelezea waliopo kwenye jedwali la tatu ambalo linaorodha ya wanyama wa kuwindwa inayojulikana kama Big Game, pia sehemu hii inaelezea wanyama wengine wote. Karibu twende pamoja ili tuwaelewe wanyama hawa. Katika makala hii nitawataja kwa majina yao yote la Kiswahili, kingereza na jina la kisayansi. Karibu sana msomaji wangu tujifunze kwa pamoja hapa.

Jina la Kiswahili Jina la Kingereza Jina la Kisayansi
Bweha dhahabu Golden Jackal Canis aureus
Bweha masikio Bat-Eared Fox Otocyon megalotis
Bweha Miraba Striped Jackal Canis adustus
Bweha shaba Silver- Backed Jackal Canis megalotis
Chatu Phython Phython sebae
Choroa Oryx Oryx beisa
Chui Leopard Panthera padus
Dikidiki (Sunguya) kirkii Dikdik Rynchotragus
Dondoro Stainbok Raphiceros campetris
Dondoro- shapi sharpie Sharpe’s Grysbok Nototragus
Fisi (Kingugwa) Spotted Hyena Crocuta crocuta
Fisi maji Otter Aonyx/Lutra
Fungo civetta Civet Cat Civettictis
Funo (Mbatuka) Red Duiker Cephalophus natalensis
Kalunguyeye Hedgehog Erinaceus pruneri
Kamendegere kapensis Jumping hare Pedetes
Kanu Genet cat Geneta genetta
Kiboko Hippopotamus Hippopotamus Africanas
Kicheche Zorilla Ictonyx striatus
Kima Monkeys Cercopithecus spp.
Kimburu Wild cat Felis lybica
Komba Bush baby Galago senegalensis
Kongoni Cokes Hartebeest Alcelaphus buselaphus cokii
Konzi Lichtenstein’s Hartebeest Alcelaphus buselaphus lichtensteinii
Korongo Roan Antelope Hipotragus aequinus
Kuro ndogoro Common Waterbuck Kobus ellipsiprymus
Kuro singsing Defassa Waterbuck Kobus defassa
Mamba Nile Crocodile Crocodylus niloticus
Mbega mwekundu Red Colobus Monkey Colobus badius
Mbega mweupe Black and White Colobus abyssinicus Colobus makey
Mbuni Ostrich Stuthio camelus
Mbuzi mawe Klipspringer Oreotragus oreotragus
Mondo Serval Cat Felis serval
Ndimba Blue Duiker Cephalophus monticola
Ngiri Warthog Phocochoerus aesthipicus
Nguchiro Mongoose Viverridae
Nguruwe Bush pig Potamocherus porcus
Nsya Common Duiker Sylvicapra grimmia
Nungunungu Porcupine Hystrix cristata
Nyamera Topi Damaliscus korrigum
Nyani mwekundu Olive Baboon Papio anubis
Nyani njano Yellow Baboon Papio cynocephalus
Nyati (Mbogo) Buffallo Syncerus Caffer
Nyegere Honey Badger Mellivora capensis
Nyumbu kidevu cheupe White bearded Wildebeest Cannochaetes taurinus albojubatus
Nyumbu kusi Nyasa Wildebeest Cannochaetus taurinus taurinus
Nzohe Sitatunga Tragelaphus spekei
Paa Suni Neotragus moschatus
Palahala (Mbalapi) Sable Antelope Hippotragus niger
Perere Tree Hyrax Dendrohyrax boreus/ validus
Pimbi Rock Hyrax Heterohyrax syriacas
Pofu (Mbunju) Eland Taurotragus oryx
Pongo (Mbawala) Bushbuck Tragelaphus scriptus
Pundamilia Zebra Equus burchelli
Sheshe Puku Adenota verdoni
Simba Lion Panthera leo
Simba mangu Caracal Felis caracal
Sungura African Hare Lepus capensis
Swala granti Grants’ Gazelle Gazella grantii
Swala tomi Thomson’s Gazella Gazella thomsonii
Swala twiga Gerenuk Litocraneus walleri
Swalapala Impala Aepyceros melampus
Tandala Kubwa Greater Kudu Strepsiceros strepsiceros
Tandala Mdogo Lesser Kudu Strepsiceros imberbis
Taya (Kihea) Oribi Ourebia ourebia
Tembo (Ndovu) African Elephant Loxodonta Africana
Tohe- kusi Southern Reedbuck Redunca arundinum
Tohe- milima Mountain Reedbuck Redunca fulvoruvula
Tohe – ndope Bohor Reedbuck Redunca redunca
Tumbili  Vervet Monkey Cercopithecus aethiops

Hadi kufikia hapa utaona karibu majina yote ya wanyamapori yameorotheshwa hapa. Hata kwenye makala ya jana ambayo nilitaja wanyamapori ambao wapo kwenye jedwali la kwanza, lakini pia wapo hata kwenye jedwali la tatu. Uzuri ni kwamba kupitia majedwali haya utajifunza pia hata majina ya baadhi ya wanyama ambao hawajulikani sana majina yao kwa Kiswahili. Hivyo kupitia makala hii naamini kabaisa utajifunza hata majina ya kisayansi ya wanyama hawa. Wanyama hwa wote niliowataja kwenye makala hii ni wanyama wanaofaa kuwindwa au wanaitwa kwa kingereza “Big game” ni wanyama wanaoruhusiwa kuwindwa kwa kibali maalumu. Katika makala ya ijayo nitawataja hapa ndege ambao wapo kwenye jedwali hili la tatu  sehemu ya tatu.

Ahsante sana kwa kusoma makala hii, naamini utajifunza na utajua, karibu kwa maswali maoni na mapendekezo. Asante sana!

Hillary Mrosso

Wildlife Conservationist

+255 683 248 681/+255 742 092 569

hillarymrosso@rocketmail.com

www.mtaalamu.net/wildlifetanzania